Wanaume waficha Wallet/pesa wakifika home.why? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume waficha Wallet/pesa wakifika home.why?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Gaga, Feb 9, 2011.

 1. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Leo kabla sijarudi home nilikaa na marafiki kama sita mahala kupoteza muda ,kuna mmoja wetu akasema mume wake kila akifika home anamwangalia kama mkewe kalala na yeye anajifanya kalala. kwa vile giza anamwona mumewe anahangaika kuficha wallet hadi sometimes chini ya kapet, chooni na wakati mwingine chini ya kitanda.

  wakiamka asubuhi mke anamwambia mumewe kuna vitu vinahitajika kununua mume anamwoshesha kwenye dressing table kwamba ana kiasi kile tu anachokiona, wakati mwingine akirudi na akianza kukoroma yule dada anaangalia kule alikoficha anakuta anazo pesa, then anaacha vilevile,akiamka akimwambia majukumu majibu ni yaleyale kujifanya hana pesa wakati anazo.

  Mimi niliona kitu cha ajabu sababu unafichaje halafu chumbani, kwa nini usiache kwa gari au ofisini.Wadada wawili walimuunga mkono wakasema ni kweli wanaume wengine wanatabia hiyo hadi mmoja wao aliamua kumfundisha adabu mumewe alipoficha tu yeye akachukua zote kulipokucha wanaenda kazini anamwona anatafuta akauchuna hadi jioni ndio alimrudishia na kumwambia amwamini asiwe anafichaficha pesa au wallet
  sasa swali langu kwa wanaume wa jf ni kweli huwa mnafanya hivyo? na mnafanya kwa manufaa ya nani?Ni nini kinapelekea mtu kuamua kufichaficha kihivyo
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Duh tunajifunza kila siku, kweli watu wanaishi maisha ya tofauti, hao kina dada na wenyewe wanafanya kazi au ni mama wa nyumbani.., na je bajeti zao zinaendana na kipato cha waume zao?
   
 3. LD

  LD JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Haya Gaga ngoja tusubirie watuambie kama ni kweli na kwa nini wanafanya hivyo.
   
 4. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,367
  Likes Received: 3,201
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna haja gani ya kutembea na kiasi kikubwa kwenye wallet badala ya kuacha benki, unachukua kiasi kidogo tu. ATM ni 24 hrs, tena wengine tunaamua kuwa na account/benki zaidi ya moja, ikikorofisha hii unaenda benki nyingine.

  Kwa nini wanaume wanaficha; Unajua kuna wanawake wakiiona mme ana hela basi inakua taabu atatunga matumizi hata ambayo hayakuwepo ili hela imtoke mme.

  Mimi sharti langu mke asiniambae kitu kinachohitaji hela kubwa ghafla bali aniambie jioni au asubuhi ili jioni inayofuata nije na hiyo hela. Kwa vitu vya hela ndogo ndogo hamna shida si nakuwa nayo kwenye wallet na wala sifichi.
   
 5. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,367
  Likes Received: 3,201
  Trophy Points: 280

  Tafadhali naomba uchangie maana kwenye thread fulani umesema wewe ni MWANAUME ila unatuzuga na avatar ya kike
   
 6. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Anaficha halafu anapeleka wapi?? hili swali zito ngoja tuwaachie mnaolala wawili!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,596
  Likes Received: 82,152
  Trophy Points: 280
  Hii kali hahahahahahah miye nilidhani njemba zinaficha pochi zikiwa na CDs tu kumbe hata na wake zao hahahahahahah...Kweli hizi ndoa zina mambo LOL! Sasa ni hapo mke baadaye anainuka anaenda kuhamisha michuzi yote kwenye pochi halafu anakula kobisi hahahahahah...Njemba ikiamka asubuhi na kukuta pochi haina ngawira kutazuka valangati la kufa mtu LOL!

   
 8. LD

  LD JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ChapanaloJr unajua kumeza!!! Mmmmmh nitakupm basi tuongee vizuri.
   
 9. M

  Mantisa Senior Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndoa za siku hizi zina mambo sana. Wanawake wamekuwa hawatabiriki kabisa. Anafanya kazi nawe unafanya kazi ila hela yake huioni. Utasikia tu hana hela baadae unastuka kumbe anamjengea mama yake kwao na nyie hata kiwanja hamna
   
 10. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Afadhali cc tunaficha fedha na tunahudumia familia, fedha ya mwanamke ukiiona siku hiyo ufanye sherehe.
   
 11. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kapos kama izi wanakuwa wameopoana kwenye baa ama!?
  Spati picha aisee.
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  dah,ndoa hzi!zna v2ko kweli!
   
 13. E

  Edo JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Na kwa nini nyie muangalie kama wanaume wanaficha? jua alishalizwa ndo maana anakuwa makini (sio kuficha)!
   
 14. loveness love

  loveness love Senior Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natmani nimpate mume wa kuficha pesa zake alafu, nikimchabo tu!! Imekula kwake na lazima ajute kwani mie ndio nitakua nampa kama ni ya matumizi au nauli. Au simpi kabisaaaa!!!! kwa uzembe wake.Ila nitamuambia nimeokota wallet so usinipe pesa ya matumizi mpaka nitakapo kuambia.:clap2:
   
 15. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wewe unaionekana utakuwa mjinga fulani hivi....zuzu hivi....unapoteza muda? ndio maana unakuja na thread za kishwaini asubuhi asubuhi...shame on u....
  .....na mtakuwa watumwa wa wakenya na wahindi mpaka muote sugu makalioni....pambafu kabisa.....
   
 16. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Inategemea na mke mwenyewe yukoje maana wengine wana tabia ya kuficha pesa au kuleta mahitaji kibao binafsi akikuta wallet imejaa. Mimi kwa kweli wife wangu anapohitaji pesa namwambia tu kaangalie kwenye wallet maana sina cha kumficha. Tunaplan pamoja maisha na yuko reasonable sana.
   
 17. Runner

  Runner Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ya kuficha pesa kwa wanaume inatokana na tabia ya baadhi ya wake zetu,huwa hawana matumizi mazuri ya pesa...hata ukimpa kiasi gani cha pesa zinaisha siku hiyo hiyo,kesho tena atataka nyingine,sasa inabidi kufichiwa ili tena kesho apewe nyingine
   
 18. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo wanawake hawajui kama kuna kesho wanataka kutumia pesa yote leo kwa matumizi yasiyo na tija. Tunaficha hizo pesa ili zitumike kesho. Mwanamke anaweza taka kutumia pesa zote leo na kesho akataka pesa nyingine
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,815
  Trophy Points: 280
  Eee Mungu nisaidie nipate garrrrrr,
  Niweze ficha hela kwenye garrrrrr,
  Manake waifu hana mamlaka na langu garrrrr,
  Tunanyanyapaliwa si tusio na magarrrr,

  Garrrrrr garrrrrrr garrrrrr garrr yangu.
  Nakupenda sana garrr,
  sina hela ya kununua garrrr,
  naficha hela ili ninunue garrrrr,
  Halafu nifiche hela kwenye garrrr.....
   
 20. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  :first:
   
Loading...