BOB LUSE
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 3,738
- 3,198
I greet you all my elders,
Hizi sehemu ni maarufu kwa wanaume wenye vipato vya kati na matajiri huenda
kufanya scrub, kunyoa, steamer, kuweka black, mask/facial etc ili kupendeza na
kwenda na wakati,ni jambo jema.
Kule ndani kwenye hizi saloon kuna vyumba maalum vya kuosha nywele baada ya kunyoa na hizo huduma nilizozitaja hapo awali.zote zinatolewa na hawa wadada ambao nawapongeza kwa kazi yao nzuri iliyotukuka.
Kuna baadhi ya wadada katika kutoa huduma hizi wanatumia madhaifu ya wanaume kutomasa wanaume maeneo wanayoyajua kuwa yanaweza kusababisha mwitikio chanya wa malengo yao (invitation to treat) Upande mwingine kuna wanaume wanaingia humu kwenye vyumba hivyo na tabasamu na vicheko bashasha wakiwa na nia ovu ya kukonga
roho na vimwana wa hizo saloon, wana hakikisha wakitoka hapo anachukua namba ya mdada na kupanga kuvunja amri ya sita.
Wakaka wa saloon wanajua hilo na wanawatumia hao wadada kama chambo ya kuwakamata na kulinda wateja.Wanawaambia wanaume chagua unayetaka akuhudumie! lakini tatizo lililopo wanaume hawajui kuwa kila mwanaume anayeenda pale anapewa
huduma kama yake!
Ushauri sio sheria jiheshimu na kuwa serious ukienda sehemu hizo pia wadada wa saloon, acheni tabia ya kugawa namba za simu na kuwatega wanaume heshimu kazi zenu hiyo ni ajira kama zingine, msishushe thamani ya kazi na utu wenu.
Nakaribisha wenye uzoefu na hii sector.tuwarudishe kwenye mstari baadhi ya ndugu zetu waliopinda.
Week end is over kesho ni . . kula kwa jasho.