FisadiKuu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 8,337
- 13,656
Hapana...umeenda mbali mno.
Nachosema ni kwamba, humu watu hujenga taswira za watu kulingana na jinsi ambavyo watu wanachangia.
Sasa, watu tuna backgrounds tofauti tofauti.
Binafsi nimeshaambiwa eti kulingana na mambo ambayo huwa ninayaandika humu basi ni lazima nitakuwa nimekula chumvi nyingi ya kutosha, yaani mzee flani hivi.
Watu hudiriki hata kudai eti nina miaka 60 na kwenda juu [umri wa mama yangu mzazi huo].
Jana tu kuna mtu kanijia PM eti anadai nina mtoto wa kike ambaye ana Master's degree na nina mke mwenye PhD.
Kweli, mtoto ninaye tena wa kike, lakini hata grade school hajamaliza. Ila mke mwenye PhD? Where the hell did that come from?
Basi watu wanadhani vitu niandikavyo humu [sijui hata ni vitu gani hasa] haviwezi kuandikwa na kijana. Ni lazima viandikwe na mtu mzima, mzee mzee hivi.
Ambacho wanashindwa kuelewa ni kwamba, watu tuna backgrounds tofauti sana humu. Mazingira niliyokulia ndiyo yaliyonijenga.
Watu tumeanza kusoma World Book Encyclopedia tukiwa shule ya vidudu, wamekuja akina Edward Seaga na Siaka Stevens tukabebwa kwenye mabega na washua tukaenda Nkrumah hall kuwasikiliza....hapo hata kusoma vizuri sijui....lakini ni mambo ambayo mpaka leo nayakumbuka.
Ndo maana nikizingumzia habari kama hizo watu wanadhani mimi ni kibabu.....hahahaaaaaaa.
Only if they knew....
Hahahahaha dude si unajua mambo ya mitandao.. Sema una mikogo flani ambayo unawakomesha nayo sana wala vumbi.. Hahahaha