Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,662
Onyo: Tafadhali comment kistaarabu/responsibly.
Zamani wakati nakua nilijionea jinsi watu hasa akina dada na vijana walivyokuwa wanafanya juhudi kuzamia nchi mbalimbali, hasa South Africa, UK na baadhi ya nchi za Scandinavia, zikiongozwa na Sweeden na Norway. Binafsi nina kumbukumbu ya wanawake 2 ambao walitoroshwa na wazungu waliokuja kutalii, mmoja kwenda Norway mwingine Sweeden kutokea. Hao wanawake walikuwa wameolewa na wana watoto. Mmoja hadi hivi karibuni amekuwa akituma vitu hadi magari yanakuja kwa mmewe aliyemtelekeza, sijui walikula dili kuibia mzungu au vipi! Nawafahamu akina dada waliotokomea UK kwa kutoroshwa na wazungu au kutokana na tamaa na wengine kwa dili za kimagumashi, lakini wakaishia kuolewa na wanigeria au wakongo, ndoa pia hazikudumu, sasa ni mwendo wa stress tu.
Sasa kuna rafiki yangu alikuja bongo kutoka USA mwaka jana, mwezi wa 12, alah, jamaa anachati na wanawake kama 20 hivi! Nilimshtuka, kwa sababu wakati tukiwa tunapiga story anakuwa busy sana na simu, anarusharusha maneno kama vile haelewi mada, ndio baadaye kaniambia napata shida hapa kuna wanawake wamenizonga wengine wake za watu! Nikamwambia mmefahamianaje? Akasema kupitia social media. Jamaa alivyonionyesha msgs wakichati nikasema, God come back soon! Wanawake wanajilengesha kila mmoja anamtaka jamaa. Nikamwambia jamaa yangu utaingia mkenge, kuwa makini, utang'ang'aniwa na limwanamke halina nyuma wala mbele, wengine kama ulivyosema ni wake za watu. Kwa hiyo jamaa akawa anawapiga sana chenga, kama vile niko busy au nina siku chache tu nataka kurudi halafu mambo mengi. Yaani wanawake walikuwa wanajiliza, mfano "Nyani Ngabu yaani unaondoka hivihivi bila kuonana na mimi, haya bwana, sawa".
Hii hali haikusihia hapo, juzi nipo na jamaa yangu mwingine ni wa USA, namsindikiza kwenda Uhamiaji, alikuwa anaenda kurenew passport, ghafla nikakutana na shemeji yangu mmoja (shemeji asiye na undugu) mitaa ya mjini. Nikamwambia tuna haraka, alivyohojihoji, nikamjibu, namsindikiza jamaa yangu Uhamiaji, anaenda kurenew passport, yeye anaishi USA, ghafla macho yake yakahamia kwa jamaa, mara akamsalimia tena kwa kumshika mkono, alikuwa anaenda uelekeo tofauti akatufuata sasa. Wakati wa kuachana akaniomba namba, nikampa. Dakika kama tano baadaye naona text message "Huyo jamaa ana issue gani USA?", nikamwambia anafanya kazi. Akaniuliza "Ameoa", duh nikajisemea hii mbona sio heshima, nikamjibu bado amesema akipata mke pia anaoa. Oohooo, akajibu, "mwambie aje mimi nipo bwana natafuta mchumba au sio shem". Nikamjibu, na mme wako je, maana kwa kumbukumbu zangu ni kama ulishaolewa? Akajibu, "mtu mwenyewe haeleweki", nikajisemea huyu vipi, nikawa kimya kwa muda, baadaye akajibu, "Kwanza mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama, shangaa". Nilipigwa butwaa, nikamjibu nitamwambie akutafute, akajibu "Kama vipi nipe namba yake". Niliishia hapo.
Sasa wanaume wa USA mna nini? Mbona wanawake wanapagawa sana na nyie, kwa nini? Mfano, baharia kila leo ameambatana na lundo la wasichana pamoja na uzee wake wote, kisa aliwahi kutua USA, najiuliza mna nini jamaa zangu nyie? USA kuna uchawi wa kunasa wanawake nchini Tanzania?
USA Baby!