Wanaume wa kiMassai. . .

Hilo la mwanamke kujenga na kutafuta chakula na mmewe akinyeshewa mvua inakuwa kesi sitachangia chochote, mimi nitachangia hili la mwanamme kwenda kuchunga na mkewe kufanya shughuli zingine kama kutafuta kuni, kupika, kukamua na kulea mtoto.

Mimi natoka jamii ya kifugaji na ukulima, kazi ya kuchunga ni kazi ambayo inachukua zaidi ya masaa manane hadi kumi na mbili kwa siku kutegemea na wingi wa majani pamoja na umbali wa maji ya kunyweshea mifugo, ni kawaida kabisa kwa mchunga ng'ombe kutoka saa moja asubuhi na kurudi saa moja jioni, kumbuka hiyo ni shughuli ya kila siku, niambie hapo atapata muda wapi wa kufanya shughuli zingine, lakini suala la kutafuta kuni unaweza kwenda mara moja ukatafuta kuni za wiki nzima, unaweza kuchota maji hata ya siku tatu hadi nne kulingana na wingi wa vyombo vya kuhifadhia maji.

Nikichukulia kabila letu iwe kama case study, kuna kazi ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya wanawake na zingine kwa ajili ya wanaume, mfano kama familia inao wanaume wengi(watoto au ndugu wanaoishi kwenye familia) kazi zao ni kuchunga, kulima na ng'ombe, kujenga ingawa sio kazi ya mara kwa mara, kutengeneza zizi la ng'ombe, kuchinja na kuchuna wanyama, kwenda kuhemea chakula wakati wa njaa, kuchota maji na kwenda mashineni kama ni mbali, kuchimba visima wakati wa kiangazi na kuhakikisha mbwa wamekula, na kama mbwa atabweka usiku au ng'ombe wamevunja zizi na kutoka, kazi ya kutoka nje na kuangalia ni ya mwanamme, kama kuna mayowe yanapigwa kijijini kitu si cha kawaida kimejitokeza bado ni kazi ya mwanamme kujua upine, mishale au mkuli ulipo ili awahi kwenye tukio.

Kazi za wanawake kama wako wengi, kukamua, kupika, kulea watoto, kuchota maji na kwenda kusaga kama ni karibu, kulima mazao ambayo sio mazao makuu ya chakula wala biashara mfano: viazi, kunde, choroko, kukata kuni na wanaume ndo watakaozifuata kwa kutumia wanyama kazi.

Kazi ya kulima kwa mkono kwa maana ya kupalilia pamoja na kuvuna kwa mazao makuu ya chakula na biashara kama Mahindi, Mtama, Pamba na Mpunga hiyo ni kazi ya jamii zote.

Lakini kama familia haina watu wa kutosha ama wanawake ama wanaume si ajabu kukuta mwanamke anachunga na analima na ng'ombe na ukakuta mwanamme anakamua, anapika na amebeba mtoto wakati mkewe kafuata maji au yeye mwenyewe kufuata.

Kwa hiyo huko kwetu usukumani specifically kwa wanyantuzu huo ndo ulikuwa mgawanyo wa kazi, inawezekana hata kwa wamasai nao huo ndo mgawanyo wao wa kazi.
 
lizzy,
mijanaume ....oopphs sorry
wanaume wa kiafrica wengi ndivyo walivyo...
kazi yao kusugua miguu mwaname ndo atafute...
alime, apike, alee
yaani taabu tupu....

usishangae kwa makabila ya walimaji, mume na mke wakitoka shamba(kama mume siku hiyo kaenda kulima) mke atabeba jembe, mtoto, na atapita kuchuma mboga na kuokota kuni, mume atarudi nyumbani asubiri mke apike ale aende kilabuni.... jioni mke na watoto wende shamba............................

umetudhalilisha sana mkuu... sijui kama wewe ni me/ke lakini this is an utter disrespect and totally out of place... it could that you dont know what you are talking about, or you are not exposed to our culture, or probably you are gay... who sometimes separate themselves from men!!

You cant generalize things like that, and you can take any sample in Tanzania kujionea

Hakuna kitu kibaya kama kasumba....
 
Janjaweed usiwe na hasira namna hiyo, hapo kaongelea wanaotoka kwenye makabila tofauti na sio waMassai pekee. Hata kwetu nimewaona hivyo ni jambo ambalo lipo.

RussianRoulette niko napenda kujua na kuelewa mambo mengi hili likiwa moja wapo hivyo kweli karisachi kadogo kanahusu. Binafsi nimeishi na waMassai sana tu kipindi cha utoto wangu, tulikua marafiki nao, familia nazo zilishirikiana kwa yale yaliyowezekana kwahiyo najua ni watu wazuri. Na hili swala la mila na tamaduni zao hazinifanyi niwaone waajabu ila napenda tu kuelewa iwapo wao wenyewe wanaupenda/kubaliana na mfumo uliopo. Nikijua wengi wao wanakubaliana nao basi ntauheshimu hata kama ni tofauti na ambavyo ningependelea mimi, kama sio ntaheshimu kwa wale wanaoukubali na kuwaonea huruma wale wanaoona ni wa kikandamizaji.
 
Last edited by a moderator:
mmasai akisoma hii lazima avunje computer ati akutafute.

Hahahaha. . haya bana.

Masuke najua swala zima la mgawanyiko wa majukumu ila bado nna uelewa tofauti na ulivyoandika wewe. Nikipata nafasi baadae ntaelezea hili kwa kirefu.
 
Last edited by a moderator:
Janjaweed usiwe na hasira namna hiyo, hapo kaongelea wanaotoka kwenye makabila tofauti na sio waMassai pekee. Hata kwetu nimewaona hivyo ni jambo ambalo lipo.
My friend, naelewa nilichosoma....

Its like taking my personal experience na kuanza kusema wanawake ni wh0res, money mongers, sellers of their dignities and untrustworthy creatures.... hata kama ni personal experience au kabila langu si vyema kwani ni generalization

Anyway, nisiwaharibie mood... ngoja nirudi kule kwetu
 
Lizzy, utamaduni, mila, desturi naustaarabu (kama unavyotaka kuwaza wewe) havipimwi kwa mtazamo wa mtu mmoja amakabila ama taifa moja tu. Kwa mfano, mimi sikubaliani na dhana kwamba ili mtuawe amestaarabika ni lazima afanye mambo kama mzungu. Ni vyema ujue kwambamataifa na makabila yanatofautiana katika falsafa ya maisha, yaani utamaduni namfumo wa maisha. Jambo unaloona wewe kuwa la kishamba sio lazima liwe hivyo kwautamaduni wa watu wengine kwa hiyo usiwe mwepesi wa kuwahukumu watu na kuwaonani washamba ama washenzi (wasiostaarabika) kwa kuwa hawafanyi mambo kamaufanyavyo wewe ama kama wafanyavyo watu wengine. Kwa mfano unapozungumzia habari yaujenzi wa nyumba kwa Wamaasai ni jambo la utamaduni tu wala sio uonevu dhidi yamwanamke.Kwa Wamaasai ni jambo la kugawana wajibu tu wala siouonevu dhidi ya mwanamke kama ambavyo makabila mengine ya Kiafrika na wazunguwanavyoweza kutafsiri. Ni ajabu kwamba hata simba dume huwa hawindi; siku zote mwindajini simba jike. Kwa mantiki hiyo mtafutaji wa chakula ni simba jike na simbadume anabaki kuwa mlinzi wa familia! Ieleweke kwamba kazi yaujenzi wa nyumba ya Kimaasai siyo kama ujenzi wa nyumba za kisasa. Sisi Wamaasaihatutumii magogo wala miti mizito kujenga, tunatumia matawi ya miti ambayo simizito na kwa mantiki hiyo pia hatukati miti kama wafanyavyo watu wengine. Hii inasaidiapia kuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Hivyo kazi ya ujenziwa nyumba ya Kimaasai siyo kazi ya kutisha kama kuchunga ng’ombe ambapomchungaji analazimika wakati mwingine kupambana na simba ama wanyama wenginewakali wanaoshambulia mifugo, na ni kwa sababu hiyo hatuwaruhusu wake zetukufanya kazi inayohatarisha maisha yao kwa sababu kwetu sisi mwanamke (mama) ninguzo ya familia. Hapa, kinachohitajika ni kuelewa mfumo wa maisha ya Wamaasaikabla ya kuanza kuhukumu kwamba wanaume wa Kimaasai ni ovyo. Ningalikuwa na muda wa kutosha ningalikueleza mengi but time and scope does not permit. Lizzy, wewe unawezakupambana na simba?
 
Sio sawa kwasababu hajasema 'wanaume wote'. . . amekua specific kabisa, hivyo hoja yake ina ukweli kama yakwako tu kuhusu wanawake isipokua wewe ndie uliyejumlisha wote.
 
Oldarasu kwanza sijawahi hata kufikiria kwamba waMassai ni washamba au sio wastaarabu hata nnapowaona wamefunga rubega na pensi inachungulia kwahiyo ondoa shaka juu ya hilo.

Tukirudi huku kwingine asante sana kwa somo,NIMEKUELEWA ila bado napenda sana kusikia/pata mtazamo wa wanawake ili nijue kama nao wanaona ni sawa kama muonavyo nyie wanaume.
 
Last edited by a moderator:
Dah. . . kumbe waMassai nao wanajua kuFLIRT ehhhh?Hehehe. . nilidhani hayo ni mambo ya watu wa mujini tu.

Nwy siku zote tunasikia na kuambizana kwamba mwanaume ni yule anaeweza kujali,lisha na kulinda familia yake (provide for them). Miongoni mwa watu wanaoonekana wanaume kwenye jamii yetu ni waMassai kwa uhodari wa kuwinda na hata kuua simba kwa mikono, tena wakiwa na mikuki/sime zao ndo kabisa wanaonekana wa ukweliii.

Pamoja na kwamba nimewahi kuishi nao miaka ya nyuma, sikuwahi kujua baadhi ya mila zao juu ya maisha ya kila siku na namna yanavyoendeshwa ila sasa nimejua na ndio nikapata maswali kadhaa juu ya wanaume hao.

Kwanza kabisa hawajengi. Anaejenga ni mwanamke (mke/wake zake), na ole wao mvua inyeshe alafu bwana anyeshewe. . . lazima mama aambulie kibano na aeleze kwanini 'bwana inyeshewe'( in a Massai accent).
Pili chakula anatafuta mama.
Kutwa nikiangalia naona wanawake ndio wanaopita na punda + madumu kwenda kutafuta maji na kuni wanakokujua wao.

Wanaume utawaona wanapita fimbo zao + mbuzi na ng'ombe kupeleka machungani tu BASI. Wakija dukani wanaume wengi ni wanaulizia kiroba na beer. . . wachache sana watataka chumvi, sukari, mafuta, mchele au hata pipi za watoto kuashiria anakumbuka na kujali familia.
Mashine (kusaga na kukoboa) wanaokuja ni wanawake. . .
Kukamua wao. . .
Kupika wao. . .
Malezi wao. . .
Yani wanaume wao ni machungani kwenda kupiga soga huko wakati wamama wanapanda na kushuka na barabara. Kwa ufupi. . .wanalelewa na kutunzwa na wake zao.

Je nao ni wanaume? Au ndo sawa na wale wanaoitwa 'MARIO' mjini? Au yeye sio muAfrika hivyo ule utamaduni wa 'mwanaume wa kiAfrika ni provider' hauwahusu?

Lizzy, umewahi kuangalia The White Maasai? Mimi nimekaa na wamasai kwa miaka mitatu, nimefanya research sana, kwa

ile jamii mwanaume ni kila kitu! Kwao mwanamke ni 'property' kama alivyo ng'ombe au jembe. Anatumika kama chombo

cha uzalishaji. Kwa wale waliovijijini ambapo bado hawajapata kuchanganyika, hata tendo la ndoa kwao sio burudani

ila hufanyika mara chache pale ambapo baba anahitaji mtoto mwingine! Mara chache sana they will do that for pleasure.

Na mara chache sana mwanamke akafurahia tendo la ndoa maana kwanza amekeketwa, pili hakuna maandalizi na tatu

wanatumia miti shamba inayoongeaza ukubwa wa uume kiasi kwamba ukichukulia the two factors nlizotaja mwanamke

anaishia kuumia zaidi. Kumbuka kwamba kuoga kwa mmasai ni option. Katika maboma yao hakuna vyoo wala bafu.

Ile huduma kubwa hufanywa vichakani/porini na yapo mapori ya wanaume na wanawake. Kwa sasa wengi wameanza

kubadilika hasa kwa wale waliokaa maeneo ya mjini na kuchanganyana na watu!
 
ukitaka haki sawa kubali ku act as a man also so usawa ni upi km baba atafanya kila ki2, dem uuuuuuuuuuu
 
Tamaduni zinatofautiana lakini for objective qualities make a man a true man and husband. Love, protection, provision, and decision! You lack one, think careful
 
Dah. . . kumbe waMassai nao wanajua kuFLIRT ehhhh?Hehehe. . nilidhani hayo ni mambo ya watu wa mujini tu.

Nwy siku zote tunasikia na kuambizana kwamba mwanaume ni yule anaeweza kujali,lisha na kulinda familia yake (provide for them). Miongoni mwa watu wanaoonekana wanaume kwenye jamii yetu ni waMassai kwa uhodari wa kuwinda na hata kuua simba kwa mikono, tena wakiwa na mikuki/sime zao ndo kabisa wanaonekana wa ukweliii.

Pamoja na kwamba nimewahi kuishi nao miaka ya nyuma, sikuwahi kujua baadhi ya mila zao juu ya maisha ya kila siku na namna yanavyoendeshwa ila sasa nimejua na ndio nikapata maswali kadhaa juu ya wanaume hao.

Kwanza kabisa hawajengi. Anaejenga ni mwanamke (mke/wake zake), na ole wao mvua inyeshe alafu bwana anyeshewe. . . lazima mama aambulie kibano na aeleze kwanini 'bwana inyeshewe'( in a Massai accent).
Pili chakula anatafuta mama.
Kutwa nikiangalia naona wanawake ndio wanaopita na punda + madumu kwenda kutafuta maji na kuni wanakokujua wao.

Wanaume utawaona wanapita fimbo zao + mbuzi na ng'ombe kupeleka machungani tu BASI. Wakija dukani wanaume wengi ni wanaulizia kiroba na beer. . . wachache sana watataka chumvi, sukari, mafuta, mchele au hata pipi za watoto kuashiria anakumbuka na kujali familia.
Mashine (kusaga na kukoboa) wanaokuja ni wanawake. . .
Kukamua wao. . .
Kupika wao. . .
Malezi wao. . .
Yani wanaume wao ni machungani kwenda kupiga soga huko wakati wamama wanapanda na kushuka na barabara. Kwa ufupi. . .wanalelewa na kutunzwa na wake zao.

Je nao ni wanaume? Au ndo sawa na wale wanaoitwa 'MARIO' mjini? Au yeye sio muAfrika hivyo ule utamaduni wa 'mwanaume wa kiAfrika ni provider' hauwahusu?

Umefanya research juu ya hili?
 
unabahati haupo karibu maana mori yangu ishapanda..yaani wanaume wa kimasai sio wanaume??? wewe unafanya mchezo kabisa na makabila ya watu..
 
Lizzy, umewahi kuangalia The White Maasai? Mimi nimekaa na wamasai kwa miaka mitatu, nimefanya research sana, kwa

ile jamii mwanaume ni kila kitu! Kwao mwanamke ni 'property' kama alivyo ng'ombe au jembe. Anatumika kama chombo

cha uzalishaji. Kwa wale waliovijijini ambapo bado hawajapata kuchanganyika, hata tendo la ndoa kwao sio burudani

ila hufanyika mara chache pale ambapo baba anahitaji mtoto mwingine! Mara chache sana they will do that for pleasure.

Na mara chache sana mwanamke akafurahia tendo la ndoa maana kwanza amekeketwa, pili hakuna maandalizi na tatu

wanatumia miti shamba inayoongeaza ukubwa wa uume kiasi kwamba ukichukulia the two factors nlizotaja mwanamke

anaishia kuumia zaidi. Kumbuka kwamba kuoga kwa mmasai ni option. Katika maboma yao hakuna vyoo wala bafu.

Ile huduma kubwa hufanywa vichakani/porini na yapo mapori ya wanaume na wanawake. Kwa sasa wengi wameanza

kubadilika hasa kwa wale waliokaa maeneo ya mjini na kuchanganyana na watu!

Ronn M nilishaiona . . .nakumbuka sana maisha aliyotambulishwa yule bibie.

Mengine ulosema yanaendana tu na hawa huku. Kwamba mtu anaoa ili ajengewe,atafutiwe chakula, apikiwe, azaliwe, alelewe yeye akichunga ng'ombe na kusubiria mabinti wakue ili aozeshe japo hajashiriki sana kwenye malezi.

Nwy. . .ngoja nione kama wanawake wao wanaona ni sawa au nao wangependa mambo yawe tofauti.
 
Last edited by a moderator:
unabahati haupo karibu maana mori yangu ishapanda..yaani wanaume wa kimasai sio wanaume??? wewe unafanya mchezo kabisa na makabila ya watu..

Hahahaha umeshika mkuki, fimbo,rungu au sime? Unaruka juu huku ukipiga kelele?

mkaliwakitaa shusha bana. . . mie nimeuliza sijasema!!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom