Wanaume wa kiMassai. . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume wa kiMassai. . .

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, May 29, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah. . . kumbe waMassai nao wanajua kuFLIRT ehhhh?Hehehe. . nilidhani hayo ni mambo ya watu wa mujini tu.

  Nwy siku zote tunasikia na kuambizana kwamba mwanaume ni yule anaeweza kujali,lisha na kulinda familia yake (provide for them). Miongoni mwa watu wanaoonekana wanaume kwenye jamii yetu ni waMassai kwa uhodari wa kuwinda na hata kuua simba kwa mikono, tena wakiwa na mikuki/sime zao ndo kabisa wanaonekana wa ukweliii.

  Pamoja na kwamba nimewahi kuishi nao miaka ya nyuma, sikuwahi kujua baadhi ya mila zao juu ya maisha ya kila siku na namna yanavyoendeshwa ila sasa nimejua na ndio nikapata maswali kadhaa juu ya wanaume hao.

  Kwanza kabisa hawajengi. Anaejenga ni mwanamke (mke/wake zake), na ole wao mvua inyeshe alafu bwana anyeshewe. . . lazima mama aambulie kibano na aeleze kwanini 'bwana inyeshewe'( in a Massai accent).
  Pili chakula anatafuta mama.
  Kutwa nikiangalia naona wanawake ndio wanaopita na punda + madumu kwenda kutafuta maji na kuni wanakokujua wao.

  Wanaume utawaona wanapita fimbo zao + mbuzi na ng'ombe kupeleka machungani tu BASI. Wakija dukani wanaume wengi ni wanaulizia kiroba na beer. . . wachache sana watataka chumvi, sukari, mafuta, mchele au hata pipi za watoto kuashiria anakumbuka na kujali familia.
  Mashine (kusaga na kukoboa) wanaokuja ni wanawake. . .
  Kukamua wao. . .
  Kupika wao. . .
  Malezi wao. . .
  Yani wanaume wao ni machungani kwenda kupiga soga huko wakati wamama wanapanda na kushuka na barabara. Kwa ufupi. . .wanalelewa na kutunzwa na wake zao.

  Je nao ni wanaume? Au ndo sawa na wale wanaoitwa 'MARIO' mjini? Au yeye sio muAfrika hivyo ule utamaduni wa 'mwanaume wa kiAfrika ni provider' hauwahusu?
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  lizzy,
  mijanaume ....oopphs sorry
  wanaume wa kiafrica wengi ndivyo walivyo...
  kazi yao kusugua miguu mwaname ndo atafute...
  alime, apike, alee
  yaani taabu tupu....

  usishangae kwa makabila ya walimaji, mume na mke wakitoka shamba(kama mume siku hiyo kaenda kulima) mke atabeba jembe, mtoto, na atapita kuchuma mboga na kuokota kuni, mume atarudi nyumbani asubiri mke apike ale aende kilabuni.... jioni mke na watoto wende shamba............................   
 3. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Acheni kuchunguza chunguza kila mtu ana mila yake.
   
 4. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,393
  Likes Received: 6,576
  Trophy Points: 280
  hili ni kama tusi kwa jamii ya kimasai.u r totaly wrong..na ninawasiwasi kama umeichunguza vyema hii jamii ya kimasai..labda umesikia hadithi tu..kutoka kwa watu..
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nimeona mwenyewe maana niko katikati yao. Wewe kama unaona niliyoona sijayaona vizuri basi jaribu kunipa picha tofauti.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  BT kama ulikuwepo vile. . .
  Alafu bado utakuta nao wanajiita kichwa cha familia, wakati utendaji wao sawa na wa mkia!!!
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Lizzy hii sikuwahi kuijua wala kuifikiria ingawa nilikuwa ninaona maisha ya aina hii ndani ya jamii hii ya kimasai. Ila kama ni mila zao sidhani kama ni kitu cha ajabu pengine ni kutaka kugeneralize maisha yawe mamoja. hahah yaani tutake atakavyoishi John Mkilanga ndivyo anavyotakiwa kuishi Laizer Alaileyoo huko Mang'ati!

  By the way ninasikia kuwa hawa wanajua kupenda teh teh teh
   
 8. B

  BARRY JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 362
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Masai ni jamii ya binadamu lakini siyo watu
   
 9. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  na bado akirudi kutoka kilabu usiku, anataka mchezo, tena game heavy! tufiakwa, najitemea mate kifuani, its beter to stay single!
   
 10. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 1,262
  Trophy Points: 280
  ..aisee hii..ni Documentary tosha...umenipa idea . Lizzy
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Miaka 100 iliyopita hata Ulaya walikuwa hivi hivi ndio dunia ya zamani ilivyokuwa. Hapa Pemba wanaume wanalazimisha wake zao wajamiiane na Muarabu ili azaliwe mtoto mweupe, walio weusi wanajutia kwa nini bibi zao nao hawajabakwa na Waarab enzi hizo, Mashehe usiku kucha na ngazi kupiga chabo
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Nitarudi kutofautiana na Lizzy kwa asilimia fulani.
  Nitafanya comparison na wasukuma, yote yakiwa makabila ya wafugaji japo wasukuma na ukulima upo.

  Kwa kifupi, wanamme haswa!

  Nimerudi Lizzy kama nilivyokuahidi.

  Kwanza kabisa kila jamii ina mgawanyo wake wa kazi kulingana na mahitaji yake na kazi hizo zimegawanyika kulingana na vipaumbele.
  Sijakaa umasaini lakini kwa mtizamo wa kifugaji na ukizingatia kwamba wamasai kwa asili ni wafugaji tu kwwa hiyo kwao mifugo ndio ilikuwa 'resource' kubwa ya familia.

  Na nikiangalia jiografia ya maeneo ambayo wamasai wanaishi ni maeneo yaliyo karibu na mbuga za wanyama. Nikizidi kuaangalia ufugaji wa kimasai ni ule wa kuhama hama na si wa kutulia eneo moja ili kutafuta malisho na maji kutokana na wingi wa mifugo waliokuwa nayo.

  Basi kulingana na sababu hizo hapo juu jukumu kbwa la mwanamme wa kimasai ilikuwa ni kulinda mifugo kati ya wanyama wakali pamoja na kuwinda, nadhani ndio maana wao wana courage hata ya kupambana na simba. Kwa hiyo majukumu mabayo kwao yalionekana marahisi kama kusaga, pika, jenga nyumba waliachiwa wanawake.

  Nikiwalinganisha na wasukuma kidogo kuna utofauti sababu hawa ni wafugaji na wakulima.
  Nadhani ndio maana wao wana makazi ya kudumu, na kwa kuangalia jiografia hawako mbugani kwa hiyo nguvu iliyo kwenye ulinzi ni ya wastani.

  Hii imefanya kazi za kuchunga, kujenga nyumba(permanent) ni za wanamme. Kilimo ni 50/50 japo napo kuna mazao ambayo ni jukumu la baba(nafaka na pamba) na ambayo ni jukumu la mama(viazi na mboga) japo wanafanya kazi kwa pamoja

  Wasukuma hao hao, walio mpakani na wamasai na wakurya mara nyingi walikuwa wanajikuta wanapigania mifugo, katika maeneo hayo (nadhani maeneo ya Bariadi) utakuta jukumu la kuchunga ni la na kukamua waliachiwa akina mama. Hii nadhani ilitokana na wanamme hao hao wa kisukuma kugawa nguvu zao zingine katika ulinzi wa mifugo uliotokana na wizi wa wakurya na wamasai.

  Kwa hiyo kwa wanawake wa kimasai kufanya kazi hizo sioni kama wanamme wao si wanamme sababu kwao kipaumbele kilikuwa kwenye ulinzi.

  Nikupe tu mfano: Maeneo ya pwani kuchinja kitu chochote si kazi ya mwanamke hata kuku, wakati kwa wasukuma kuku anachinjwa na watoto wa kiume au mwanamke anayepika sababu kuku hakuwa kupaumbele naye kuwa ni mnyama wa kushughulikiwa na mwanamme mkubwa. (warining: ukija kwangu ukala kuku jua nimenchinja mwenyewe)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wamasai wamegawa majukumu kwa kila mtu wa jamii zao,hivyo kuona shughuli za mwanamke ni nyingi sio kweli kwani Mwanaume wa kimasai kwa shughuli ya uchungaji wa wanyama ni ngumu kweli kweli sababu huko porini mara wakutane na wanyama hatari.
  Hivyo usidharau mila na utamaduni kwa niwatu wazima walio anzisha Mila hizi.
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 15. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 16. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Huku ZNZ ni kinyume chake.
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hhhmmm. . .kama kupenda kwenyewe ndo huko kwakufanyishana kazi kama punda I think i'll pass.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Usisahau tu kunitaja kwenye hiyo Documentary mtu chake .
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  We Kongosho juzi tena ulisema utarudi sikukuona.

  Pharaoh . . .duh. . .kweli kazi wanayo.


  Pori gani wakati wanachunga mi nawaona? Kungekuwa na wanyama wakali hapa karibu hata mimi ningekua hatarini. Kwenye wanyama ni hukoo mashambani, sehemu ambayo hawawezi kuchunga maana wanyama wataharibu mazao ya watu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Kipaji Halisi

  Kipaji Halisi JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 2,263
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  ....ucjari..nitakutaja...ni kijiji gani hiko..nipate kwa kuanzia..
   
Loading...