Wanaume tusiwe hivi

Wanaume tusiwe hivi

Umenikumbusha mwaka 2010 mtaa wa ohio dar es salaam..mida ya 11 jioni Nikamuona mwanaume mmoja almost kama 42 yrs akiwa anampiga makofi na mateke mwanamke mbele za watu mpaka akawa anavuja damu hakuna mtu aliyetokea kuwaamua, yule mwanaume alionekana amejazia Bausa. Baadae akachukua taksi na na kumwingiza yule mwanamke ndani kwa nguvu. Taksi ikaondoka mwendo kasi kupitia alihasani Mwinyi road

Kile kitendo kiliniumiza sana, katika maisha yangu nachukia uonevu na udhalilishaji. Kijana nikajitosa kichwa kichwa nami nikachukua taksi nikawa nyuma yao kama gari 3 hivi. Tulivyofika palm beach hotel kukawa na foleni kubwa nikashuka nikakimbia kwa miguu mpaka salenda police station nikaripoti tukio. nikapewa askari polisi 2 wenye silaha, ikawekwa road block pale salender, ile gari ilipofika ikaelekezwa iingie polisi station.

Wote wakachukuliwa nikiwepo na mimi, kumbe walikuwa mtu na mkewe! polisi wakaajitolea kumpeleka yule dada hospital akafungwa majeraha. Wakati huo yule bwana na mie tuko chini ya ulinzi..Yule dada amerudi almost saa 2 usiku, bwana akafunguliwa file la udhalilishaji, kupigana hadharani na kusababisha majeraha

Mashtaka yule mume anamshutumu mkewe ni malaya, kesi ikanigeukia mimi mume ananishutumu mie ni bwana wa yule mkewe, ukweli sikuwa nawafahamu hata kidogo. Huwezi amini niliwekwa lockup mpaka saa 8 usk, wakaja kudhaminiwa na ndugu zao wakaachiwa wote mie nikabaki lockup kumbe yule dada hakuondoka pale kituoni akarudi akanidhamini nikaachawa,dada akanikodishia taksi akanisindikiza mpaka getho kwangu ilala..

Kesho yake nikaripoti polisi baadae wakadrop ile kesi nikawa huru. Yule dada akawa ananipigia simu kunishukuru mwishowe it become happy ending........(dhambi ya happy ending nimeshatubu na kuacha.)

Ila Wanaume tutambue kabisa pshychological kumpiga mwamke unajidhihrisha wazi kwamba uwezo wako wa kufikiria ni mdogo kupita kiasi mpaka unaamua kutumia nguvu.. Lets be a real MAN
Ukamtafunia baunsa kitumbua chase ha ha ha
 
Mwanamke kwanini ukubali kupigwa hivyo, kwani huyo mwanaume umezaliwa naye, kwenu sikupo uende. Pole yake huyo mwanamke mwenzetu
 
nikweli kabisa... halaf pia amna mtu ambae hakosei na kwa mtu timamu akirekebishwa anaelewa....sio kwenda kudhalilishana mtaani
Nachukia sana tabi a hiyo.Wak ati umempenda unataka awe mke wako unambembelezaaaa wee akishafika ndani una mgeuza ngoma ya mnanda siyo ishu,hongera kwa watu ambao huwa wanawashughulikia kwa vipigo wanaume wenye tabia hiyo.
 
Wakuu,

Habarini!

Leo katika mtaa fulani, nimeshuhudia mwanamke mmoja akipigwa kwa ngumi na mateke na mwanaume mmoja. Baada ya kusogea karibu nijue tatizo nini kumbe walikuwa ni wana ndoa, vijana waliokuwepo maeneo yale ikabidi wamkamate yule mwanaume na kumpa kisago kama mwizi.

Yule jamaa baada ya kupewa kisago kitakatifu, akaanza kujitetea kwamba ni mke wake, vijana wakamwambia kama ni mkeo kwa nini uje kumdhalilisha huku mtaani badala ya kumalizana nyumbani, hivi ninavyoongea huyo kijana kapakizwa kwenye toroli anapelekwa kituo cha Polisi, maana hawezi kutembea kabisa na waliompa kisago wamesepa, pia na mkewe nae katokomea kusikojulikana.

Wanaume, kama tuna mifarakano katika ndoa ni bora kuzikontroo hasira zetu, na ikiwezekana tuyamalize nyumbani na sio kuwapa faida wengine mitaani.
Point
 
Wanaume wenginr wajeuri wanajifanya wajuaji sana. Amepata stahiki yake. Unapiga mtu ruhusa unaipata wapi? A man who beats a woman is an idiot a really stupid idiot. A coward who cannot fight anothet man!!!
 
wanaume wengine bure kabisa ambayo hayawahusu nyie ndo marefarii sasa hayo hayawapi hela, chakula, kodi za nyumba, matibabu, ada za shule, luku na mengineyo embu yaacheni ya watu msipende umbeya haunaga mshahara. Unataka utoe msaada baada ya siku watu wamerudiana achaneni na ya watu

Duh! Kweli binadamu tumetofautiana sana, kwahiyo mkuu wewe mwanamke, anaweza kupigwa na hata kutiwa kilema mbele yako na usichukue hatua yoyote ?
Let's say ndio angekuwa dada yako anadhalilishwa hivyo wewe ungechulia poa?
 
Huyo mwanaume Angetakiwa avunjwe miguu yote wako wanaume wakorofi wanapiga wake zao kama watoto kisa Wana nguvu na wanawake nguvu zao kulia acha na yy aisome namba mana hapo nikuzalilishana
 
Huyo jamaa simkubali... siku hizi ni bastola tu..
 
Back
Top Bottom