kwetumasoko
JF-Expert Member
- Aug 24, 2016
- 866
- 518
Wakuu,
Habarini!
Leo katika mtaa fulani, nimeshuhudia mwanamke mmoja akipigwa kwa ngumi na mateke na mwanaume mmoja. Baada ya kusogea karibu nijue tatizo nini kumbe walikuwa ni wana ndoa, vijana waliokuwepo maeneo yale ikabidi wamkamate yule mwanaume na kumpa kisago kama mwizi.
Yule jamaa baada ya kupewa kisago kitakatifu, akaanza kujitetea kwamba ni mke wake, vijana wakamwambia kama ni mkeo kwa nini uje kumdhalilisha huku mtaani badala ya kumalizana nyumbani, hivi ninavyoongea huyo kijana kapakizwa kwenye toroli anapelekwa kituo cha Polisi, maana hawezi kutembea kabisa na waliompa kisago wamesepa, pia na mkewe nae katokomea kusikojulikana.
Wanaume, kama tuna mifarakano katika ndoa ni bora kuzikontroo hasira zetu, na ikiwezekana tuyamalize nyumbani na sio kuwapa faida wengine mitaani.