Wanaume tunatia aibu, inakuwaje mwanaume unafanya haya!

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,017
Asalam aleykum

Wakati tunaendelea kujikinga na ugonjwa wa Covid-19. Naomba kutoa maoni yangu. Uyachukue au uyaache lakini ukweli u-prevail.

Kihistoria ya human evolution toka maisha ya enzi yaani early stone age , middle stone age na late stone/ iron age binadamu akipitia ktk hatua mbali mbali za maendeleo Mwanaume amekuwa na wajibu ufuatao ktk familia na ktk jamii.

1. Kuilinda familia na jamii dhidi ya maadui yaani wamyama wakali na binadamu wabaya.

2. Kuhakikisha familia inapata mahitaji muhimu kama malazi, chakula na mavazi.

3. Kumtunza, kumkanya, kumuadadabisha na kumfundisha mke adabu njema. Watoto wawe na heshima n.k.

4. Kudumisha upendo, umoja na mshikamano ndani na nje ya familia.

Wajibu hizi ndizo zinazomtofautisha mwanaume na mwanamke kutoka enzi hizo hadi leo nyakati hizi za utandawazi na maendeleo makubwa ya kijamii, sayansi na teknolojia.

Hata leo hata ukiwa muuza mkaa na mkeo ni mwalimu bado atahitaji vipesa vyako vya kuunga unga umunulie nguo na kutoa matumizi ya familia. Tusalamike kuwa wanawake ni wabinafsi ndivyo nature ilivyo na ndio wajibu wetu. Kumbuka concept ya Alpha Male.

Sasa mambo ya ajabu ya leo kwa mwanaume na naomba abadilike ili tuendeleze heshima yetu wanaume kwenye familia na jamii.

1. Inakuwaje mwanaume unaoa mke na unamwacha?? Yaani mke uliyemtongoza mwenyewe ukiwa na hisia kali za kimapenzi inafika mahali unasema sasa basi?? Kweli?? Nini kinatokea ambacho kinakushinda ku-control??
2. Umezaa na mtoto wa kike uliyemfata kumtongoza na kumgegeda kwa raha mstarehe leo anapata mimba unaanza visingizio mpaka unatelekeza uzao wako??

3. Mwanaume wa leo una roho gani hadi huna upendo? Unaanza vipi kukaa mbali na mwanao/ wanao uliowazaa?? Mnajua kuwa sisi tunapaswa kuwa na huruma kuliko wanawake??

Wanaume tubadilike. Tuwe na tabia za kiume. Kutelekeza familia kwa visingizio vinafanya wanawake sasa wanatupanda vichwani tusiruhusu hili. Tulinde heshima.yetu.

Karibu kuchangia mambo mengine ya ajabu na toa suruhisho cha kufanya tuokoe familia tuendeleze upendo.
 
Yote uliyosema yana viukweli fulani ila hujakutana na wanawake pasua kichwa wewe aisee ye ye ye ye ye .........

Utajuta na hautakuwa na option zaidi ya kuachana nae hata kama wewe ni jemedari vipi na uanaume wako
 
Usitukane mto, wewe upo kwenye penzi jipya au mahaba tu yamenoga, huwa akili zinaendaga likizo...na usia dike ukiwa na muhemko, calm down babu
 
Majukumu yetu na wao wanataka yawe majukumu yao!

Majukumu yao pia wanataka yawe majukumu yetu, kitu ambacho hakiwezekani. Wenyewe wanakwambia "haki sawa"
Sasa haki sawa kweli wataweza kusukuma mkokoteni pale kariakoo kifua wazi kama vidume?
 
Yote uliyosema yana viukweli fulani ila hujakutana na wanawake pasua kichwa wewe aisee ye ye ye ye ye .........

Utajuta na hautakuwa na option zaidi ya kuachana nae hata kama wewe ni jemedari vipi na uanaume wako
Ni kweli wapo magume gume yaliyoshindikama lakini mwanamke ni namna unavyomchukulia hakuna kinachokushinda hata we mwajuma.ndala ndefu bado mwanaume umepewa uwezo wa kumcontrol.na akatulia. Hawa wanawake wameumbwa kwa ajili yetu. Tuwatunze na tuwatumie.
 
Majukumu yetu na wao wanataka yawe majukumu yao!

Majukumu yao pia wanataka yawe majukumu yetu, kitu ambacho hakiwezekani. Wenyewe wanakwambia "haki sawa"
Sasa haki sawa kweli wataweza kusukuma mkokoteni pale kariakoo kifua wazi kama vidume?
Hii haki sawa ni muhimu sana tatizo ni interpretation ya hiyo haki. Haki sawa tunataka wanawake wapate elimu, wapewe ajira na uhuru wa kufanya mambo yao kama wanawake. Wanawale waliofanikiwa duniani wanalijua hilo. Wanaheshima kwa wapenzi au waume zao. Wema akimuona DIAMOND nyumbani ni mnyenyekevu mno. Huwezi kudhani kama ni yule wa mitandaoni. Mengine wanafanya kujionesha tu. Wanwake msidate mkumbo wa haki sawa isiyo na tija mnadanganywa.
 
Mkuu, shida kubwa ipo kwenye malezi.

Ninakumbuka enzi zetu watoto wa kiume walilelewa kama wanaume hasa, kama viongozi.

Kule kwetu kwa mfano, ilikuwa ni jambo la aibu mtoto wa kiume kusogelea jiko, kupika, na kufanya majukumu mengine yaliyoonekana ya kike. Pia, mtoto wa kiume alikuwa na mandate na anashirikishwa katika kufanya maamuzi. Alikuwa ni mlinzi wa kwanza wa wadogo zake na watoto wote wa kike katika familia.

Kizazi cha Kikwete na Magufuli ndio hawa wanalelewa kwa haki za binadamu, haki sawa, n.k. Siku hizi ni jambo la kawaida kabisa kumkuta mtoto wa kiume jikoni, ni jambo la kawaida kabisa kumkuta mtoto wa kiume anapika au anaosha vyombo, n.k.

Watoto wa kike nao wamekuja na feminism. Wanafundishwa usawa katika kila kitu. Katika mazingira kama haya, utampata wapi mtoto wa kiume hasa? Utampata wapi mtoto wa kiume ambaye ni mlinzi wa familia? Utampata vipi mwanaume ambaye ni kiongozi?

Mbaya zaidi, utampata wapi mwanamke mtiifu kwa malezi haya ya mazingira ambayo mtoto wa kike anamuona mtoto wa kiume kuwa sawa na yeye?

Shida kubwa ipo kwenye jamii zetu na malezi.
 
Pole kaka naona wameshaanza kukushambulia.
Wakina nani?? Mimi nachukia na sipendi kuona Mshikaji wangu anazaa na mwanadada halafu anamtelekeza hizi ni akili au matope?? Au mtu anazaa na wanawake watatu hadi wanne na wote hajaoa hata mmoja na watito kila mmona anaishi anakojua. Unadhani mwanamke aliyeathirika kama hivi si atatuona wanaume wote mambulula??
 
Umeoa?

Umezaa?
 
Asalam aleykum

Wakati tunaendelea kujikinga na ugonjwa wa Covid-19. Naomba kutoa maoni yangu. Uyachukue au uyaache lakini ukweli u-prevail.

Kihistoria ya human evolution toka maisha ya enzi yaani early stone age , middle stone age na late stone/ iron age binadamu akipitia ktk hatua mbali mbali za maendeleo Mwanaume amekuwa na wajibu ufuatao ktk familia na ktk jamii.

1. Kuilinda familia na jamii dhidi ya maadui yaani wamyama wakali na binadamu wabaya.

2. Kuhakikisha familia inapata mahitaji muhimu kama malazi, chakula na mavazi.

Dogo kuoa/kuacha ni suala LA watu 2
 
Back
Top Bottom