Naomba kusema, wanaume tuheshimiane tena tuheshimiane, tabia ya kuachana na mwanamke lakini huishi kumfuata fuata kwa maneno jiheshimu tena jiheshimu.
Nimechoka na nimekuchoka ndio maana nimekuja kukuambia hapa, kwa kuwa ni member hapa najua utasoma na unajua mimi ni nani.
Nimechoka kukunyamazia, mwanaume gani unakosa busara hata chembe tu? jiheshimu narudia tena jiheshimu.
Huyu mtu mimi nilikuwa kwenye mahusiano nae yapata miaka 7 na tuna mtoto mmoja alikua amefanya taratibu zote za kufunga ndoa isipokuwa tulikuwa bado kufunga ndoa tu.
Tukaja tukashindwana kila mtu akaendelea na maisha yake, wakati wakuvunja mahusiano mimi kama mtu ambaye nilihisi kuchoka.
Niliifahamisha familia yangu na nilitoa sababu zangu ambazo kwa upande wa familia waliamua kumwambia mshenga.
Basi mshenga akapewa taarifa na kwakua mshenga alikuwa anajua habari za huyu mtu wangu vizuri alieleza mengi pia kwa familia yangu hasa ambayo hata mimi sikutaka familia wayajue.
Kutokana na taarifa hizo baba yangu akikasirishwa sana na kuniomba kikao cha pande mbili.
Tulikutana kwenye kikao wazazi wake wakaongea na yeye akaongea, na mimi nikaongea na mshenga akaongea khaa!
Jambo la ajabu yeye akasema "jamani naomba mimi na mwenzangu tutaenda kuyaongea" khaa!
Baba yangu akahamaki na kumwambia kuanzia leo nauvunja huo uhusiano, wewe kajirekebishe na huyu akasome.
Baada ya hapo kama utakuwa umejirekebisha mlango upo wazi nitakukaribisha, kuanzia leo mwanangu yupo chini yangu. tukafunga kikao.
Baada ya hapo yeye alinibembeleza sana nisiachane nae kwakua tuna mtoto na aliahidi angejirekebisha, na mimi roho ilikuwa inaniuma kuhusu mtoto.
Nikawa najitahidi kuwa karibu nae kwakua mtoto nilimwachia yeye mimi nilienda kukaa sehemu nyingine ambayo sikutaka kabisa yeye aijue maana namjua vizuri lakini sikuacha kila wkend kwenda kumuona.
Sasa shida sikuwahi kuona mabadiliko kwa zaidi ya miezi 8, kwanza kila siku ilikuwa afadhali ya jana, mwanaume mgomvi, anamatuasi yaani akilewa ananivua nguo kwa maneno mchana kweupe.
Nikaamua kukaa kimya kwa muda ila mtoto nilikuwa nawatuma wadogo zangu wanaenda kumuona na kumpelekea vitu vya mtoto.
Baada ya muda nikawa nikipiga simu kutaka kuongea na mtoto, hapokei, yaani zaidi ya mwezi simu haipokelewi wala msg hajibu.
Nikaamua kumpeleka ustawi kudai haki yakumuona na kuongea na mtoto, kumbe bwana huyu akavuta jiko wakawa wanaishi wanapika na kupakua.
Kilichofuata ni ndugu zake kunishambulia mimi nakusahau mema yote niliyokuwa nawatendea, kwakua tulichokanaa hiyo siku yeye kaja na timu toka kwao, mimi peke yangu, tukatukanana mbele ya polisi hadi basi, baada ya siku mbili akanipigia simu mimi 'eti niende nikawaombe msamaha ndugu zake kwa kua yeye hataki kuachana na mimi" nikamuuliza kwa lipi?
Eti umewatukana wazazi wake hawana kazi za kufanya, nikamwambia usinitafute maneno, na hilo haliwezekani kamwe, akawa ananitukana sana kwa msg kuna wakati hadi najikuta namjibu.
Nikaa kama mwezi, akaanza tena kunipigia "Ooohh! naomba turudiane," nikamwambia wewe si umeoa?
Akasema mimi naishi tu na huyu mwanamke lakini sina mapenzi wala malengo nae" nikamwambia endelea kuchezea watoto wa watu, huo ni uchafuzi, kuhusu mimi sahau sahau.
Baada ya hapo akaa kimya cha muda lakini jambo la ajabu kaanza tena kunitukana sana kwa msg, kiasi kwamba sielewi ana tatizo gani?
Mimi naishi naendelea na maisha yangu kwa amani lakini yeye kila siku anaishi anawaza kukabiliana na mimi, mimi nimekuchoka na hizi tabia.
Wewe kaa ishi kwa amani yako, niache na mimi niwe na amani yangu, Nilikupa nafasi miaka 7 tena kwa uaminifu mkubwa, uliyoyafanya unayajua vizuri sasa tulia, "usiweweseke kujua kuhusu mimi" na lazima ujue naishi maisha mapya SITAKI STRESS TENAAAA,
Nimekuchoka najua utapita hapa, soma ukimaliza nenda kawasimulie waliokudanganya ukakosa mwana na maji ya moto.