Wanaume tuheshimiane

Wanaume tuheshimiane

Status
Not open for further replies.
Pole dada yangu, wanaume wenye upendo wa dhati tumebaki wachache sana hapa dunia....nawaonea huruma sana jinsi ya kumpata mwanaume mwenye upendo wa kweli na anaejua thaman ya mwanamke.
 
Dizaini kama nakufahamu vile,, kama mwanao yuko kanda ya kat na kufaham kama sio basi nimefananisha matukio.

Anyway Pole sana, mblock tu namba yake. Siku iz kuna app nying ambazo ukimblock mtu anakuw hana uwezo wa kukupata ila wewe ukimtafta unampata. Na hii yote ni kwa sababu unahitaji kuongea na mwanao
 
Baadhi ya wanaume ndivyo walivyo.Akishajua kakupoteza na kila anayemhitaji hafikii quality yako ndo anaanza kuhaha mara matusi.Tena walivyo waajabu anakutaka mrudiane ukikataa matusi kibao na dharau.Chakufanya kaa kimya usiwe unamjibu mbona atachoka japo muda mwingine unashindwa kuvumilia.Omba Mungu na jiepushe naye mana ni mshari.Pole sana mana haya ni mambo ambayo baadhi ya wasichana tunayapitia
 
Hapana hapa unalea tatizo kwa makusudi au bila kujua, tafuta njia nyingine ya kuwasiliana na mwanao

Nimelisha anzisha jaribu kuwa nawatuma wadogo zangu kwenda kumuona mtoto na hata kumchukua, akawa analalamika kwa watu mimi siendi kumuona mtoto wala sipigi sim, pia walikua wanawatreat vibaya sana wadogo zangu wakienda pale, yaani kuna wakati nilibadili line hadi nikahisi kuchanganyikiwa.

Nawaza pia hilo, japo sioni njia rahisi kwa kweli

Muachie huyo mtoto endelea na maisha yako, mtoto akikua atakutafuta tu.

Kumfuatilia ndio kunampa kichwa cha kukutukana.

Ukikaa kimya atarudi kwenye sense zake.


Unajua hua sipendi hata kumpigia hata hivyo hua simpigii hadi niwe namuhita mtoto, kwa hiyo inaweza kupita hata wiki 3 mimi sijui mwanangu anaendeleaje, Lakini pia inanilazimu kumfuatilia maana ni mtoto wa kike n kuna mambo nikiyafikiria huwa nakosa amani kabisa.

mfano, kunasiku nilimuuliza mtoto nani anakusafisha ukienda chooni?? mtoto akanijibu anasafishwa na kaka wa ng'ombe(mfanyakazi wa ng'ombe) nikampigia nikamwambia kwanini mtoto anasafishwa na kaka wa ng'ombe?? hakuonyesha kujali hata kidogo, aliona ni kawaida tu, lakini mimi nilishamfundisha mwanangu kujitegemea kwa kila kitu, sasa sijui ilikuwaje hadi kumruhusu kaka wa ng'ombe kumsafisha mtoto wa kike.

Zaidi wakati mwingine wanaruhusu mtoto wa kike eti alale na baba ake mdogo mwenye umri wa miaka kama 23 au 24 jamani hebu niambieni kweli hawa watu wanaakili kweli???????

Kwakweli moyo wangu una maumivu sana nikifikiria hayo na nipo kwenye mkakati wakuomba nimchukue na niondoke nae mbali kabisa.
 
Matatitizo yalikuwemo zamani toka kwenye mahusiano yenu, bali hukutaka kuyaona au kuyapa kipaumbele. Moving forward, nyinyi nendeni tena ustawi wa jamii mpangiwe zamu za kuishi na mtoto au kutembeleana. Jingine, ni kuwa liweke wazi huo usumbufu wake, ningekuwambia ubadili namba au umblock lakini kwa ajili ya mtoto mwache kwanza.

Ikibidi mtoto uwe unawasiliana nae kwa ndugu zake, huyo kibuti ndo kimemtia kichaaa.
 
Sorry, kwanini hauishi na mwanao? Ana umri gani?

Namuhitaji mtoto hata leo, lakini tatizo ni mtu mwenye roho ya ugomvi nikaona isiwe tabu mtoto huyo mchukue, akamchukua anakaa nae kwa wazazi wake. miaka 5
 
Kisa cha kuja kunitukana hapa ni nini? sasa Dawa yako najiua tuone utafaidika nini.....Mtakao baki duniani siku ya uchaguzi chagueni Lowasa, mwambieni kura moja imepotea kizembe kabisa
 
Matatitizo yalikuwemo zamani toka kwenye mahusiano yenu, bali hukutaka kuyaona au kuyapa kipaumbele. Moving forward, nyinyi nendeni tena ustawi wa jamii mpangiwe zamu za kuishi na mtoto au kutembeleana. Jingine, ni kuwa liweke wazi huo usumbufu wake, ningekuwambia ubadili namba au umblock lakini kwa ajili ya mtoto mwache kwanza.

Yah!!! matatizo yalikuwepo na nilikuwa nayafumbia macho kwa kua nikikua nadhani labda atabadilika, itanipasa niende huko tena. asante
 
Hivi ikituma ujumbe humu ndo bei iko chini kuliko kumtumia yeye kwenye simu yake?..nachojua hapa ni gharama kubwa kuliko sms ambayo ingeingia moja kwa moja kwenye simu yake.
Binafsi naona hata wewe sio mke uvumilivu kwasababu uvumilivu wako unaupimia kwa miaka ya ndoa si kwa kiwango chako cha umri. Namshauri mwanaume.mwenzangu huyo uliyemlenga ujumbe huu "ASIKUJIBU CHOCHOTE" ila akupe.miaka 7 hiyo hiyo..uishi njia zako zote unazozitaka..km MUNGU atawaweka hai, alete mrejesho. nadhani itakuwa nafasi nzur sasa yakujipima busara yako..miaka saba iliyopita..ila kama hutoshindana na nature..basi haya yatakuwa sehemu is majibu yako; 1. Nisamehe ulikuwa ujana,2. Kumbe sikujua km kuna wanaume wabovu zaidi yako 3. Najuta sn .na majibu ambayo kitaalamu tunayaita "negation" ila ninae muhurumia sn ni mwanao atakapoingia mikononi kwa mama wa kambo mwenye roho nyepesi km yako..mwisho wa siku mwanao atachukia wanawake wote kwa ukatiri..kumbe chanza ni wewe kuwa ni mihemko...." AKIRI ZA KUAMBIWA ONGEZA NA ZAKO by horn jk"

Hivi mtu mwenye umri 35 nae tuseme anaujana????????? khaaa!!!!!!!!!! basi kazi ipo.
 
wanawake wa dizain yako Ni kazi Sana kuwahendo...

Trust me....

By the way,huyo jamaa anakupenda Sana...hujajua Tu...

Miaka 7 ilitosha sana kujua hayo unayoyasema.

Nataka nikuhakishie, nilipokuwa nae nilijitoa mimi sana, na tulifanya vitu vya maana sana tu, sasa kapata mke mwema kaona ndivyo sivyo ndio anagundua mimi nilikuwa muhimu kwake, akinipigia nikamwambia ukweli anatukana sasa hiyo akili au matope, yeye kama anaamini mimi nilikuwa mwiba kwake atulie afurahie amani, ila mimi naamini yeye alikuwa mwiba kwangu ndio maana nina amani sasa.
 
Khaaa!!! JF ishakuwa agony aunt,mtu unafunguka watu wakusaidie. inasikitisha tatizo hii story ni one side of the coin,hatujui story ya upande wa pili
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom