Wanaume tuheshimiane

Wanaume tuheshimiane

Status
Not open for further replies.
Hizo msg si ndio tiketi yako ya kumshtaki???????

Heheheh wewe mwanaume wa CHIKITITA umkomeeeeeeeeeeeeeeeee

Hujui kukataliwa

(Loh ingawa hapa tumesikia hadithi ya upande mmoja....shemeji njoo uelezee upande wako)
 
Last edited by a moderator:
Hizo msg si ndio tiketi yako ya kumshtaki???????

Heheheh wewe mwanaume wa CHIKITITA umkomeeeeeeeeeeeeeeeee

Hujui kukataliwa

(Loh ingawa hapa tumesikia hadithi ya upande mmoja....shemeji njoo uelezee upande wako)

hahah nimekuelewa vyema
 
Last edited by a moderator:
Mie nasubiri bwana shemeji apite.....

I hope hatamwagia mvua ya matusi kwa simu

Nilikua sijui ushenga kumbe una kazi ndefu hivi
niliwahi ona mtu anaombwa kuwa mshenga akakataa
kumbe ni shughuli pevu..kusuluhisha migogoro na kutumwa huko na huko kwa wakwe..utasema wanalipwa..
sasa mshenga huyu itabidi atafute na smart phone kama hana ili apate updates...za kesi hii
 
Khaaa!!! JF ishakuwa agony aunt,mtu unafunguka watu wakusaidie. inasikitisha tatizo hii story ni one side of the coin,hatujui story ya upande wa pili

Hakuna hatari kama sms za kawaida, mim msg za kawaida situmii hata maana najua madhara yake.
 
Miaka 7 ilitosha sana kujua hayo unayoyasema.

Nataka nikuhakishie, nilipokuwa nae nilijitoa mimi sana, na tulifanya vitu vya maana sana tu, sasa kapata mke mwema kaona ndivyo sivyo ndio anagundua mimi nilikuwa muhimu kwake, akinipigia nikamwambia ukweli anatukana sasa hiyo akili au matope, yeye kama anaamini mimi nilikuwa mwiba kwake atulie afurahie amani, ila mimi naamini yeye alikuwa mwiba kwangu ndio maana nina amani sasa.

hizi ligi zenu za kipuuzi zinamuumiza mwanenu na sio nyie..

huyo binti yenu analelewa malezi ambayo hastahili kwa sababu nyie watu wazima mliokomaa na hadi mna minywele kila sehemu ya miili yenu mmeshindwa kukaa chini mkatafakari hatima ya malezi ya mtoto wenu..badala yake mnaendekeza mashindano...na sasa mashindano yenu yamehamia huku kwenye social networks..

hivi unadhani hapa JF hakuna watu wenye matatizo kwenye familia zao tena zaidi ya hayo yako?

anyway,hapa unataka tujifunze nini sasa kwa mfano...nia yako ya kuleta hii mada hapa Ni ipi....

Make naona tayari Una maamuzi yako na haupo kwa ajili ya ushauri...

kikubwa...nyie chezeni mdundiko,makirikiri,ligi,but at the end of the day atakayeathirika Ni huyo,binti yenu mdogo....anayehitaji malezi ya Baba na mama kwa pamoja...

All the best Madam.
 
Kuwa mshenga sio kazi ndogo. Kikinuka unaambiwa unaanzia kwa wasimamizi wa ndoa...kisha mshenga....then ndio wazazi.

Sasa mshenga inabidi anunue smartphone ili atumiwe screenashot za matusi ili akusanye ushahidi




Nilikua sijui ushenga kumbe una kazi ndefu hivi
niliwahi ona mtu anaombwa kuwa mshenga akakataa
kumbe ni shughuli pevu..kusuluhisha migogoro na kutumwa huko na huko kwa wakwe..utasema wanalipwa..
sasa mshenga huyu itabidi atafute na smart phone kama hana ili apate updates...za kesi hii
 
Huyo mwanaume atakuwa sio mzima kabisa akapimwe akili.

Toka lini mtoto wa kike akasafishws na mwanaume? Au akalazwa chumba kimoja na mwanaume????

Anataka mtoto abakwe???

Hivi ana akili timamu kweli huyo?

Nakushauri tafuta utaratibu kisheria umchukue huyo mtoto. Kuna mijanaume mipumbavuninaona fahari kujivunia kuwa na watoto ilhali kulea haiwezi.

Sorry swala hili kama mzazi limenipa hasira.









Wewe mwanaume kama unapita hapa jirekebishe. Utamlazaje mtoto na janaume? Una nia na malengo gani na huyo mtoto???

BADILI TABIA unampa mtu ushauri ambao hauhitaji na japo huyo baba mtu pengine anastahili lawama kwa kiasi fulani lakini sio kwa asilimia zote kwasababu pengine hayo yanapotokea (mf. mtoto kusafishwa) yeye anakuwa hayupo. Na huyu mwenzie (MTOA MADA na MLALAMIKAJI MKUU) hafanyi lolote kusaidia hiyo situation. Anaishia kulalamika bila kufanya kile ambacho kwa maoni yake ni sahihi/bora zaidi.

#Amesema YEYE ndo aliyemuachia mwanaume mtoto. Sasa kama alijua hatopata malezi mazuri huko au ana wasiwasi kwanini alimuacha huko?
#Amesema alienda ustawi wa jamii kulalamika kuhusu kunyimwa kumuona mtoto, sio kumchukua ila kumuona.
Sasa anatakaje? Mtu utakaaje pembeni ukilalamika "ohh mtoto wa kike anasafishwa na kijana, mtoto wa kike analala na baba mdogo" huku ukiendelea kuishi maisha yako bila kujali kwamba malezi ya bintiye ni jukumu lake pia? Anaonekana ni mtu mlalamishi ambae ha-take responsibility kwa lolote lile. Ye anaona anaonewa tu.
 
Last edited by a moderator:
naomba kusema, wanaume tuheshimiane tena tuheshimiane, tabia ya kuachana na mwanamke lakini huishi kumfuata fuata kwa maneno jiheshimu tena jiheshimu.

Nimechoka na nimekuchoka ndio maana nimekuja kukuambia hapa, kwa kuwa ni member hapa najua utasoma na unajua mimi ni nani.

Nimechoka kukunyamazia, mwanaume gani unakosa busara hata chembe tu? Jiheshimu narudia tena jiheshimu.

Huyu mtu mimi nilikuwa kwenye mahusiano nae yapata miaka 7 na tuna mtoto mmoja alikua amefanya taratibu zote za kufunga ndoa isipokuwa tulikuwa bado kufunga ndoa tu.

Tukaja tukashindwana kila mtu akaendelea na maisha yake, wakati wakuvunja mahusiano mimi kama mtu ambaye nilihisi kuchoka.

Niliifahamisha familia yangu na nilitoa sababu zangu ambazo kwa upande wa familia waliamua kumwambia mshenga.

Basi mshenga akapewa taarifa na kwakua mshenga alikuwa anajua habari za huyu mtu wangu vizuri alieleza mengi pia kwa familia yangu hasa ambayo hata mimi sikutaka familia wayajue.

Kutokana na taarifa hizo baba yangu akikasirishwa sana na kuniomba kikao cha pande mbili.

Tulikutana kwenye kikao wazazi wake wakaongea na yeye akaongea, na mimi nikaongea na mshenga akaongea khaa!

Jambo la ajabu yeye akasema "jamani naomba mimi na mwenzangu tutaenda kuyaongea" khaa!

Baba yangu akahamaki na kumwambia kuanzia leo nauvunja huo uhusiano, wewe kajirekebishe na huyu akasome.

Baada ya hapo kama utakuwa umejirekebisha mlango upo wazi nitakukaribisha, kuanzia leo mwanangu yupo chini yangu. Tukafunga kikao.

Baada ya hapo yeye alinibembeleza sana nisiachane nae kwakua tuna mtoto na aliahidi angejirekebisha, na mimi roho ilikuwa inaniuma kuhusu mtoto.

Nikawa najitahidi kuwa karibu nae kwakua mtoto nilimwachia yeye mimi nilienda kukaa sehemu nyingine ambayo sikutaka kabisa yeye aijue maana namjua vizuri lakini sikuacha kila wkend kwenda kumuona.

Sasa shida sikuwahi kuona mabadiliko kwa zaidi ya miezi 8, kwanza kila siku ilikuwa afadhali ya jana, mwanaume mgomvi, anamatuasi yaani akilewa ananivua nguo kwa maneno mchana kweupe.

Nikaamua kukaa kimya kwa muda ila mtoto nilikuwa nawatuma wadogo zangu wanaenda kumuona na kumpelekea vitu vya mtoto.

Baada ya muda nikawa nikipiga simu kutaka kuongea na mtoto, hapokei, yaani zaidi ya mwezi simu haipokelewi wala msg hajibu.

Nikaamua kumpeleka ustawi kudai haki yakumuona na kuongea na mtoto, kumbe bwana huyu akavuta jiko wakawa wanaishi wanapika na kupakua.

Kilichofuata ni ndugu zake kunishambulia mimi nakusahau mema yote niliyokuwa nawatendea, kwakua tulichokanaa hiyo siku yeye kaja na timu toka kwao, mimi peke yangu, tukatukanana mbele ya polisi hadi basi, baada ya siku mbili akanipigia simu mimi 'eti niende nikawaombe msamaha ndugu zake kwa kua yeye hataki kuachana na mimi" nikamuuliza kwa lipi?

Eti umewatukana wazazi wake hawana kazi za kufanya, nikamwambia usinitafute maneno, na hilo haliwezekani kamwe, akawa ananitukana sana kwa msg kuna wakati hadi najikuta namjibu.

Nikaa kama mwezi, akaanza tena kunipigia "ooohh! Naomba turudiane," nikamwambia wewe si umeoa?

Akasema mimi naishi tu na huyu mwanamke lakini sina mapenzi wala malengo nae" nikamwambia endelea kuchezea watoto wa watu, huo ni uchafuzi, kuhusu mimi sahau sahau.

Baada ya hapo akaa kimya cha muda lakini jambo la ajabu kaanza tena kunitukana sana kwa msg, kiasi kwamba sielewi ana tatizo gani?

Mimi naishi naendelea na maisha yangu kwa amani lakini yeye kila siku anaishi anawaza kukabiliana na mimi, mimi nimekuchoka na hizi tabia.

Wewe kaa ishi kwa amani yako, niache na mimi niwe na amani yangu, nilikupa nafasi miaka 7 tena kwa uaminifu mkubwa, uliyoyafanya unayajua vizuri sasa tulia, "usiweweseke kujua kuhusu mimi" na lazima ujue naishi maisha mapya sitaki stress tenaaaa,

nimekuchoka najua utapita hapa, soma ukimaliza nenda kawasimulie waliokudanganya ukakosa mwana na maji ya moto.

lazima nyie ni watoto wa uswazi.
Pia umri wenu ni mdogo
 
Yes Lizzy

Hawa baba na mama wa huyo binti wote nadhani hawana muda wa malezi ya mtoto.

Heri wampeleke kwa bibi/ babu wa upande wowote ambao mtoto atakuwa salama. Kisha waendelee kuonyesheana ubabe.





BADILI TABIA unampa mtu ushauri ambao hauhitaji na japo huyo baba mtu pengine anastahili lawama kwa kiasi fulani lakini sio kwa asilimia zote kwasababu pengine hayo yanapotokea (mf. mtoto kusafishwa) yeye anakuwa hayupo. Na huyu mwenzie (MTOA MADA na MLALAMIKAJI MKUU) hafanyi lolote kusaidia hiyo situation. Anaishia kulalamika bila kufanya kile ambacho kwa maoni yake ni sahihi/bora zaidi.

#Amesema YEYE ndo aliyemuachia mwanaume mtoto. Sasa kama alijua hatopata malezi mazuri huko au ana wasiwasi kwanini alimuacha huko?
#Amesema alienda ustawi wa jamii kulalamika kuhusu kunyimwa kumuona mtoto, sio kumchukua ila kumuona.
Sasa anatakaje? Mtu utakaaje pembeni ukilalamika "ohh mtoto wa kike anasafishwa na kijana, mtoto wa kike analala na baba mdogo" huku ukiendelea kuishi maisha yako bila kujali kwamba malezi ya bintiye ni jukumu lake pia? Anaonekana ni mtu mlalamishi ambae ha-take responsibility kwa lolote lile. Ye anaona anaonewa tu.
 
Last edited by a moderator:
Nimelisha anzisha jaribu kuwa nawatuma wadogo zangu kwenda kumuona mtoto na hata kumchukua, akawa analalamika kwa watu mimi siendi kumuona mtoto wala sipigi sim, pia walikua wanawatreat vibaya sana wadogo zangu wakienda pale, yaani kuna wakati nilibadili line hadi nikahisi kuchanganyikiwa.

Nawaza pia hilo, japo sioni njia rahisi kwa kweli




Unajua hua sipendi hata kumpigia hata hivyo hua simpigii hadi niwe namuhita mtoto, kwa hiyo inaweza kupita hata wiki 3 mimi sijui mwanangu anaendeleaje, Lakini pia inanilazimu kumfuatilia maana ni mtoto wa kike n kuna mambo nikiyafikiria huwa nakosa amani kabisa.

mfano, kunasiku nilimuuliza mtoto nani anakusafisha ukienda chooni?? mtoto akanijibu anasafishwa na kaka wa ng'ombe(mfanyakazi wa ng'ombe) nikampigia nikamwambia kwanini mtoto anasafishwa na kaka wa ng'ombe?? hakuonyesha kujali hata kidogo, aliona ni kawaida tu, lakini mimi nilishamfundisha mwanangu kujitegemea kwa kila kitu, sasa sijui ilikuwaje hadi kumruhusu kaka wa ng'ombe kumsafisha mtoto wa kike.

Zaidi wakati mwingine wanaruhusu mtoto wa kike eti alale na baba ake mdogo mwenye umri wa miaka kama 23 au 24 jamani hebu niambieni kweli hawa watu wanaakili kweli???????

Kwakweli moyo wangu una maumivu sana nikifikiria hayo na nipo kwenye mkakati wakuomba nimchukue na niondoke nae mbali kabisa.

Kusanya ushahidi nenda Ustawi wa Jamii waambie unamtaka mtoto.
 
Mapenzi ni mmojawapo ya headache kubwa kabisa duniani hasa unapowekeza hisia muda rasilimali zako, uaminifu wako na matumaini yako kwa wrong number wrong choice INAUMIZA SANA... lakini ukiweza kusimama imara yakapita utapata mwanga mpya wa kuweza kusimama tena na kusonga mbele

~^~Don't fall in love with a dreamer~^~

Mbona anaezungumziea ni kama wewe mkuu? Acha kuvunga
 
Namuhitaji mtoto hata leo, lakini tatizo ni mtu mwenye roho ya ugomvi nikaona isiwe tabu mtoto huyo mchukue, akamchukua anakaa nae kwa wazazi wake. miaka 5

Dah pole but kama kuna liwezekanalo mchukue mwanao bana ukae nae
"mama tu" ndo anauwezo wa kumpa mwanae "kila kitu na kwa uhakika zaidi"
 
Nashindwa kumblock kwakua ninapotaka kuongea mtoto lazima nimpigie yeye.

unaweza kum-block coz si kila mda utataka kuongea na mwanao we utapotaka kuongea na mwanao una m-blockua(un-block) unampigia ukimaliza block tena au unaweka laini special kwa ajili ya kuwasiliana na mwanao tu ukimaliza unaitoa
 
unaweza kum-block coz si kila mda utataka kuongea na mwanao we utapotaka kuongea na mwanao una m-blockua(un-block) unampigia ukimaliza block tena au unaweka laini special kwa ajili ya kuwasiliana na mwanao tu ukimaliza unaitoa

Umesema kitu, asante
 
Mkishamfuta nafasi yake niwekeni mie.... maana siku hizi navaa suruali na msuli

Hahaha. Japo hili ni tusi, tutakufikiria mpendwa. Meanwhile, kati ya vigezo vya kuwa mwanachama ni pamoja na 1. Uwe na certificate of good conduct, kutoka Interpol. 2. Uwe na uwezo wa kutumia urinals 3. Uwe na uwezo wa kurubuniwa 4. Uwe na serikali mbili (vichwa viwili).

Masharti mengine tutayajadili baada ya kutimiza hayo.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom