Wanaume tabia hii vipi?

Wanaume tabia hii vipi?

kuna wanawake wakipata mtoto wanakuwa wachafu, gubu, na mapenzi yote wanahanishia kwa watoto.

jiangalie kama baada ya kupata mtoto umemaintain mambo hayo!

alaf jaribu katafta mtu wa kukusaidia kazi za nyumbani, kwa watoto wanavyosumbua sidhani kama unaweza kutekeleza majukumu ya nyumbani na kulea mtoto mchanga namna hiyo.

ila usidhani wanaume wote tuko hivo.. mimi nikitoka kazini ndo ahueni yake, ananipa mtoto na kufanya shughuli zake! namkabidhi tu pale anapolia sababu ya njaa.. mpaka atakapolala saa mbili usiku! wa kwangu ana miez 8 kwa sasa
 
Ningekua cjaoa ningekuchukua ufurahie ndoa mama wewe ni wife material muombee mumeo kwa Mungu atabadilka tu
 
Hua lazima wanaume tukutane kwenye kijiwe cha kahawa tubadilishane uzoefu wa kupata mnoti.hata mimi hapa saa hii naelekea kwenye kahawa mitaa fulani hapa Rock City.home ntatinga saa3 usiku,jana wife kanisemaaaa weeeee mi namcheki tu maana hajui undani wa yeye kubadilisha sato,kuku,mbuzi na ng'ombe.so mtoa mada uki mind sana sepa kwenu na ukishafikisha miezi 6 toka muda wa kujifungua ndo urudi.
 
My dia tafuta housegal au msaidizi yoyote hapo ndani..usitegemee.mumeo katoka kazini kachoka akuunge mkono tena kwenye zamu za kubeba watoto..kumbuka kule anakotoka ni kazini naye pia anakua kachoka..usije ukadhan kazin hakuchoshi...
Anaondoka sababu anajua akibaki tu watoto wote utamrushie yeye...
Ukitafuta mtu utaona anabaki home..kwanini..kwasababu ht km kacheza au kabeba mtoto kachoka na anahitaji kupumzika.yupo mtu atampa amsaidie kucheza nao...ss hivi akibaki akikaa na mtt mara kakurudishia ukae nae utaanza mlaum hapendi watoto ooh hataki kukusaidia...na sidhn km kweli hapendi watoto..
 
Habarini wana mmu,
Mimi Ni mwanamke ambaye nimeolewa na Nina Mtoto mmoja mchanga miezi 3, tatizo nililonalo Ni kwamba mume Wangu huwa hapend kukaa nyumbani yeye akirud kutoka Kazini Ni kupumzika kidogo then anatoka Hadi usiku Sana

Hana muda Hata wa kunisaidia kukaa na Mtoto angalau nami nipumzike kidogo maana anajua jinsi Mtoto anavyosumbua na tunakaa wenyewe tu Mimi na yey mume Wangu, daima yeye anajali company za marafiki tu.

Je hapo tabia hii inaashiria nini? Mapenzi yapo kweli au ndio Sina changu tena?
Daah! Umeolewa na "Bachelor Husband"...
Yani ni mwanaume aliyeoa ila bado anaishi maisha ya ki-bachelor...

Ni changamoto sana
 
Jaribu kujichunguza na upande wako pia. Wanaume hawapendi kelele wala dharau...

Vinginevo pata muda wa kuongea nae kumweleza vile unavotamani awe karibu na familia. Ukiongea nae kwa utulivu naamini atabadilika,hakuna mwanaume kichwa ngumu kwa mwanamke mnyenyekevu....
True that
 
Back
Top Bottom