Inatokea hasa kwa ndoa changa kwa sababu mwanaume au mwanamke(wachache) alikuwa na kundi la marafiki ambao ndio aliojenga nao maisha na furaha yake hadi mnakutana, kwa hali hiyo inamuwia vigumu kubadili gia ya kurudi nyuma ghafla huku gari inaenda mbele kwani atachekwa na kuonekana kapigwa pini....Ilitokea nilipooa na nakumbuka mke wangu hakuchukulia hili jambo kwa haraka ila aliomba nigawe siku za marafiki na za familia, tukakubaliana iwe wk-end, jumanne na alhamisi nyumbani zilizobaki za marafiki.... Baadae akaomba tuwe na siku moja ya kutoka kwa ajili ya marafiki nayo ikawa ijumaa naye anaunga tela.... Sasa mwaka wa 7 sijui hata zile ratiba ziliishia wapi kwani ratiba za out ni mimi na yeye kila tukiwa na ziada..... Cha kujifunza hapa ni kwamba: Usitumie nguvu nyingi kujenga ustaarabu wa ndoa yako ila tumia hekima na busara, siyo anarudi unampokea na matusi hapo ndio umelikoroga..... Tumia mbinu ya my sabuni wa Roho yangu naamini utafanikiwa ndani ya mwaka au miezi kadhaa.....Siku njema.