Wanaume, sio vizuri kudhalilisha wanawake waliovaa nguo fupi kwakuwa si mwanamke wako

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385

Nmesikitika sana baada ya kukaa na kuangalia vijana wa sasa jinsi walivyo na mambo haya hivi kweli,
Nimeangalia hii video sijaelewa lengo zima la hawa wanaume lilikuwa ni nini?

Yaani mnataka kumvua nguo zake hadharani kisa kwa nguo zake fupi duh tunaenda wapi huku.

Sawa ndio amekosea kwa kuvaa NGUO FUPI sana lakini hii sio sababu ya kutaka kumvua kabsa Nguo zake etiih kisa tu unataka kumdhalilisha...
Tujirekebishe wavulana kwa hili sio Fair kabsa ,kila mtu ana uhuru wake japo kuna watu sometime wanakwenda kinyume na maadili lakini tuwasamehe kwa kweli sio fair...
 
Nimeangalia hii video sijaelewa lengo zima la hawa wavulana/wanaume lilikuwa ni nini?
Sawa ndio amekosea kwa kuvaa NGUO FUPI sana lakini hii sio sababu ya kutaka kumvua kabsa Nguo zake etiih kisa tu unataka kumdhalilisha...
Tujirekebishe wavulana kwa hili sio Fair kabsa ,kila mtu ana uhuru wake japo kuna watu sometime wanakwenda kinyume na maadili lakini tuwasamehe kwa kweli sio fair...

Iko wapi hiyo video?
 
Sasa hivi ipo, naona kaiweka.

Huwa sielewi kwa nini watu wamnyanyase mdada aliyevaa nguo fupi.

Kwa mfano, huyo mdada kwenye video wala alikuwa hajavaa vibaya kabisa.

Ni ushenzi tu wa hao wapumbavu.
Nguo sio fupi kivile lakn wahuni walivyofanya ni karaha
 
Sasa hivi ipo, naona kaiweka.

Huwa sielewi kwa nini watu wamnyanyase mdada aliyevaa nguo fupi.

Kwa mfano, huyo mdada kwenye video wala alikuwa hajavaa vibaya kabisa.

Ni ushenzi tu wa hao wapumbavu.
Kundi kubwa ni watu wenye imani na itikadi fulani kumbugudhi mwenye itikadi tofauti na wao wanvyoamini, ni tatizo. Ndo maana hata Ulaya umezuka huu mtindo wa kuvuana hijabu.
 
Sasa hivi ipo, naona kaiweka.

Huwa sielewi kwa nini watu wamnyanyase mdada aliyevaa nguo fupi.

Kwa mfano, huyo mdada kwenye video wala alikuwa hajavaa vibaya kabisa.

Ni ushenzi tu wa hao wapumbavu.
Yaani...kuna mambo hapa bongo nasemaga bora hata mkoloni alikuja alileta elimu na hatupaswi kuwalaumi hata kidogo kwa waliovuna kwetu. Akili mgando tuu hapa ndo naziona....what if huyo angekua ni dada wa mmoja wao hapo? Au hata mpenzi..? Angeacha wamshambulie kma walivofanya?
 
Hao wanaume wenyewe hawajiheshimu hawatoweza kumweshimu mwingine.

Yani hao wamejawa na negative energy kiasi kwamba hawawezi kukaa bila kujaribu kuharibu, kupiga au kudhalilisha.

Hatari sana kuendekeza mitazamo ya kijinga.

Hapo wanajiona mashujaa kumbe wepesi kama karatasi
 
Yaani...kuna mambo hapa bongo nasemaga bora hata mkoloni alikuja alileta elimu na hatupaswi kuwalaumi hata kidogo kwa waliovuna kwetu. Akili mgando tuu hapa ndo naziona....what if huyo angekua ni dada wa mmoja wao hapo? Au hata mpenzi..? Angeacha wamshambulie kma walivofanya?
Duh mkoloni
 
Back
Top Bottom