pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 11,645
- 14,804
Habari za majukumu wapambanaji wenzangu,
Leo tukumbushane kidogo kwasababu kuna mambo yanaendelea kwa upande wa wanaume, na mengine nimeyashuhudia kwa macho yangu leo naomba niongee yafuatayo;
1. Usizalishe hovyo hovyo: mwanaume jitahidi ujenge familia, lakini ukishindwa kujenga familia basi tafuta mwanamke mmoja mkubaliane uzae nae, kuliko kuzalisha wanawake tofauti tofauti unakuwa na watoto Watano halafu kila mmoja na mama yake huo ni ujinga na utaona hasara yake baadae usiwe kama yule boss wa mawingu anayesifiwa alikuwa genius ila alikwama kwa kuzaa na kila mwanamke
2. Tunza afya yako: wanasema afya ni ya kwako na msiba ni wa kwetu mwanaume tunza afya yako hakuna mtu atapoteza mda wake kukuuguza wewe Watoto watakukimbia licha ya kuwasomesha na mke ataolewa na mwanaume mwingine mzima, watu wengi maarufu huko mitandaoni walikuwa wanakejeli na kutukana wanapopewa ushauri wa afya za oleo wanaomba michango ya kufanaya dialysis
3. Jenga mapema: usisikize maneno ya motivational speaker wanaosema nyumba sio asset ni liability ni bora uuguzwe ukiwa kwako kuliko kudhalilika kwenye nyumba za kupanga kuwa makini tafuta eneo jenga na ujiandae mapema na uzee kabla haijawa too late
4. Jithamini: yaani kuna wanaume leo hii wanapata nafasi za kazi na za kusoma nje ila wanaziacha kwasababu wanataka kuwa karibu na familia my friend hakuna familia inayomjali mwanaume ikitokea nafasi ya kukuinua basi usiiache ipotee fainali uzeeni usipoteze fursa
5. Kula vizuri: kuna kula vizuri na kula mlo mzuri mwanaume ukiwa na age yoyote ile ipuka kula vitu vya sukari na mafuta kula chips mara kwa mara, mwanaume ni dhaifu sana kwenye maradhi tunza afya yako usile kila kitu kuwa na miiko kwenye kula, hakuna tatizo la nguvu za kiume ni kubadilisha tu mlo na life style
6. Usisomeshe mwanamke wako hata awe wa ndao: yaani kwenye suala hili kila siku mambo mabaya yanatokea kama watu kuuwana na kudhuriana kama ilivyotokea pale kenya baada ya binti kumwagiwa acid, baada ya kumkataa mwanaume aliyemsomesha mwanamke hata awe wa ndoa sio ndugu yako punguza wenge MC pilipili na Nick wa II tumia kama references
7. Wekeza mapema : wanaume tunapoteza nguvu mapema sana hivyo Fanya uwekezaji mapema kabla nguvu hazijaisha kwasababu baadae utahitaji kuishi na nguvu itakuwa hauna tena kama huwezi kufanya biashara basi wekeza hata nyumba za biashara kama hotel,guest, na nyumba za kupangisha anza mapema
8. Usijisahau sana: kuna watu wanawekeza sana kwa familia kama mke na Watoto wanawapeleka shule za gharama lakini baadae wakiwa wakubwa na wakipata kazi wanawasahau wazazi wao, hasa wa kiume kwa hyo jipende ukipata hela tenga mda nenda mlimani city agiza msosi wa maana enjoy tafuta sehemu nzuri ya kupumzika nenda kapunguze Mawazo sio kila hela unayoipata unawekeza kwa mwanamke na Watoto hawana shukrani hao
9. Punguza umalaya: changamoto kubwa ya waafrika hasa watanzania ni umalaya, yaani Ngozi nyeusi tunapenda sana ngono nimeshangaa kwenye msiba wa yusuph manji licha hela zote alizokuwa nazo ila ameacha Watoto wawili tu, na hakuna vurugu za mali zimetokea kwa familia tupunguze ngono wazee ni hatari na inarudisha nyuma maendeleo
10. Usiache kuswali: kama wewe ni muislamu au mkristo kila mmoja kwa Imani yake basi aombe mungu kwasababu vita ni kubwa sana bila maombi ni ngumu sana, muislamu usiache Kwenda msikitini na mkristo usiache Kwenda kanisani hyo ndio njia pekee ya kuyashinda majaribu ya dunia
Alamsik muwe na siku njema