Wanaume ni kama wanyama’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume ni kama wanyama’

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jan 5, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  ‘Wanaume ni kama wanyama kihisia. Hawana huruma, hawajali na ndiyo maana hata kwenye msiba, unakuta wala hawaoneshi huzuni. Kwa kawaida hawajali kabisa, ni kama vile hawakuumbwa na roho.' Haya ni maneno ambayo yanatamkwa na mwanamke ambaye anaamini kwamba wanaume hawana hisia. Lakini siyo mwanamke huyu tu peke yake ambaye anaamini kwamba, wanaume hawana hisia.Kwa mfano, wanazungumzia sana kulia na pengine hata kucheka, kwamba, mara nyingi wanaume huwa wagumu kulia na hata kucheka kwao ni kwa kujikagua kwanza. Ndiyo maana unaweza kukuta wanaume wanaamini kwamba, kucheka sana kuna maana ya umwanamke au kwa mwanamke kucheka sana, kuna maana ya umalaya.

  Wanawake hufurahia kucheka sana wakati wanaume huogopa kucheka sana. Katika hali fulani, watu wengi wanaamini kwamba, wanaume hawana uwezo wa kuonesha hisia zao kirahisi. Lakini ukweli unaonesha kwamba, wanaume na wanawake, wote wana hisia sawa, bali wanaume huonesha zaidi hisia ambazo zinawaumiza wenyewe na pia hisia ambazo zinaumiza watu wengine.Imethibitika kwamba, wanaume huwa wanatumia muda mwingi kufikiria mambo mabaya kuliko mazuri, hivyo hisia wanazopata mara nyingi ni mbaya. Wanaume huwa wanashiriki hisia zao na watu wachache sana.

  Wanaume hujikaza kisabuni kwenye mambo yanayowaumiza. kusema hisia zao kwao ni kama udhaifu. Lakini hata wanapoelezea hisia zao, hawazielezi kwa njia yenye kugusa sana. Hutumia lugha ambayo haioneshi hisia na hata maneno yao pia siyo ya kihisia hasa. Lakini pia wanaume huwa hawasemi hasa hisia zao za ndani. Wanazielezea lakini husielezea kidogo au kwa kiwango ambacho sicho, yaani cha chini kuliko ilivyo. Wanaume mara nyingi wako tayari kuelezea hisia ambazo zinaonesha haja ya kudhibiti au madaraka ama nguvu. Kwa mfano, zenye kuonesha majivuno, hasira na kijicho, amri na kebehi. Wataalamu wengi wanasema wanaume wamefundishwa na jamii kuficha hisia zao, jambo ambalo huwaumiza sana bila wenyewe kujua.

  Kwenye suala la hisia mwanamke na mwanaume wanaishi dunia mbili tofauti. Kwa hiyo siyo kweli kwamba, wanaume hawana hisia au hisia zao ni kidogo. Ukweli ni kwamba, wote wana hisia, bali wanaume hawana uwezo wa kuzionesha, wanazikandamiza wakati wanawake wamewezeshwa kuzionesha. Kuficha hisia hata hivyo kunaelezwa kwamba, huwa zinawaumiza sana wanaume kuliko inavyofikiriwa. Ndiyo maana kukiwa na vurugu kwenye ndoa, ambazo hutoa maumivu sawa kwa mwanamke na mwanaume, mwanamke anaweza kuwa na nafuu kubwa kwa sababu atasema hisia zake na atakuwa amepunguza kuumia kwa mwili.

  Kwa mwanaume mara nyingi maumivu yanakuwa makubwa kwa sababu hukandamiza mengi ambayo baadae huja kumuumiza kimwili.Ni kweli kwamba, vurugu za ndoa huwaumiza wanawake zaidi, lakini kama ni vurugu ambazo mwanamke na mwanaume wanabeba mzigo sawa, mwanamke anakuwa kwenye nafuu zaidi kwa sababu ya uwezo wake wa kusema hisia zake na hivyo kuweza kupunguza maumivu.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huyo mtu ambae bado anaamini wanaume hawana hisia/hawapati uchungu/hawaumii amepitwa na wakati.

  Kutoa machozi na kulia kunaweza kukafanywa kinafiki, kuficha hisia hakufanywi kinafiki.
   
 3. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ol in ol..... miwanaume ina mioyo migumu kama jiwe yan.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Hajawahi ona mwanaume analia! Hajaona maisha, it is actually very moving and sexy kinda thing,lol
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka alipofariki mama yangu sikumuona baba yangu akilia, alikuwa kawaida sana, lakini baada ya wiki hivi tangu tumalize msiba nilimkuta nyuma ya nyumba usiku sana akilia kwa uchungu. aliponiona alijifanya kupotezea, ingawa nilikuwa mdogo, I was 10 years, nilijua alikuwa analia.
  Kwa hiyo, suala la wanaume kuficha hisia zao, ni jambo ambalo lipo sana. Na sio kwamba hatuna hisia.
   
 6. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  woow!!! kibao kimewageukia wanaume mwaka huu!!! safiii!! heshima yako babu mtambuzi!
   
 7. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mmh! sio wote kiukweli mi sijawahi kuwaona wenye mioyo kama jiwe wengi mioyo yao inakua kama ''KEKI''
   
 8. huzayma

  huzayma Senior Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maskini, hadi meona huruma.
   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wanaume tuna hisia, ila si watu wa kukurupuka ....
  Mara nyingi husubiri kupata ushahidi ....
   
 10. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Heshima yako baba,kiukweli kwa mtu anayefikiri wanaume hawana hica ana uelewa mdogo,wao pia huwa wanaumia ila mungu mwenyewe ndio kawaumbia kuficha hica na ili tofauti ipatikane ni lzm wawe hivyo kuonyesha uanaume kwan cku zote hata inapotokea tatizo au mcba na ndan ya nyumba wote ikawa ni vilio baba mama na watoto nani atahandle mambo mengine,hayo ndio maumbile yao na mungu ndio alitaka iwe hivyo!km ni wanyama hata wanawake tu wanyama pia na co tofauti baina yetu na wao haitabadilika kwan ni mpango wa mu
  Google
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  I know, right?!
  Mi hua napenda, nadhani kwasababu haitokei kila siku.
   
 12. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  acha hizo wewe..
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  dah tatizo kuleta ubishi wa jeans na maji ndio wanaume tulivyo..
   
 14. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  du! Kwa ishu ya kulia ata mimi ni mgumu sijui kwanini yaani nikienda misibani nasikitika sana lakini machozi inakua ngumu kutoka.ila nakumbuka dada'ngu alinambia story moja kuhusu marehemu babangu machozi yalitoka yenyewe tena kuliko siku baba alipofariki nikiwa form 2.
   
 15. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kudos canta..
   
 16. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Sasa mlitaka wanamume walielie kama mademu kwenye misiba!¿? Shughuli za mazishi zitafanywa na nani sasa? Hata wanaume machozi yapo jirani saaana ila tu huwa wanaya-hold ili shughuli zingine ziendelee kama ilivyopangwa.
   
 17. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mwanaume kulia si lazima atoe machozi akinuna tu ndo kulia kwenyewe
   
 18. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ndio hiyo sasa tofauti alioisema da canta na ankoli mtambuzi
   
 19. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mmmh!! hii nayo kumbe ipo!!
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu, ngoja niende hapo kwa Mpemba nikakununulie Mkate Boflo wa kukupongeza kwa mchango wako mahiri,
   
Loading...