luckyline
JF-Expert Member
- Aug 29, 2014
- 15,150
- 21,802
Kutokana na sasa hivi
ugonjwa wa heart broken kuonekana wazi umekosa chanjo na matibabu yake
ni ya magumashi tupu kama Ebola thread hii itasaidia kila jinsia ijue
jinsia nyingine priorities zake/zao ni zipi hasa?
Mimi nachokoza tu mjadala kwa wote wanandoa na wasio wanandoa kwamba
wanawake wenye ndoa Priorities inaonekana ni hizi ili tusijekuhisi
hatupendwi kumbe kosa ni kuwa hatujui vipaumbele vya wenzetu.
1.Mtoto/watoto
2.Mume
3. Kazi
Wanawake wasio na ndoa
1. Pesa
2. Mwanaume
3. Kazi
Nawakaribisha wanawake muoneshe vipaumbele vyenu ili wanaume wajifunze
kitu kutoka kwenu itasaidia sana watu kupenda kwa akili na si kama
matutusa.
Sasa mimi kwa wanaume nimeona kuna tatizo kidogo na ni ujinga wa hali ya
juu.
Tazama vipaumbele vya mwanaume
1.Mwanamke
2. Kazi
3. Mtoto/ watoto
Mimi sasa nashauri wanaume sasa tubadirike na vipaumbele vyetu viwe kama
hivi,
1. Mtoto/watoto
2. Kazi
3. Mwanamke
Mimi nimechokoza tu mjadala wadau sasa tutililike.
Pia dada zangu msinishambulie kwamba naiamsha mibuzi yenu itakakata
kamba naomba msiwe na hofu, misukule huwa haifufuki.
Cc; BADILI TABIA lara
1 Kongosho The
Boss Heaven on Earth
Pdidy Mtambuzi and
all of you.
fweza muhimu
Last edited by a moderator: