Wanaume na ndoa!

Mom

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
708
29
wapendwa naomba mnisaidie kwa hili, kwanini wanaume ni waoga sana kuingia kwenye ndoa? yani hata kama mmeishi pamoja ikija kwenye suala la ndoa ni kupiga kalenda tu, ni kwanini inakua hivyo? je anakua hana mapenzi na mwenzi wake lakini anaendelea kudanganya kuwa anampenda?
 
Kumbuka kuoa au kuolewa ni kwamba umeamua huyo ni wa maisha yako yote awe dokozi au kikojozi, lazima uwe makini na mtulivu kufanya maamuzi.

Ukiona mwenzio anataka kutoka mbio, usiingie kichwa kichwa! Lazima uchungulie kulikoni.

Only that na wala si uoga!!
 
Hiyo SEKTA ina ugumu wake.. Ni lazima kuamua kwa dhati unapoingia, Kwani ina mlango mmoja tu wa kuingilia.. Ukisha ingia, Kutoka hakuna...
 
mi naona kama uoga hebu imagn mfano huyu mwanaume na mwanamke wameishi zadi ya mika 10 na wanawatoto kama 4 hivi lakini kila akikumbushwa kuhalalisha uhusiano huo hatakosa kisingizio mara hatujamaliza ada, nyumba haijamalizika mradi tu hakosi kisingizio je shida inakua nn hapo?
 
Hiyo SEKTA ina ugumu wake.. Ni lazima kuamua kwa dhati unapoingia, Kwani ina mlango mmoja tu wa kuingilia.. Ukisha ingia, Kutoka hakuna...

na inachukua muda gani mpaka mtu aamue kwa dhati?
 
wapendwa naomba mnisaidie kwa hili, kwanini wanaume ni waoga sana kuingia kwenye ndoa? yani hata kama mmeishi pamoja ikija kwenye suala la ndoa ni kupiga kalenda tu, ni kwanini inakua hivyo? je anakua hana mapenzi na mwenzi wake lakini anaendelea kudanganya kuwa anampenda?
chanzo ni nyinyi wanawake!
 
na inachukua muda gani mpaka mtu aamue kwa dhati?

Inaafatana na mtoa uamuzi. Inaweza kuchukua mwaka, na hata miaka! Ila wengine tunaogopa MAJUKUMU! Unajua yula wakukutana na kuachana, hana gharama!
 
napend akuwashauri wadada wackubali kuishi na mwanaume bila kutangaza nia inayoeleweka kwanza.
 
ni kweli nyamyao hata mi ningeshauri hivyo lakini kuna wale ambao hawakupata ushauri huo na wako hivyo sasa
 
Mkiingia ndani ya ndoa unyenyekevu wote unaisha, mwanaume anahitaji kujiridhisha kwamba sasa yupo tayari kumtunza mwanamke, kutunza family na majukumu mengine ya ndoa. kwa miaka ya sasa wanaume wengi hupenda kujikamilisha kielimu, kifedha wengine haoi mpaka apate degree, masters kwa sababu nyie wanawake wa sikuhizi mnapenda sana raha na starehe, usipokuwa na kazi nzuri tabu, huna gari dharau utazipata, wenye magari watasifiwa kila siku. nakumbuka rafiki ya bro wangu alikuwa na wife wake wa ukweli mno acha tu, bro akanunua chaser mayai miaka ya 98-99, bro alikuwa bd hajaoa, wife wa jamaa alikuwa haishi kumtaja bro na alikuwa akija hm kuazima gari, yule rafiki wa bro alipoona hivyo akaamua kuiba kazini kwao, na yeye akanunua corrola lkn mwaka mmoja baadaye jamaa akasimamishwa kazi, kesi ikachukua mwaka mzima jamaa akatemwa job, hivi vitu ndo vinatufanya tuwapige kalenda, ili kesho na keshokutwa usianze kunigeuka tena. na nyie muache kulazimisha acha mtu ajiandae
 
kumbe ndio hivyo! basi labda anaogopa majukumu huyu?
 
na hawa wanaume bwana! sasa una watoto wa 4, unasubiria nini tena? cha ajabu anaweza kuja kutangaza nia kwa mwingine kabisaaaa..hapo ndipo ninapowachoka.
 
sio nyie mnapenda kuwastarehesha?kama mkigundua huyu ni starehe mbele kwanini usisake asie na makuu?
 
napend akuwashauri wadada wackubali kuishi na mwanaume bila kutangaza nia inayoeleweka kwanza.

Ukithubutu kuwashauri hivyo watakuona una roho mbaya kama ya mchawi, tena mwenye macho mekundu anayestahili kukatwa katwa mapanga! Mambo ya utandawazi na kwenda na wakati ndo tatizo. Yaani leo binti anatongozwa, kesho au siku hiyo hiyo anatoa hazina yake na ndani ya week moja anahamia kwa brother men. Na kwa vile brother men anataka maziwa bila kufuga ng'ombe, anaendelea kukamua tu. Ila siku akiambiwa kuwa mwenye ng'ombe angependa kumgawia kabisa ili naye aanze kubebe mzigo wa kukata majani na kuzoa samadi ndipo kizaa zaa kinapoanzia.

Dada, hakuna mwanamume duniani anapenda kubeba mizigo ingawa utamu anautaka. Free milk ruksa ila kufuga ng'ombe NO.
 
kumbe ndio hivyo! basi labda anaogopa majukumu huyu?

huyu ataogopaje majukumu wakakti tayari anayo, watoto wa 4 na anawatunza c tayari jukumu, sema anagopa kujifunga kitanzi cha maisha.
 
Hiyo SEKTA ina ugumu wake.. Ni lazima kuamua kwa dhati unapoingia, Kwani ina mlango mmoja tu wa kuingilia.. Ukisha ingia, Kutoka hakuna...

mkuu, tafadhali fafanua hapo kwenye red.
Hata ukifumaniwa au fumania huruhusiwi kutoka? How and why
 
na hawa wanaume bwana! sasa una watoto wa 4, unasubiria nini tena? cha ajabu anaweza kuja kutangaza nia kwa mwingine kabisaaaa..hapo ndipo ninapowachoka.

shida ndio hapo sasa! na hata kuoa sawa na binti yake! ina bore sana, sikatai mwanamke ana kosa kukubali kuishi maisha hayo bila ndoa lakini kwann mwanaume hayuko tayari baaada ya miaka yote hiyo? zamani mikoa ya kusini kuna mangi mmoja alioa mke wa huko kwa staili ya kumchukua na kuishi nae japo wazazi wa pande zote walijua hakuwahi kujitambulisha rasmi na kufunga na ndoa. walijaliwa watoto2 na bahati mbaya yule mama alipata stroke akafa, si ndio ilikua shida maana wakusini wanataka kuzika na wamangi nao wanataka kuzika mwisho ikaamuliwa atoe mahari achukue mwili wa my wife wake akazike kwao! kwann kujitakia haya yote kama kweli unampenda?
 
Back
Top Bottom