Mara zote maendeleo ya mtu mmoja na namna awazavyo ndivyo unavyoweza kupata taswira ya maendeleo ya Taifa fulani.
Tukionacho kwa Mzee Gurumo sasa hivi si jambo geni sana maana ni wazee wengi tu wa zamani ambao nao wapo dhoofu ili hali pamoja na kwamba walikuwa na fursa za kutosha.
Sababu ya kufikia hapo walipo ni kwamba fursa walizozipata hawakuzitumia kwa manufaa ya kiuchumi(fikra dumavu)....hawakubadili ulimwengu wa umaarufu kuwa ndio mpenyo wao kiuchumi
Umenikumbusha!
Leo tulikuwa na mjadala hapa maeneo ya kazi
Kuna jamaa walikuwa wanadai kuna watu "wamepangiwa" kukosa na wengine kupata,nikawauliza kuhusu walipotoa huo mtazamo wao hawakuwa na majibu ya kuridhisha kabisa wakabaki wananiambia tu eti Mungu ndie anaepanga nani apate nini na kwa kiasi gani
Nilichowaambia mimi ni kuwa watu kama hawa ndio wanafanya watu waendelee kuwa maskini hasa watoto wao wanaowalea,wanawafanya wabweteke bila kujibidiisha kikazi na kifikra
Pia wanataka kumfanya Mungu aonekane ni mwenye upendeleo wa kuwapa wengine nyingi na wengine kidogo jambo ambalo sio kweli
Nijuavyo mimi Mungu hapangi nani apate na nani asipate ila ameweka kanuni ambazo kila atakaezifuata na kuzitii na pia kufanya kazi kwa bidii kwa uangalifu na kutumia akili kwa kiwango chake atapata kwa kiwango hicho,haya mambo ya kukaa na kudanganyana eti Mungu hajanipangia kuwa tajiri ni maneno ya kivivu na ni maneno ya kukemewa kwa nguvu zote
Wazee kama hao uliosema hapo wamevuna kwa kiwango chao kama walichezea watakula kuchezea hoko,Mungu sio boi wako wa kufix mistake zako tena nyingi za kijinga unazozifanya kila uchao
Ukiwa mhongaji utavuna uhongaji!!!!!!!
T.I.D,Blue,Chid Beenz,Ray C baada ya miaka 30 watakuja na ngonjera hizo
vijana maofisini wanaokopa Verossa na kila mwezi kuhonga nusu mshahara nao pia
Swadakta mkuu,
Wakati tukiwatafakari wazee hawa na jinsi walivyoyachezea maisha tusijisahau kuwa na sisi wazee wa kesho wengi wtu tunapita njia hiyo hiyo.
Vipaumbele na uwekezaji hatujui!
Tunapenda kutumia kabla hata hatujawa na akiba kiduchu, tunataka mambo makubwa kabla ya kuyafikia kihali na mali.
Ndio kama mfano alioutoa mkuu hapo, tunaanza kazi na kuchukua mikopo kisha kipaumbele chetu ni magari na kuku, bia na warembo.
Tukijatahamaki uzee huu na maandalizi hayakufanyika wakati waswahili wanasema "Fainali uzeeni"
"Ukimcheka peku na ungo unafuatia" hawa wazee wawe somo kwetu kwani na wao enzi zao waliona maisha ndio hayohayo
tatizo la nchi ni kutokuwa na Social Security ya nchi nzima ambayo kila mtu mwenye kufanya kazi na kulipwa mshahara akatwe kiasi fulani ya mshahara wake ili akistaafu basi apate na yeye anachostahili kipindi cha uzee wake. ule utamaduni wa kuwa na bima kwa kuzaa watoto wengi uliingia shubiri baada ya magonjwa na mfumo wa maisha ya mjini. kwa nini tusiwe na mfuko mmoja wa pensheni wa bima ya afya?
Mzee kama huyu ambaye amefanya kazi miaka hamsini na kama angekuwa amechangia kwa miaka yote hiyo leo kwenye mfuko wa pensheni leo angekuwa anakula pensheni yake vizuri tu. fikiria tu shilingi ya miaka sitini leo ingekuwa na thamani ya kiasi gani.
Tupiganie tuwe na social security ambayo mtu awe house girl ,mlinzi ,mwanamuziki ,mhasibu ,bar maid , changudoa , mhandisi achangie mpaka akifika muda wake wa kustaafu kufanya kazi aweze kujilkimu maisha. Hii itapunguza adha nyingi kwa wazee waliofikia muda wa kustaafu.
unajua unaweza ukawekeza vitega uchumi binafsi vikaja kudondoka au ukaweka fedha benki ikaja dondoka lakini ukiwa na Social Security ambayo na ya nchi nzima ina uwezo mkubwa wa kudiversify risk na ikawa madhubuti.
sijui hata kama kwenye katiba imendikwa ni haki ya kimsingi kwa kila mwenye uwezo wa kufanya kazi kuchangia kwenye social security na kupata mafao yake anapostaafu kazi au anapopata ulemavu wa kutofanya kazi au anapokuwa hana kazi sababu kazi hazipatikani.
Nyumba sijui but uisishangae akiwa hana
mbona marehemu Mzee Kipara alikuwa hana nyumba
na alikuwa kazaliwa mjini hapa hapa Dar?
na aliajiriwa RTD...miaka hiyo
Mkuu umeleta post yenye observation nzuri sana maana watu kwenye tasnia ya burudani wanataka wapate milion mia moja alafu akate milioni 50 ajenge nyumba au afanye jambo lolote la maendeleo. Huwa nikiwasikia wanavyoilalamikia serikali mpaka nashangaa maana sie na vimishahara vyetu na bado tunawachangia kila weekend kwa kuingia kwenye kumbi za starehe na bado tunafanya mambo, naomba kuongezea mpaka mwaka 1992 / 1993 kima cha chini cha mshahara tena sekta binafsi kilikuwa 5000 na kama alikuwa analipwa 3,000 mwaka 1978 zile zilikuwa ela nyingi sana kumbuka miaka ile serikali ilikuwa inadhibiti bei ya vitu mpaka mtu wa kima chini aliweza kujenga nyumba tofauti na sasa kupata kiwanja tu ni issue hata kama unalipwa 3 million
tatizo la nchi ni kutokuwa na Social Security ya nchi nzima ambayo kila mtu mwenye kufanya kazi na kulipwa mshahara akatwe kiasi fulani ya mshahara wake ili akistaafu basi apate na yeye anachostahili kipindi cha uzee wake. ule utamaduni wa kuwa na bima kwa kuzaa watoto wengi uliingia shubiri baada ya magonjwa na mfumo wa maisha ya mjini. kwa nini tusiwe na mfuko mmoja wa pensheni wa bima ya afya?
Mzee kama huyu ambaye amefanya kazi miaka hamsini na kama angekuwa amechangia kwa miaka yote hiyo leo kwenye mfuko wa pensheni leo angekuwa anakula pensheni yake vizuri tu. fikiria tu shilingi ya miaka sitini leo ingekuwa na thamani ya kiasi gani.
Tupiganie tuwe na social security ambayo mtu awe house girl ,mlinzi ,mwanamuziki ,mhasibu ,bar maid , changudoa , mhandisi achangie mpaka akifika muda wake wa kustaafu kufanya kazi aweze kujilkimu maisha. Hii itapunguza adha nyingi kwa wazee waliofikia muda wa kustaafu.
unajua unaweza ukawekeza vitega uchumi binafsi vikaja kudondoka au ukaweka fedha benki ikaja dondoka lakini ukiwa na Social Security ambayo na ya nchi nzima ina uwezo mkubwa wa kudiversify risk na ikawa madhubuti.
sijui hata kama kwenye katiba imendikwa ni haki ya kimsingi kwa kila mwenye uwezo wa kufanya kazi kuchangia kwenye social security na kupata mafao yake anapostaafu kazi au anapopata ulemavu wa kutofanya kazi au anapokuwa hana kazi sababu kazi hazipatikani.
Nyumba anayo mkuu, labda kama timu yake ni zaidi first 11 na wachezaji wote wa akiba...
These guys were really busy kule ikulu!!
Babu DC!!
Na ndio maana vijana wengi including watangazaji aliposema amefanya kazi miaka kibao hata baiskeli hana wao moja kwa moja wame-conclude usipokuwa na gari basi huna mafanikio, na ukiwaona wasanii wetu wanavyotembea na tabasamu nene huku muziki mtulivu kwenye gari unaweza kusema wame-win maisha lakini pindi yanapowakuta ya kuwakuta ndio unagundua hali ni tete, si mbaya kununua usafiri lakini kidogo wanachopata wanatakiwa wakifanyie mambo, wanailamu serikali ila hawajui kama inawasaidia bila kujijua kwani wakifanya matamasha wanalipwa let say milion moja ambayo haikatwi kodi na hiyo ni weekend moja wakati huku uswahilini mtu pato lake la mwezi tena wanakata na hifadhi ya jamii na PAYE na kidume kinatoka na laki 7 na bado mambo yanakwendaSwadakta mkuu,
Wakati tukiwatafakari wazee hawa na jinsi walivyoyachezea maisha tusijisahau kuwa na sisi wazee wa kesho wengi wtu tunapita njia hiyo hiyo.
Vipaumbele na uwekezaji hatujui!
Tunapenda kutumia kabla hata hatujawa na akiba kiduchu, tunataka mambo makubwa kabla ya kuyafikia kihali na mali.
Ndio kama mfano alioutoa mkuu hapo, tunaanza kazi na kuchukua mikopo kisha kipaumbele chetu ni magari na kuku, bia na warembo.
Tukijatahamaki uzee huu na maandalizi hayakufanyika wakati waswahili wanasema "Fainali uzeeni"
"Ukimcheka peku na ungo unafuatia" hawa wazee wawe somo kwetu kwani na wao enzi zao waliona maisha ndio hayohayo
mkuu una hakika? maana kwa jinsi siku hile alivyo kuwa anaongea kuwa hajafanikiwa kuwa na gari nilishindwa kuelewa kama ana nyumba. its ma hope anayo.
Say what...? Hizo habari za mshahara wa rais nimekuwa nikizitafuta kwa zaidi ya miaka 6 sasa bila mafanikio yoyote.
Wewe umejuaje mshahara wa raisi Mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 27,000? Enzi hizo mishahara ya viongozi ilikuwa ikiwekwa wazi ama?
Mkapa mshahara wake wakati akiwa rais unaujua? Kikwete je?
Hahahahahahaba Nyani Ngabu, nilipoona tu Bossman kataja mshahara wa rais nikakufiiiria.... nakikumbukaga sana kilio chako cha mishahara ya marais.....
Sure, mwisho wa huu mjadala Boss inabidi atupe sosi ya hii taarifa ili tuweze kujua mishahara ya waliofuatia
Wanasema eti Mungu hakuwapangia!!
Hata aibu hawaoni
Ifike mahali tuwajibike kwa makosa yetu!
ha haaaa, ila tuelewane kwanza kuwa uchumi siyo ubahili..... lol! sasa tuendeleeHapa ndipo utakapowajua wachumi wa darasani na wale wa kuzaliwa...
Halafu mtu kama huyo anakunywa bia kama vile ana complementary coupons za TBL..lol!!
Babu DC!!
alinunua viwanja vingi sana, ila sasa alipofilisika na kwa sababu hakuwa na investment nyingine na hakuwa na hela, pamoja na kutaka kuendeleza life style waliyokuwa wanaishi basi waliuza vyoooteeeee kidogo kidogo mpaka akamaliza. hapo sasa ndo akaridhika kuwa kafilisikaUmeona sasa
mtu ananunua magari wakati mashamba yanauzwa angenunua hata eka 1000
leo angekuwa mbaali
kabaki kulaumu watu tu