Nakubaliana na wewe mkuu...
Nilipomsikia akiongea + mambo mengine ninayayaona ya watu kama hawa, natamani kuwapima "size of prostate glands" ili niwape ushahidi kwamba the invested somewhere else!!
Babu DC!!
mfano Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini'
mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka
kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu'
Say what...? Hizo habari za mshahara wa rais nimekuwa nikizitafuta kwa zaidi ya miaka 6 sasa bila mafanikio yoyote.
Wewe umejuaje mshahara wa raisi Mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 27,000? Enzi hizo mishahara ya viongozi ilikuwa ikiwekwa wazi ama?
Mkapa mshahara wake wakati akiwa rais unaujua? Kikwete je?
hiyo ni kweli mkuu sijui wazee hawa wa zamani hawakuwa na ufahamu? mimi naona walikuwa wanapata vitu vingi bure na nafuu so wakajisahau. Nina mfano hai jana tu hapa ofisini kuna mzee mmoja mfanyakazi mwenzangu wao ndo watu wa kwanza kuajiriwa hapa ofisini hiyo ni miaka ya sabini tunakaa njia moja hivi sasa jana kaniona napita zangu kuja job yeye yupo kituoni mm sikumuona sasa akaja ofisini akasema mtani kama nilikuona wewe ukiwa kwenye gari Fulani hivi ila nikajiuliza mbona gari yako ninayoijua sio hiyo? nikamwambia nilikuwa mimi basi akaanza kulalama yani sisi tulichezea maisha mtu ulikuwa unapewa kila kitu bure mwisho wa siku unachukua mwanamke jioni unaenda pumzika nae!! yani kuanzia chakula, bia, usafiri wa kurudishwa home vyote ni bure! sasa anajuta na kusema tazama vijana wa siku hizi mambo yenu yalivyo mazuri sisi tumebaki kuwakodolea macho tu! sasa nashindwa kusema mfumo uliokuwepo ni tatizo au ni akili ya mtu binafsi!
daa nilimsikia akisema hivyo lakini interview yake ya jana siku pata kuhitazama.
LAKINI NILIPO SIKIA HAKUWAI KUMILIKI GARI NILIJIULUZA INA MAANA NYUMBA ANAYO? HADI LEO SIJAPATA JIBU KWANINI ALISEMA GARI? HUYU MZEE NI WAZI KWAKE GARI HALIKUWA KIPAUMBELE KABISA NA ALISEMA VILE KUTAFUTA HURUMA TUU.
The Boss HEBU NIJUZE KAMA KWENYE MAONGEZI ALIONEKANA NI MTU MWENYE NYUMBA YAKE NA SIWEZI KUMHUKUMU KWA KUTOKUWA NA GARI BALI KWA KUTOKUWA NA NYUMBA YAKE BINAFSI.
Mkuu umepotea sana
back to topic
mwenyewe jana alisema mshahara wa 'shilingii mia tatu' ulikuwa sawa na milioni ya leo
halafu akahama bendi na kulipwa mshahara wa 'elfu tatu'
karibu sawa na milioni kumi basi yaleo..
still anadai 'hakupata chochote' na mziki wake
bado 'connections' za watu mbalimbali alizopata
Mwaka 1992 nilisoma kwenye gazeti la Mfanyakazi...kama unalikumbuka
na walisema 'mshahara wa Rais wakati huo ni 27,000/-
na bado nakumbuka....hilo...mishahara ya Marais wengine sikupata data
lakini unaweza fanya calculation kwa kuanzia kima cha chini
by the time Nyerere anatoka mshahara wa Rais ulikuwa mara 12 ya kima cha chini
now nasikia ni mara 58 ya kima cha chini
Nyumba sijui but uisishangae akiwa hana
mbona marehemu Mzee Kipara alikuwa hana nyumba
na alikuwa kazaliwa mjini hapa hapa Dar?
na aliajiriwa RTD...miaka hiyo
Mfanyakazi nalikumbuka sana na coverage yake ya ile kesi mpiga picha/mwandishi wa habari (jina limenitoka kidogo) ndo iliyompaisha Masumbuko Lamwai kutoka kwenye obscurity na kuwa household name. Nilikuwa napenda sana kusoma 'Amini Usiamini'.
Je, kwa sasa umesikia huo mshahara ni mara 58 zaidi ya ule wa kima cha chini toka kwa nani/wapi?