Ukutaka kunielewa sasa hata niongee vipi hautonielewa. Jeans haivaliwi mvao mmoja PERIOD.Matola, hongera kwa kunukia. Ila hapo kwenye kufua jeans wala sikubaliani na wewe. Na uvaaji wa suit na kufua inategemea na hali ya hewa. Siwezi kukuachia uvae suti na majoto ya dsm, unaenda harusi ukumbi wa makuti. Ukivua shati lote mgongoni limelowana, afu niitundike ikauke? Kazi ya hela ni matumizi, tutakata budget ya bia tuwekeze kwenye usafi baba. Binafsi, under very rare circumstances inahalalisha kurudia nguo. Usafi wa ulipokuwa na pengine hali ya hewa rafiki.
hahaha, mnaniudhi nyie! Mtu akiketi, akiamka unatafuta pa kuhemea! Kwani isipopauka kiwanda si kitafungwa! Na ikichanika unapokanyagia uache kuivaa!
Sasa ukute huyo mwanamke anayenuka...unaweza kuanza kuugua homa! acheni hizo bana usafi ni muhimu kwa wote,
Hahaha mbona kuna wanawake ambao wasafi juu juu wananukia wakivua utadhani umefungua ndoo ya samaki kutoka feri
Mwingine akikatiza jirani yako utadhani mbuzi beberu la kule Vingunguti linakatiza.
Mkaka hii thread ni special kwa wanaume, wanawake thread zipo nyingi za usafi na mambo mengineyo. Hivyo wewe sit back, relax tuendelee kuongelea usafi kwa wanaume.
Hivi kweli mpaka issue ya usafi mke amuhimize mume? mbona ni kitu ambacho kila mtu anatakiwa ajitambue kwa hili?!! yaani mtu hawezi feel ananuka mpaka mkewe? au aoni anarudia sana nguo mpaka mkewe aone? khaah!! wanawake mbona kazi ipo.
Kuna kaka mmoja tulimpa live ofisini, alikuwa imezidi harufu si mdomo si mwili...kweli siku hizi amebadilika na fukuto limeisha pia hakuweka uadui..kijana handy ila alikuwa anatema vibaya mno.
na ukiivua tu naiweka kwa maji! Ukinunua jeans ukaona unaipenda, kesho yake nenda dukani kanunue kumi kama msukuma. Staki uvundo mie, ntaificha ndo ukome!
dada BelindaJacob unataka watu watumie nguvu kubwa kutafuta hizo sredi zinazohimiza mjisafishe vyema wakati hata hapa tunaweza kulitekeleza hilo cuz both men n women wanapitia hii sredi,nimeamua kufanya hivyo kwasababu binadamu tuna tabia ya usahaulifu hivyo ni jukumu letu sote kukumbushana yatupasayo kufanya,MSIJAFISHE NA NYIE WANAWAKE,kwasababu mnatupa wakati mgumu mno wakati wa mchana na jioni kwenye daladala,sijui mkitumika lunch time kwenye guest bubu zetu hamkogi?
Kipenda roho bana hivi unajua kuna nguo za bahati? Kwani katiba inakataza kuvaa nguo wiki?
Jeans tofauti na flana au shati haitakiwi ifuliwe saaaana unaharibu hata show yake
Hawa watu wakitema wanatema kweli..fukuto lake si la kitoto ati!!
Mwambie mpwa. Heshima ya jeans ukiivua uisimamishe isimame yenyewe.