Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,701
- 6,936
Ewe mwanaume tengeneza mazingira rafiki kwa ajili ya ustawi na afya za mama dada mtoto ndugu na jamaa zetu wakike. Inasemekana aslimia kubwa wanaume huwa ni wachafu sana linapokuja suala la usafi na matumizi ya choo.
Je, unaongelea vyoo vya wapi? Nyumbani, ofisini, au public toilets au mashuleni au vyuoni? Kama public toilets na maofisini kuna gents na ladies, hivyo utakuwa umelenga majumbani labda kama kuna baadhi ya public na toilets za ofisini hazina huo utaratibu. Kama ni majumbani, je unaongelea nyumba za kupangisha vyumba au nyumbani kwako au kwenu?
Pia je, unaongelea aina gani ya choo? Kama ni urinal, iweje utumie urinal wakati wewe ni mwananmke?
Suluhisho la tatizo lako tayari lipo kiteknolojia ambalo ni uwepo wa urinal!