Raynavero
JF-Expert Member
- Apr 29, 2014
- 38,375
- 56,096
Habari za Ijumaa,
Pole na mihangaiko ya jua kali,
Nimerudi kwa wanaume wenye ndoa, tunajua wanaume wengi michepuko ndo mambo zenu ila sasa zisifike hukuu. Nina rafiki yangu ameolewa na wana watoto wanne na mwenziwe. Juzi mume karudi kaoga, amelala.
Mwanamke akaingia chumbani akakuta suruali ya mmewe imedondoka chini,akaikota ili aitundike juu. Akahisi kwenye mifuko kuna uchafu wa karatasi,kaingiza mkono kwenye mifuko ya suruali akatoa karatasi.
Akazifungua kakuta karatasi za hospitali za majibu ya HIV ya jina la mumewe na mdada mwengine wametoka kupima, yule baba kazisahau kwenye mifuko ya suruali, jamani mdada kapigia simu analiaa, nikamuambia tulia wewe majibu yanasemaje? Wako negative nikamuambia shukuru kakumbuka na kupima maana hayo ni mapito tu.
Ila huyu mume ni stubborn jamani, anapenda chini kashafumania sana dada wa watu mpaka na wadada wa kazi.
Sawa tunajua kubadilika kua na mke mmoja hamuwezi kwa hila zenu, but at least heshimu mkeo basi kama unagonga show za nje gongea mbali na makazi yako, kaa Kinondoni, chepuka Gongo la mboto na usitengeneze mazingira mkeo akajua loohh!
Mnatia aibu sana na mnaumiza sana wanawake zenu.