Wanaume 'msio na pesa' hapa tu ndo mnapokosea

Wanaume 'msio na pesa' hapa tu ndo mnapokosea

Tusio na pesa tujae kwa wingi kwenye uzi huu kuna fursa ya mdau masharti yake ni nafuu yaan "USIJIKWEZE" mkiwa kwenye bata
Unaniitia Mingo mkuu....hahahahaah
 
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji113]
 
Kwa hili umetuweza aiseeee, ila sometime unakuta nakufanya mchepuko bila kujijua sasa nakuonea huruma siku nikikuacha lawama zitakua nyingi, mara yani nimetumia hela zangu kukulipia out nikijua utanioa, sasa ili tusilaumiane sana mwishoni inabidi tu nilipie kupunguza lawama.
 
Wanaume wengi, hasa wa JF wanalalamika sana kuwa wanawake tunataka wanaume 'wenye pesa' au waliofanikiwa tu. Pia kuonesha hii (kukubalika bila kuwa na pesa au kuhonga) ndio concern kwa wanaume wengi ni pale nyimbo nyingi za Kitanzania message ni hiyo hiyo, mfano: "Japo sina kitu,......", "Ukawaacha wenye pesa......" Tukilala njaa......"

Nikirudi kwenye mada, Kukosa pesa sio tatizo!!!!!

Mimi ni mtu ninayependa finer things in life. Napenda vitu vizuri na sisubirii mtu anipe. Kwenye kujipa raha sinaga subira wala uoga, najigharamia. Halafu kingine ni kuwa I am generous, sio mchoyo kabisa. Kuwa na mimi na utaexperience kila ninachoexperience. Ukiwa mtu wangu automatically ntakuinclude nikienda shopping, movies, nikipanga safari ya bata nakujumuisha na kila kitu.

Sasa unakuta uko kwenye mahusiano na mtu, akishajua jinsi unaendesha maisha yako anataka kujitutumua kukuimpress. Anataka kukupa huduma zile zile unazojipa mwenyewe au hata zaidi kwa pesa ambazo hana ili tu umuone bora zaidi. Inatia huruma!

Unakuta unamuinvite mtu out anataka kulipa wakati unajua kabisa hawezi kuafford, kwanini mnajitesa wanaume. Mtu ukishapendwa usiwe na hofu, ujue umekubalika ulivyo. Matokeo yake inabidi nishushe hadhi ya starehe zangu ili mpenzi aweze kuafford, ni kuikatili nafsi huko!!!!

Na mwanaume wa hivi atake kulipia kitu halafu umwambie hapana Weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee....mnuno wake hauishi leo. Atakuaccuse vitu kibao. Baada ya siku kadhaa unamkuta anakula karanga na kijoti, kisa kulipa Ankara zisizo zake.

Ndio maana wadada wanaishia kwa wenye nazo ili kuondokana na hali ya kuona huruma kila siku.
Mjirekebishe!!!!!!!!
4aca53eb9e7ee9196f2f245ff0e8f588.jpg
 
Sa unakuta mwanamke hana pesa wala kazi kutwa kutaja vitu vizuri vizuri tuu
Na huyu tusemeje!?
 
Kwa hili umetuweza aiseeee, ila sometime unakuta nakufanya mchepuko bila kujijua sasa nakuonea huruma siku nikikuacha lawama zitakua nyingi, mara yani nimetumia hela zangu kukulipia out nikijua utanioa, sasa ili tusilaumiane sana mwishoni inabidi tu nilipie kupunguza lawama.
Kwa wanawake wengine siwezi kuwazungumzia..ila mimi sina vinyongo aisee. Kutoa ni tabia sinaga motive nyuma. Na kama hali yako nzuri sio mbaya kumspoil babe wako lakini iweje ujipukute kila kitu ili tu kumuimpress mtu? Unataka yeye ajiskie vipi?
 
Kuwa na pesa ni relative term, kwa mmoja LAKI si pesa, wakati kwa mwingine laki is everything.
 
Back
Top Bottom