Wanaume mna nini na simu zenu?

Tuchki

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
1,740
1,441
Habari za leo wanajamvi,

Jamani leo nimestaajabu. Nikiwa nimetolewa dinner na shemeji yenu mtarajiwa huku tukibadilishana mawazo ya hapa na pale nikapata simu ya msiba sasa kwa kuwa sina salio la kutosha nikasema nichukue simu ya shem wenu ili nipate kujua zaidi juu ya msiba.

Lakini mwenzenu ile nimeshika simu tuu nikashangaa ghafla nimevutwa mkono yani mkono umenyongorotwa kidogo nitoe damu. Ile nataka kukimbia nayo nikavutwa mpaka mkono kidogo nivunjike. Hivi jamani wanaume mna nini ni vitu gani au siri zipi ambazo hampendi zijulikane.

Naombeni kujuzwa
 
Alikuwa anataka akusaidie kutoa password..!

Leo alitaka kuondoka na mkono, kesho ataondoka na kichwa.
Simu ya mwanaume ione kama mkwe wako.
duu hadi nimekimbia sura imebadilika kama simba
 
habari za leo wanajamvi.....jamani leo nimestaajabu.Leo nikiwa nimetolewa dinner na shemeji yenu mtarajiwa huku tukibadilishana mawazo ya hapa na pale nikapata simu ya msiba sasa kwa kua sina salio la kutosha nikasema nichukue simu ya shem wenu ili nipate kujua zaidi juu ya msiba lakini mwenzenu Ile nimeshika simu tuu nikashangaa ghafla nimevutwa mkono yani mkono umenyongorotwa kidogo nitoe damu...Ile nataka kukimbia nayo nikavutwa mpaka mkono kidogo nivunjike. Hivi jamani wanaume mna nini ni vitu gani au siri zipi ambazo hampendi zijulikane naombeni kujuzwa
Kwa nini hukuomba? Hukutumia ustaarabu, halafu ulitaka ukimbie nayo angekuvunja tu mkono, hapo wala usingeweza kujitetea maana angesema ulitaka kumpora!
Wanawake kumbe mnakuwaga na vitimbi vya hovyo hivyo..
Usishindane na mwanaume, mwisho utaumia na kushindwa tu!
 
Kwa nini hukuomba? Hukutumia ustaarabu, halafu ulitaka ukimbie nayo angekuvunja tu mkono, hapo wala usingeweza kujitetea maana angesema ulitaka kumpora!
Wanawake kumbe mnakuwaga na vitimbi vya hovyo hivyo..
Usishindane na mwanaume, mwisho utaumia na kushindwa tu!
kama mpenzi wake siruhusiwi kushika simu? jaman mbna wanaume mna kera yani nimeharibu hadi valentine yangu bora ningelala home tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom