Wanaume mmezidi vurugu

Wanaume mmezidi vurugu

Ukiona unaombwa sana pesa na kila mwanaume basi jichunguze vizuri inawezekana huna unachovutia wanaume zaidi ya hicho.. Tena hata x wako anakupigia kukuambia shida yake ya pesa!! Badili tabia kama maongezi yako ni kuonesha sana uwezo wako wa kifedha unapokuwa karibu na vidume utakopwa sana tu
 
Humu ndani mu wazima?

Kwanza naomba ieleweke kuwa mimi ni ke. Baada ya kuachwa chali. Nikiwa bado nina mapenzi ya dhati kwa aliyeniacha, niliumia kama mwanamke, nikaomba sana msamaha lakini mwenzangu alinijibu maneno ya kashfa kiasi kwamba naahindwa hata kuyaandika.

Baada ya maneno hayo, niliamua kuwa mtu mpya kabisa. Kwanza nilibadili lifestyle yangu na pia niliamua kujichanganya sana na marafiki. Niliamua kufocus kwenye maisha yangu na kutumia muda mwingi ninapokuwa mwenyewe kusoma na kuongeza maarifa zaidi.

Katika kujichanganya na watu mbalimbali, wameibuka vijana kadhaa walioonyesha interest ya kuwa nami jambo ambalo sijawahi kuliafiki. Wamekuwa karibu wakidhani pengine siku moja nitabadili mawazo.

Jambo la kushangaza sasa, vijana hawa wote, wanaact kama vile ndio tayari mmeanza kujenga future. Mara hoo najenga, tutahamia kwetu nikopeshe basi laki mbili nikamalizie nyumba. Mara hoo mama anaumwa sasa nimechacha pls nisaidie nitakurudishia. Kubwa zaidi hadi aliyenimwaga kwa kashfa naye anapiga kusalimia mara hoo naumwa sina hata pesa.

Mara hoo. Zimekuwa nyingi sana. Unajua mtu huyu ana kazi yake na mbaya zaidi anakupeleka hadi kwa wazazi wake bila ruhusa yako na bado wewe hujawahi kumwomba hata mia. Nyie wanaume badilikeni sasa.

Huku mnapoelekea si pazuri. Mnakua hamna tofauti na wale wadada wanaouza miili yao ili kupata pesa. Nina amini hawa watu hawana hisia na mimi.

Mnakera sana.

Karibuni kwa mapovu.
Nikimpata mwanamke ambae hapigi mizinga ambayo haina kichwa wala miguu ntampenda milele
 
Ulivyosema 'wanaume' utafikiri wanaume wote ni watu wa vizinga hemu jiheshimu kidogo binti
 
Ukiona unaombwa sana pesa na kila mwanaume basi jichunguze vizuri inawezekana huna unachovutia wanaume zaidi ya hicho.. Tena hata x wako anakupigia kukuambia shida yake ya pesa!! Badili tabia kama maongezi yako ni kuonesha sana uwezo wako wa kifedha unapokuwa karibu na vidume utakopwa sana tu
Mtu hajui kama nina kazi ama la. Hajui lolote juu yangu. Kakuona saa Tisa lakini saa kumi na moja kapiga simu ya shida lol...
 
Hayo mambo yenu binafsi na ving'asti wako...
 
Unakutana na vijana. Tafadhali tupe heshima yetu wanaume. Pole sana kwa yanayokusibu.
 
Nimekuelewa saana.. wanaume wa hivyo wapo tena wengi tu.

Wachane then keep distance. Nimekusoma kwenye hizo lines nimegundua wewe ni mwanamke unayejielewa saana. Ila usije ukaanza kusema nami nakusandia. Kacomment kangu mwisho wake hapa
 
Hahaaa
 
Back
Top Bottom