Wanaume mmezidi vurugu

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Humu ndani mu wazima?

Kwanza naomba ieleweke kuwa mimi ni ke. Baada ya kuachwa chali. Nikiwa bado nina mapenzi ya dhati kwa aliyeniacha, niliumia kama mwanamke, nikaomba sana msamaha lakini mwenzangu alinijibu maneno ya kashfa kiasi kwamba naahindwa hata kuyaandika.

Baada ya maneno hayo, niliamua kuwa mtu mpya kabisa. Kwanza nilibadili lifestyle yangu na pia niliamua kujichanganya sana na marafiki. Niliamua kufocus kwenye maisha yangu na kutumia muda mwingi ninapokuwa mwenyewe kusoma na kuongeza maarifa zaidi.

Katika kujichanganya na watu mbalimbali, wameibuka vijana kadhaa walioonyesha interest ya kuwa nami jambo ambalo sijawahi kuliafiki. Wamekuwa karibu wakidhani pengine siku moja nitabadili mawazo.

Jambo la kushangaza sasa, vijana hawa wote, wanaact kama vile ndio tayari mmeanza kujenga future. Mara hoo najenga, tutahamia kwetu nikopeshe basi laki mbili nikamalizie nyumba. Mara hoo mama anaumwa sasa nimechacha pls nisaidie nitakurudishia. Kubwa zaidi hadi aliyenimwaga kwa kashfa naye anapiga kusalimia mara hoo naumwa sina hata pesa.

Mara hoo. Zimekuwa nyingi sana. Unajua mtu huyu ana kazi yake na mbaya zaidi anakupeleka hadi kwa wazazi wake bila ruhusa yako na bado wewe hujawahi kumwomba hata mia. Nyie wanaume badilikeni sasa.

Huku mnapoelekea si pazuri. Mnakua hamna tofauti na wale wadada wanaouza miili yao ili kupata pesa. Nina amini hawa watu hawana hisia na mimi.

Mnakera sana.

Karibuni kwa mapovu.
 
Karibuni kwa mapovu.
Dada, kwanza pole kwa kumwagwa,ila mwisho wa safari moja ndio mwanzo wa safari nyingine. Maisha lazima yaendelee, kusupportiana kwa vitu vidogo vidogo ni jambo zuri, kama unaweza saidia, saidia, unajua wote ni watoto wa wakulima na sometimes opportunities zinagoma, hawa wenye ajira zao nao wameshakopa kila benki, kwa hiyo wana mshahara jina tu...
Kipindi hiki sio kizuri sana kiuchumi kwa watu wengi, so pale unapoweza piga tafu, fanya hivyo na Mungu akubariki. Mwisho nakutakia umpate umpendaye, na yeye akupende ila pia awe na kipato kizuri aweze kukupa bata zote bila kukwama kwama...
 
Sasa mkuu kwa siku moja unapata maombi ya matano kweli hizo baraka so zimepitiliza?
 
Back
Top Bottom