Wanaume mliooa tulieni na wake zenu

Wanaume mliooa tulieni na wake zenu

Kwani ulilazimishwa umpe namba si kiherehere chako, mpaka kufikia hatua ya kumpa namba ya simu inamaanisha na wewe umempenda.
Nyie wanaume mliooa tunaomba mtulie na wake zenu. Kama mlioa kwa bahati mbaya ni juu yenu. Msiwe mnatusumbua wengine kabisa kwanza mnatupa gundu tu ambao hatujaolewa, kaeni ma wake zenu. Nani anataka kuwa mchepuko siku zote? Alaa!

Mwanaume umeoa kazi kupigia simu tu wanawake, mara video call si muwapigie wake zenu kwani mmeambiwa hawataki kupigiwa? Sie tunapambana na ambao hawajaoa hao wapige hata pote ruksa, sio mme wa mtu umepata namba tu unajipigisha simu tu haipokelewi wala hujiongezi kwanini huyu hapokei bado tu, badilikeni!

Mnatuma SMS za mapenzi mnatutia mashakani wake zenu wakikuta mnapenda tugombane sio? Mume wa mtu anaaandika nakupenda eti nikujibu nakupenda pia khaa , mlioolewa mna kazi aisee muwe mnaiba simu mnachungulia muone waume zenu ambavyo hawatulii.

Sipendi mme wa mtu aniambie nakupenda naona tu unanilaghai wallah we kama tunapiga game la mchangani tupige lakin hakuna mambo ya kuambiana nakupenda maana hutonioa wala hatuna mpango endeleevu.

Kuna huyo mme watu alipata tu namba yangu jamani hizo SMS zake sasa ananiambia unanitesa "pambafu"nakutesa nini kaa na mkeo huko mim nadeal na ambao hawajaoa tu waume za watu kaeni mbali tulieni na wake zenu kama hamridhiki mtajijua.

Wengine mna miaka hamjawahi kuwaambia wake zenu mnawapenda tumieni huo muda kuimarisha ndoa zenu sio kuhangaika kutafuta nyama. Nyama ni ile ile bucha tofauti tu..

Ifikie muda wanawake ambao hatujaolewa msiwapende sana hawa watu wanawapotezea muda tu ye ashaoa wewe je? Jua tu kuna sehemu mmeo yupo atakuja kwa muda wake tu.

Mama G ndio nishasema
 
Wanayatoa haswaa sasa wamekutana na mimi kiburi jeuri,jini mkata kamba napangua tu dish...
Watekenye tuu wamwage sisi tuko na pen tunaratibu waume watu shemeji zetu ili tueshimiane hakuna mambo ya shemeji bae [HASHTAG]#SAYNOMORETOSHEMBAE[/HASHTAG]
 
pole ila nahsi aliyekuplkea kuuandika uzi huu n mwanaume yule ambaye ana au amekutongoza alafu ww humpnd cos hata angekuwa hana mwanamke usingempnda piaa...so ninaimna kama angekuwa kaukalia moyo wako usileta uzi huu na ungeneng'eneka nae hata kama ana mke...
 
Pole lakini dada ila unatakiwa ujue jambo moja kwamba wanaume waliooa hawajaanza leo wala jana kuchepuka, tangu enzi na enzi mambo haya yalikuepo.Ukiona anakusumbua sana mpige block.
Nishalipiga block
 
pole ila nahsi aliyekuplkea kuuandika uzi huu n mwanaume yule ambaye ana au amekutongoza alafu ww humpnd cos hata angekuwa hana mwanamke usingempnda piaa...so ninaimna kama angekuwa kaukalia moyo wako usileta uzi huu na ungeneng'eneka nae hata kama ana mke...
Bonge moja la point.
 
pambana na ambao hawajaoa lakini wana mtoto kama wewe ucje kuwazibia chance wale ambao hawajaolewa na pia hawana mtoto
 
Back
Top Bottom