Wanaume mliooa tulieni na wake zenu

Wanaume mliooa tulieni na wake zenu

Nyie wanaume mliooa tunaomba mtulie na wake zenu. Kama mlioa kwa bahati mbaya ni juu yenu. Msiwe mnatusumbua wengine kabisa kwanza mnatupa gundu tu ambao hatujaolewa, kaeni ma wake zenu. Nani anataka kuwa mchepuko siku zote? Alaa!

Mwanaume umeoa kazi kupigia simu tu wanawake, mara video call si muwapigie wake zenu kwani mmeambiwa hawataki kupigiwa? Sie tunapambana na ambao hawajaoa hao wapige hata pote ruksa, sio mme wa mtu umepata namba tu unajipigisha simu tu haipokelewi wala hujiongezi kwanini huyu hapokei bado tu, badilikeni!

Mnatuma SMS za mapenzi mnatutia mashakani wake zenu wakikuta mnapenda tugombane sio? Mume wa mtu anaaandika nakupenda eti nikujibu nakupenda pia khaa , mlioolewa mna kazi aisee muwe mnaiba simu mnachungulia muone waume zenu ambavyo hawatulii.

Sipendi mme wa mtu aniambie nakupenda naona tu unanilaghai wallah we kama tunapiga game la mchangani tupige lakin hakuna mambo ya kuambiana nakupenda maana hutonioa wala hatuna mpango endeleevu.

Kuna huyo mme watu alipata tu namba yangu jamani hizo SMS zake sasa ananiambia unanitesa "pambafu"nakutesa nini kaa na mkeo huko mim nadeal na ambao hawajaoa tu waume za watu kaeni mbali tulieni na wake zenu kama hamridhiki mtajijua.

Wengine mna miaka hamjawahi kuwaambia wake zenu mnawapenda tumieni huo muda kuimarisha ndoa zenu sio kuhangaika kutafuta nyama. Nyama ni ile ile bucha tofauti tu..

Ifikie muda wanawake ambao hatujaolewa msiwapende sana hawa watu wanawapotezea muda tu ye ashaoa wewe je? Jua tu kuna sehemu mmeo yupo atakuja kwa muda wake tu.

Mama G ndio nishasema
Kwa tajiri cha nini maskini nitakipata lini??
 
Aiseee
Mara nyingi huwa ni makubaliano yao wawili, ka mtu hapendi hizo nakupenda na ukamwambia mchepuko wako lazima aelewe tuu!!
Kama mie napenda hizo I love you jamani!!

Babu Asprin nakupenda mwaya, ingawa uliwahi kuwowa, najua ningezaliwa mapema ungeniwowa mie badala ya sky!! Teh
Sakayo mchepuko wangu mwaminifu upo??
 
Tatizo ni mazoea tu, Wanawake wengi wakishaolewa wanajua wamemaliza wanaanza kuzingua na hilo ni kosa kubwa wanalofanya wengi....."Sisi wanaume hatuzoeleki kama kanga"
 
"Mnapambana na ambao hawajaoa wapige hata kote ruksa"hapa unamaanisha nini dada.
 
Hapana gudume jaman ni kikohozi msg sent waume za watu muache usumbufu
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]duh nimekuwa dume leo

Mm Demiss bhn aka Gujikeee

[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Tumekuskia... muda mwingine tuna wapa tulizo tu. Sasa mnafikiri mtahudumiwa na nani kimapenzi?
 
Kumkataa mwanaume kwa sababu ya kudanganya..ni sawa na kukimbia nchi inayonyesha mvua.....mvua inanyesha kokote
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]duh nimekuwa dume leo

Mm Demiss bhn aka Gujikeee

[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Khaaaaa [emoji15][emoji15][emoji15] hiyo avatar ilinivuruga nilijua gudume [emoji3][emoji3] demiss wewe
 
Back
Top Bottom