Mpasuaji wa Manesi

JF-Expert Member
Mar 13, 2016
299
1,370
Wanaume,

Sherehe ni jambo lililowekwa na wanadamu ili waweze kufurahia mafanikio yao na wengine hufanya sherehe wakati wa kuomba Dua kwa miungu yao.

Vilevile Sherehe ilikuwa ni swala ambalo hufanyika kuonyesha Mwanzo au Mwisho wa Maisha fulani au hatua fulani katika Maisha. Mfano; Kuzaliwa kwa Mtoto, Kijana anapokua(kutahiriwa), Kuzaliwa kwa familia(NDOA), Kuanza kwa msimu mpya(Msimu wa kupanda au wa kuvuna) na mwisho wa uhai (Msiba).

MY POINT
Katika hizi Sherehe zilipokuwa zinafanyika, Wanaume na wanawake kila mmoja alikuwa na jukumu lake katika shughuli hizo. Wanaume walikuwa na majukumu ya kulinda(security) na kusimamia shughuli mbalimbali huku wanawake wakiwa na jukumu la mapishi, kuwapokea na kuwaburudisha wahudhuriaji katika style za uchezaji ambazo hazikuwa za kuvutia kihisia (erotic or sensual).

Uchezaji wetu ulikuwa wa kiume na ulionyesha uanaume, Wanaume waliruka juu, walichanganya miguu, walitikisa mabega, walicheza kwa kupeleka miguu katika mtindo unaofanana nk. Na Wanaume waliocheza vizuri zaidi basi waliwavutia sana Wanawake waliokuwepo eneo hilo.

Style zote hizo za uchezaji wa Wanaume zilionyesha Ujasiri, Nguvu, Kujiamini na wakati huo huo Style za uchezaji za wanawake zilionyesha femininity na Motherhood.

Wanaume waliolewa sana, walizuiliwa kucheza kwasababu wangeweza kujidhalilisha kwa watoto wao, wangekosana na wazee au wangekasirisha Miungu. Na Sherehe pia zilihusisha michezo mbalimbali kwa lengo la kuchombeza.

LAKINI, nini kilichopo sasa hivi?
Tumekuwa na kundi kubwa la vijana kwa Kiume wanacheza kwa kupinda viuno, wanatikisa matako, wanakuwa wanacheza kama Makahaba. Na kuna wengine wanacheza kwa kujibana na kusugua tupu za kiume nyuma ya makalio ya Wanawake(wanabambia), na ufalla zaidi wengine wanakojoa (Ejaculate) wakiwa katika style hio ya uchezaji.

Mwanaume kuwa na mipaka katika uchezaji wako, hakikisha vinyocheza ni Mabega na Miguu tu, ni aibu sana Mwanaume unatikisa makalio kuzidi hata wanawake.

Swala la kuonyesha ubora wa mtikisiko wa makalio na kunyonga viuno waachie wanawake.

Be a Man, Respect yourself.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom