Wanaume Madaktari bingwa wa kinamama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume Madaktari bingwa wa kinamama

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by nyumba kubwa, Jun 21, 2011.

 1. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,725
  Trophy Points: 280
  Jamani nilikuwa nasikiliza BBC sasa hivi nimecheka sana. Nchini Burundi akina mama na kina baba walikuwa wanahojiwa kuhusu mwanamke kutibiwa na daktari wa kiume hasa wakati wa ujauzito.

  Akina mama wanasema wanasikia aibu sana lakini hawana jinsi kwani kuna madoctor bingwa wa wakinamama wawili tu wa kike Burundi. Wanasema madokta wanawachezea, na wao wanajisikia vibaya ila hawana jinsi. Mama mmoja anasema mume wake alimuuliza aliyekupima ni dokta wa kike au wa kiume akamjibu wa kiume; mwanaume wacha asikie wivu.

  Wanaume nao wakahojiwa wanasema hawapendi kabisa wake zao wahudumiwe na madoctor wa kiume lakini wafanyeje. Kuna mmoja kaniacha hoi anasema aliongozana na mkewe clinic, kufika kwa doctor doctor kamwambia atoke nje ampime wife. Akamwambia doctor kwa nini nitoke na huyu ni mke wangu na namjua vizuri hakuna cha kunificha? Dokta kakomaa mpaka jamaa katoka. Sasa mwandishi akawa anamhoji jamaa, uoni kuwa daktari hataweza kufanya kazi yake vizuri ukiwepo; jamaa inajibu, kwani mimi nashikilia sindano si natazama tu na kucheki usalama.

  Aaah. That is why mi niliamuaga kwenda regency.
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  ha ha ha... umenikumbusha story moja... Jamaa kamchukua mkewe na kumsindikiza
  kwa Doctor wa wanawake.. kufika pale anakutana na jamaa alosoma nae - Huyo jamaa
  alikua ni kiwembe saana na siku zoote alikua akikiri kua atakuja kusomea udaktari wa wanawake
  ili awe analipwa kuzichezea..lol.. Jamaa anamuuliza mkewe "Huyu ndo Dr wako wa siku zoote?"
  Akamwambia ndio for the last three years....lol
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  tehe tehe pale marie stopes mwenge yupo dr mkini na sasa kuna dogo mya yupo pale hardly ana 35 yrs halafu ana babyface flani anaonekana km kijana mdogo. sasa nikiwaangalia wengine akina mama watu wazima wakimuona mpaka wanatingisha vichwa wanaooona kweli kazi ipo. jamaa na yeye kazi anayo nadhani atakuwa kila wakati lzm kitu kiewe hewani
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Jibu hapo ni kuwa mwenye vyake awepo wakati wa shughuli yote ili kuhakikisha mambo yanakwenda salama..............................vinginevyo dokitari huyo aweza kuchakachua mazingira......Mmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhh
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
   
 6. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,725
  Trophy Points: 280
  Ukiwepo unaweza kuanzisha varangati kwani mambo wanayoyafanya ni bora yabaki kuwa siri kati ya doctor na mgonjwa. Haina tofauti na fore play


   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Hapo ni jamaa kuishiwa pozi... Dr huyo ndo the best na si unataka what is best for your wife...lol
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Unajua this is one of the reasons kwa nini utilization ya maternal health services kwa wamama wengi. Nadhani kuna haja ya kuangalia hili kwa undani kwa sababu linachangia sana kurudisha nyuma efforts towards realization of ile Millenium Goal inayolenga kureduce maternal death at least by 75% by 2015 ............

  (Naomba mwenye information zaidi juu ya hili anisaidie...am interested)
   
 9. A

  Adam waTZ Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Daah hata mimi ningependa sana kuwa daktari ili wakinadada wanaotoa mimba ni lazima kwanza halafu kazi inafata maana nitampima ukimwi kwa hiyo ntakua huru
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  MJ1 katika vipengele ambavyo vinachangia failure katika "Realization of Millenium Goal" inayolenga ku reduce maternal death (Hii iko chini ya uangalizi wa karibu na International community - World Health organisation ikijulikana kama Millenium Goal 5).. Hio ya daktari wa kiume kutoa huduma ndo kusababaisha ina nafasi ndogo saana katika nchi zetu za kimaskini. Na kwa wale ambao tumebahatika kuzaa unakuta ni bora uhudumiwe na mwanaume for they are so sensitive and considerate..... naona ile hali ya kuona wanawake wanatoa watoto zao kwa hio njia ya kuzaa hata scissor huchangia saana wawe na compassion.

  Sababu kubwa zinazochangia a lot of maternity deaths and birth rates ni tu ule umasikini ulokithiri... umasikini ulopelekea mhusika kutokua na access ya hiyo huduma ya muhimu ya kuzaa, aidha anaishi interior yuko mbali na zahanati, aidha chakula cha shida mno anakua malnourished, aidha hajajiunga na huduma ya Clinin sababu iko mbali na mambo kibao - Hayo mambo yakichangiwa saana na serkali in things such as miundo mbinu, zahanati na hospitali mbali mbali kukosa huduma kama umeme, vifaa, maji na dawa, Na Mengine meeengi...

  MJ1 hivi nilivyo jibu did i get you?? or niko nje ya swali lako??
   
 11. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Heheeee! hayo mambo yapo sana
  Madoctor wana mambo kuna dada yangu mimba iliharibika kaenda kusafishwa hospital doctor wakumsafisha alikuwa ni wa kiume alivyomaliza kumsafisha akamwambia kuwa ana k nzuri, je huyo doctor alikuwa na maana gani kusema hivyo?
   
 12. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Angemtibu yeye sasa, mwenzake amesoma na kua daktari wa wanawake kwa malengo, kuwachezea na kuwafanyizia wanawake ndio zao. Safi sana madaktari wa Congo!
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Umenisaidia sana mpenzi yaani nilikuwa najiuliza sana nini kinachotukwamisha??.........lakini ukiangalia mbona tunaambiwa kuwa huduma hizi ni free na at least sasa zimesogezwa zaidi sana na watumiaji (kuna ile mnaita sijui Sisterhood nini nini kule) but bado hali si swari. Nakubaliana na wewe mambo ya chakula na lishe, usafiri (unfortunately definition ya Exceptions and Waivers katika Cost sharing policy haikuangalia vitu kama hiv) but najaribu tu kuwaza what will be the role of cultural factors in explaining the low level of utilization of these services? Ofcoz hii ya wahudumu wa kiume nadhani inamatter sana vijijini ambako bado watu wana attachment na culture zao na TBA bado wana nguvu... au?
   
 14. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,725
  Trophy Points: 280
  Culture inaweza ikachangia. Kuna shangazi yangu alikuja kututembelea toka kijijini. Miaka ya 80s. Alikuwa mja mzito. Huwezi amini alipopata uchungu kaenda migombani na mdogo wake akamzalisha ilikuwa usiku. Baba wacha aje juu. Nadhani mazoea ya kutumia wakunga wa jadi ambao ni wanawake inaweza kufanya wamama vijijini kuprefer kuzalia majumbani kuliko hospital sababu ya aibu. Ni ngumu ku conlude bila research ila nadhani we need a research on that. Kwamba ni kweli watu wanazalia majumbani kwa kuwa hakuna hospital karibu au kuna walio na acces na hospital na wanaziogopa?


   
 15. charger

  charger JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mh inataka moyo sana namshangaa hata huyo aliyekuwa ana ng'ang'ania kuwepo wakati wife wake anakuwa attended,oh oh inafika point eti kajamaa kanapima njia sjui unakuta kanafumba jicho moja huku kanaangalia juu vidole ndo vinacheza maeneo yako ya kujidai,unaweza rusha ngumi haki ya nani!!
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  MJ1 dear with the information you have given me it seems you are really interested as i am and thus you are well aware of most... l love that for ni wadada wachache ambao hua interested as much as they are women... Hio habari ya kusema kua ni bure - ni kweli but haya basi is there a frequent flow of these maternal health related necessities?? Kuna usimamaizi mzuri wa kuhakikisha kua they are used inavyotakiwa?? - as in most health related worker huchukua wakaa nazo after a certain period wanarudi nazo na kuuza hizo hizo....

  Kuhusu mambo ya cost sharing... sincerely hapo no question ilitakiwa hata isiwepo kabisa... as in your own words "Exceptions and Waivers ktk Cost Sharing Policy " ina upungufu, tena mzito - thou they do claim haopo but hizi ni siasa tu za maamuuzi but fuatilia... hizo medicine bureaucracies zinachefua!! They do not even care kwamba the person in question is a pregnant woman in need of immediate attention. Tukizungumzia Cultural factors... MJ1 acha hizo dear... i can write a paper of hata 15 of cultural factors in explaining the low level of utilization of these services for katika nchi yetu hii the one of the most crucial aspect to be obseved hasa ukiangalia ethnic groups, tribes and religion... wacha tu hata the mfumo dume wenye pretence ya kusema umeeisha while other wise... BUT at the end of the day it will be no news for you... because if you know of the weeknessess za Exceptions and Waivers in cost sharing Policy especially related to health then my dear you have a great idea of Culture and its role in the world of pregnant women na related problems wakiwa kti situantion...

  Upande wa wahudumu wa kiume najua ina matter vijini ila bado nina msimamo ina matter at minimal compared to other factors...
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  haa hha ha, Charger bana!...LOL!
  miiko ya udakitari inazingatiwa jamani, hebu acheni watu na fani zao...
  (ashakum si matusi!) bila 'kutekenya' njia itafungukaje?
   
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  We Bidada natamani nikuone live tudiscuss hii mambo. Aksante sana umenifumbua macho katika mengi........... Ni mangi yako under culture hata sijui niframe vipi.... kuna swala la dini ( amballo pia ni elelment ya culture).........Tanzania kama sikosei elimu au uelewa wa umuhimu wa maternal health mwanamke anaupata pale anapokuwa mjamzito!! yaani anapokwenda antenatal clinic kwa mara ya kwanza ndo huanza ku'hubiriwa' umuhimu wake kwa yeye na mwanae,,,,,,,tunasahau kuwa kuna circumstances nyingine ambazo hiyo'mara ya kwanza' inakuwa hindered....mano binti ambaye amepata ujauzito katika umri mdogo..jamii inamcondemn.........anaona aibu anajificha mwisho wa siku 'mara yake ya kwanza' inakuwa siku ya kujifungua ...sasa kama kuna tatizo litachelewa kuwa dictected during early times!Not only that lakini pia kuna zile sehemu (hasa vijijini) ambako wazee i.e. wamama watu wazima ndio wanaaminika kuwa na 'elimu' juu ya uzazi, mama anapata shida anaambiwa ni kawaida, au mimba si ugonjwa jikaze......hadi hali inapokuwa mbaya ndio anakiri kuwa kashindwa....na hawa haijalishi kama zahanati iko jirani au lah! Inasikitisha kusema ukweli..........

  Nakumbuka nilikuwa naongea na mdada mmoja wa kihaya akanambia kuwa kimila mama mjamzito akiumwa na uchungu kama ndani ya nyumba kabaki na Baba mker hawezimwambia!! au akimwambia Baba mkwe hawezimsaidia..........sasa hali kama hii inawezaleta maafa!
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...hivi nyieee?!....mmefungua semina hapa? lol!
   
 20. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...utani mbali,....kiukweli kuna madaktari wachache sana Gynecologist wakike nchini, naamini hata nje ya nchi.
  Unapo i frame akili yako kwamba mjamzito ni sawa na ugonjwa, nadhani haitokuwa busara kuchagua mganga.
  Kwenye ujauzito kuna mengi, ...complications wakati wa kujifungua nazo ni nyingi...kuna breech, kuna kifafa cha mimba,
  na mengine mengi...

  Kwahili la ujauzito hakuna jinsi, nitapanga foleni tu kwa Doctor Shaffiq pale Aga Khan, amalize ujuzi wake apendavyo.
  Upande wa pili wa shilingi,....kina baba siku hizi prostate cancer ni mojawapo ya gonjwa lililoshika kasi!
  Ili dakitari aweze kupima enlargement ya hiyo prostate, inabidi aingize kidole kwenye nanihii....mnh!...

  Kwakweli yataka moyo jamani, mungu atuepushilie mbali!
   
Loading...