Wanaume Madaktari bingwa wa kinamama

Sijui kwa nini Masangoma wanaaminika sana kuliko ma-Daktari wa ukweli, Sangoma akisema mwache mkeo akae hapa kwangu nitamfanyia dawa kwa mwezi mmoja, wanaume huwa hawalalamikii, hasa wanawake wenye matatizo ya kutopata mimba, utakuta Sangoma anasema eti inabidi dawa ya kufungua kizazi anaipaka ktk nanihii yake ya kiume ndyo itakayotumika kusugulia dawa ukeni iingie vizuri, kutwa mara mbili kwa mwezi, akina mama hawalalamiki!
 
Mimi nimehudumiwa na madaktari wa kike na wa kiume mara zote sijawahi ingizwa vidole ingawa nimewasikia marafiki zangu wakilalamikia kupimwa njia kwa vidole kila wanapoenda clinic.
 
Ni kweli hatuumwi, kwani mimba kama wasemavyo watu si ugonjwa. Kwa hiyo you can plan and choose a doctor!

Nafikiri nyie mnaochagua madactari hamuumwi. Hivi kweli Maria stopes kuna madaktari? wote naona ni vihiyo tu kazii yao kubwa kutoa mimba, Gyno mwenye miiko hawezi kutoa mimba unless kuna tatizo kubwa sana. Mii gyno wangu ni mzee yuko pale Regency (muhindi) sijaona ananitia kidole popote labda kuwe na tatizo kubwa. Gyno anayepenad kuvua nguo za watu kutia vidole huyo ana ualakini.

Poleni sana nyie wenye gyno feki mtaishia kuweka vidole tuuu hata sehemu zisizo.
 
Ok niwaambie kitu dr ni dr awe wa kike au wa kiume wote wana maadili yale ambayo walifundishwa kuwafanyia wagonjwa hata mimi ni dr wa kike sijaona tofauti kati yetu napenda kuwaeleza wenzangu either mwanaume au mwanamke humu jamvini usichague dr kwani hujui yapi yatakukuta
 
kasheshe wanapataga kikienda kibibi kizee ambacho hakijaosha nanilihi...niliipataga hiyo kwa mshikaji wangu yeye rafiki yake Bingwa wa wanawake...alikoma lkn afanyeje...
 
Tunajua kuwa kuna ethics na hakuna aliyebakwa na dr. Tatizo aibu ndugu yangu. Ndio maana kwa sisi wengine tuna prefer dr wa kike. Tunatofautiana wengine hawajali na hawaoni aibu.


Ok niwaambie kitu dr ni dr awe wa kike au wa kiume wote wana maadili yale ambayo walifundishwa kuwafanyia wagonjwa hata mimi ni dr wa kike sijaona tofauti kati yetu napenda kuwaeleza wenzangu either mwanaume au mwanamke humu jamvini usichague dr kwani hujui yapi yatakukuta
 
dokta ukienda na mkeo
anakwambia tupishe,,nenda nje,,
halafu kabla hujatoka anamwambia mkeo vua nguo ulale kitandani..
halafu unamlipa pesa..
unaweza huyo kukuta huyo mwanamke mpaka anakuvulia nguo
ulitumia pesa nyingi,,,,
yeye anavuliwa bure na kulipwa juu...
inaumaaa....
The Boss..umenichekesha sana kwa post yako

Kwenye nchi zilizoendelea, unaweza ukakaa kwenye examination room mkeo akiwa anahudumiwa, ama hata akiwa anajifungua. Pia unaweza kushirikishwa katika kila hatua, kwa kuwa kuna nafasi na infrastructure inaruhusu. Fikiria kama katika hali ya kawaida ingewezekana Amana ama Temeke, ambapo kunakuwa na daktari mmoja anayesubiriwa na akina mama 20 walio tayari kujifungua, yeye anatakiwa afanye vipimo vyote, na ahakikishe wanajifungua salama. Je mtu huyu katika hali ya kawaida anaweza vipi kukaa na mmoja kwa muda mrefu?..pia fikiria katika hali ya kawaida, wakina mama 20 wote wako uchi wakiwa wanasubiri kujifungua, katika chumba kimoja, je inawezekana vipi Baba akubaliwe kuingia ndani kutoa support?. Hata kama wangeruhusiwa isingewezekana katika hali ya kawaida. Pili, huduma ya uzazi, japokuwa inahusisha watu wawili, yani baba na mama, ila muhudumu anapaswa kuhakikisha kwanza mama yuko tayari kwa mtu mwingine hata kama ni mume wake kuwepo eneo la tukio. Kule Labor ward kuna mambo mengi sana ya siri, ni siri za mama na muuguzi wake, ambazo hata baba hutakiwi kuzijua. Ni siri ambazo muuguzi na daktari wanazitunza na muuguzi ameapa kutozitoa. Kuzitoa ni kosa kubwa la maadili.

Finally, Ni kweli kwamba daktari hawezi kukumbuka umbile la mkeo hata kama atamuhudumia mara kumi, ukitoka hapo ameshasahau hata rangi ya nje tu, wanaona wengi sana, tena wenye maumbile tofauti tofauti, na sio rahisi kumkumbuka hata mmoja haswa nyeti zake. So kusema kwamba wanafaidi na wanalipwa, ni kuwaonea bure,..actually, inapunguza sana hamu ya kujamiiana hata na wake zao,..you can imagine!

stun
 
Ila kweli Mbu wamama wengi huwa wana develop mapenzi ya ajabu na doctor wakati wa ujauzito. Mimi nina similar experience but thanks God daktari wangu huwa ni mwanamke always. Yaani sometimes you just feel like seeing the doctor without any reason. Na nimepitia vitabu vya mambo ya uzazi wanasema ni kawaida kwa kuwa dokta anakuwa karibu nawe wakati mwingine kuliko mumeo. Mnaelewana zaidi lugha. So when you feel loney unaeda mara unasingizia mtoto achezi mradi muonane.

Mapenzi na mtoa huduma ni swala jema, kutengeneza mahusiano mazuri kunakufanya usiogope kuuliza chochote, na pia kuzingatia yale yote anayokuambia. Inakupa nafasi ya kushiriki katika matibabu anayokupa, na kuyaamini zaidi. Pia hii inategemea na jinsi daktari anavyo-m-handle client wake. Kuna wale ambao mtu hataki kurudi kwake, ila kuna yule ambaye lugha yake tu unajisikia umepona. Ni kweli kuwa madaktari wa akina mama ni watu wenye huruma sana, maana wamezoea kuwaona katika maumivu, disappointments, na frustrations,..na wameshajifunza kupanga maneno kutokana na mazingira na mood yako, na ndo sababu unaona kama kila unachokiongea mnakuwa kwenye page moja. Ni kwa kuwa ameshakutana na watu wengine mia wenye hali kama ya kwako exactly, so anajua what will follow..., kitu ambacho hata mumeo hawezi maana huo ndo ujauzito wako wa kwanza, na hata wa pili hauwezi kuwa sawa na wa kwanza.
 
Mimi nimehudumiwa na madaktari wa kike na wa kiume mara zote sijawahi ingizwa vidole ingawa nimewasikia marafiki zangu wakilalamikia kupimwa njia kwa vidole kila wanapoenda clinic.

@Jomse, ni kweli kuwa kama swala ni ujauzito tu, PV examination sio swala la kawaida. Labda kama wamehisi kuwa njia inafunguka kutokana na lalamiko lako. Ila kama ni swala la magonjwa ya akina mama (gynaecological problems), say kutokwa na uchafu wenye harufu, ama damu pasipo mimba, lazima akuangalie, asipokupima (PVE), anakuwa hajakutendea haki. For normal antenatal visits its very very rare kufanyiwa hicho kipimo cha vidole. Ila uchungu ukianza, hakiepukiki.
 
Madaktari hovyo sana, tena ukute mlevi duh!
unakumbuka ule usemi wa wahenga "usitukane wakunga....."
sasa hapo ndugu yangu Gagurito umefanya mjumuisho wa kila mtu kuwa ni wa hovyo. Kila binadamu ana mapungufu yake, na ana mazuri yake pia. Ulevi pekee sio tija.
 
Lakin kisheria kabisa mke wako kama anakwenda kwa doctor na kunacomplication ambazo zinahitaji apigwe nusu kaputi inaruhusiwa kuomba nesi awe naye kama watakuzuia wewe,kwenye nchi zilnazoendelea kama china mwanaume unaweza kuomba kushuhudia mke wako akijifungua lakini lazima utoe two weeks notice wakupime afya halafu uhudhurie.

Kule kwetu ndugu yangu hii ni ngumu sana. Tunakuwa na common labor ward ambapo kuna wakina mama wengi wako katika stages mbali mbali za kujifungua, hata kama tungewaruhusu akina baba kushuhudia uzazi, wasingeweza, maana hamna privacy. hata kitamaduni, hatujawaandaa akina baba kiasi hicho, wanaweza kuogopa kuwagusa wake zao baada ya kushuhudia mamumivu ya uzazi nakwambia..hahaha..
ila tafiti zinaonyesha kuwa, ni kweli uwepo wa baba wakati wa kujifungua mama, kunaongeza care, na kunatengneza bond zaidi na mtoto aliyezaliwa.
 
I beg to dis agree with you, kina mama wengi tu wanafia aghakhan na hospitali za mjini kuliko hata huko kusiko kuwa na hospitali?Ushasikia hg kapewa mimba bahati mbaya kafa? Ni very rare, wake zetu mayai hawa ndio wanaoshindwa kupush pamoja na access ya huduma bora!
Ndugu Watu, ni kweli kabisa, Dar ina Maternal mortality ratio kubwa zaidi ya wastani wa taifa kwa sasa. na ni mjini. Huko Aga Khan na Regency wakishindwa, na mgonjwa akiwa mahututi wanamsukuma haraka MNH ili akafie huko, apunguze idadi ya vifo katika hospitali yao, ili kuweka recors sawa. Ni mbaya sana maana unakuta mgonjwa ameshachelewa sana.
 
Madoc wengine wana mamikono makubwa balaa lol
dada Gaga, ni kweli kuwa mikono mikubwa inaweza umiza, kuna wengine vidole ni vidogo na vifupi, na pia ili waweze kufikia "cervix" inavidi kutumia nguvu, na wanaweza kukufanya ukajisikia vibaya zaidi hata wenye mikono mikubwa. But all in all, hicho kipimo (PVE) sio kipimo kizuri sana, wengi wanaofanyiwa hulalamika kuwa inasababisha "discomfort", na wakina mama hawakipendi basi tu, utafanyaje wakati ndo "gold standard?"
 
dawa ya ugonjwa sindano.mbona kawaida sana,mimi cjawai muuliza mama yangu nani aliyempa msaada wa kujifungua.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom