Wanaume huwa mnahitaji nini?

.

Screenshot_20210511-022244_Gallery.jpg
 
Habarini zenu ndugu zangu?

Kwa kweli inafikia kipindi nakuwa sielewi hizi ishu za mahusiano.

Mwenzenu nimekuwa kwenye mahusiano na mkaka wa miaka 33. Amenizidi miaka 4. Na tumekuwa naye kwa muda mrefu sana. Katika mahusiano yetu hayo, kiukweli sijisifii lakini nimejitahidi kuwa mwema sana kwake. Nimekuwa mnyenyekevu na msikivu sana kwa mwenzangu.

Tofauti na wengi wanavyosema kuwa ukiwa hivyo unaleta upendo lakini kwangu mimi naona inakuwa tofauti. Badala ya upendo, naonekana kama mtu mjinga ambaye nimekufa na nimeoza kwake kiasi kwamba siwezi kujitetea kwa lolote.

Tabia hii kwa mwenzangu, ikazua yeye kuwa na wanawake wengine kisirisiri na inapotokea nimegundua anataka kunifanya mimi nionekane nimemkosea adabu! Kweli nina madhaifu kama binadamu, lakini kwa upendo wa dhati kwa huyu mtu kwa kweli nilikuwa nao.

Yeye mwenyewe anajua na hiyo ilimtia sana kiburi. Sasa amezua tabia mpya. Inapotokea naona mwenzangu anafanya mambo ya kipuuzi na kuwa na wanawake wengine, namwambia achague. Na cha ajabu anachagua mwenzangu mie naendelea na maisha mengine. Lakini haiwezi kupita mwezi bila huyu jamaa kurudi na kuomba msamaha sana.

Nimechoka hali hii na ninahitaji sana kuendelea na maisha mengine wadau. Naombeni mnisaidie mawazo yenu labda wapi nakwama na nini nahitaji katika suala hili la mahusiano maana naona ule uvumilivu na upendo unakufa na chuki inaibuka moyoni mwangu juu ya huyu kaka. Nilidhani ni hali ya kawaida ila sasa nina siku ya tatu akinitafuta, sina uwezo wa kuongea naye vizuri. Kwa mara ya pili toka tuanze mahusiano nimemtukana na nimemruhusu aende anapotaka kwenda.

Ila bado analalamika kwa marafiki zake kuwa nimekuwa mjeuri.
Achana na huyu mpumbavu mara moja, wanaume tupo wengi, huyo siyo
 
Huyo jamaa ni muanga wa mapenzi wanaume tunapitia kipindi kigumu sana wakati wa ukuaji tunatukanwa na kuzalilishwa inatikia kipindi unasema sitakuja kumuamini mwanamke katika maisha yangu tena mara ghafla unapata kazi maisha yanakuendea vizuri sasa unakuja muda wa kisasi, ni ngumu sana kutulia na mwanamke au kuamini upendo wake wakati hapo kabla wanawake walikuwa wanakudharau , unajua kabisa huyu amefuata maisha hivyo unalipiza kisasi automatic.
 
Aliyekwambia tunaridhika na mbususu moja ni nani ?

Tunafanya kwa kujificha sababu tunawapenda ukiona huyo hajifichi hakupendi

We zunguka kote tabia zetu ni zilezile
 
Back
Top Bottom