Wanaume huwa mnaangalia nini mtafutapo mke?

Wanaume huwa mnaangalia nini mtafutapo mke?

mwanzo alimtaka mjanja na kumkataa mshamba kwa kuwa alikuwa bado mtoto,ajali ilivyompata akawa mtu mzima baada ya kuujua ulimwengu na kujifunza akahitaji tena binti makini mwenye uzuri wa tabia na roho,kitu ambacho wanaume wote wanaojitambua wanakitafuta kutoka kwa binti wa kuishi nae maishani
 
mwanzo alimtaka mjanja na kumkataa mshamba kwa kuwa alikuwa bado mtoto,ajali ilivyompata akawa mtu mzima baada ya kuujua ulimwengu na kujifunza akahitaji tena binti makini mwenye uzuri wa tabia na roho,kitu ambacho wanaume wote wanaojitambua wanakitafuta kutoka kwa binti wa kuishi nae maishani
"Mwanaume yeyote anayejitambua".
 
Habari wana JF,

Leo nimepewa story ambayo imenifurahisha na kunisikitisha kidogo.

Kuna jamaa alikuwa na mpenzi wake waliedumu kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa, baadae jamaa akaanza visa tu na kumuacha binti bila sababu za msingi.

Alikuwa akiulizwa na marafiki zake kwanini amemuacha yule binti wakati ni bonge la (wife material), jamaa alikuwa akisema eti binti ni mshamba mshamba yeye anahitaji binti mjanja, kweli akampata boonge la duu na akawa anajiona amefika haswa.

Baada ya muda jamaa alipata ajali mbaya iliyopelekea kuhitaji huduma hadi za kuogeshwa na ndugu zake walikuwa mbali, marafiki walimuhudumia japo sio kivile na wakati mwingine alipitisha hata siku tatu bila kuoga, (inshort) alihitaji huduma ya karibu sanaa.

Mpenzi wake mpya hakumjali na wala hakujishughulisha nae, yule binti wa kwanza alipopata habari kuwa jamaa anapata tabu sana alikwenda kumuona na kuamua kumhudumia vizuri sana hadi jamaa alipopata nafuu, na binti alijitolea kweli hata kifedha.

Jamaa sasa akili ndio zikamrudi na akamuomba binti msamaha na kumuomba warudiane, ila binti alikataa katakata na kumwambia kuwa amemuhudumia tu kama ambavyo angeweza kumhudumia binadamu yeyote aliyepatwa na shida ila hawezi kurudiana nae. Jamaa alijitahidi kila njia ila binti aligoma kurudiana nae.

Baada ya mwaka binti aliolewa na mwanaume mwingine. Na jamaa kabaki hadi sasa anahangaika tu na kulaani wanawake anasahau kuwa yeye pia aliwahi kuvurunda huko nyuma.

Hapo ndipo nikawaza "ama kweli wanaume hawajui nini wanataka kwakweli".
Tv
 
Back
Top Bottom