Wanaume huwa mnaangalia nini mtafutapo mke?

Wanaume huwa mnaangalia nini mtafutapo mke?

Kumkosoa kwa kwenda kinyume na kumkosoa kwa kumshusha maks ndy maana yangu kuu
Nneshataja sababu kuu ya kumshusha maks,lkn mazuri yake nayaona kbs.
Basi hongera mkuu.
 
Habari wana JF,

Leo nimepewa story ambayo imenifurahisha na kunisikitisha kidogo.

Kuna jamaa alikuwa na mpenzi wake waliedumu kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa, baadae jamaa akaanza visa tu na kumuacha binti bila sababu za msingi.

Alikuwa akiulizwa na marafiki zake kwanini amemuacha yule binti wakati ni bonge la (wife material), jamaa alikuwa akisema eti binti ni mshamba mshamba yeye anahitaji binti mjanja, kweli akampata boonge la duu na akawa anajiona amefika haswa.

Baada ya muda jamaa alipata ajali mbaya iliyopelekea kuhitaji huduma hadi za kuogeshwa na ndugu zake walikuwa mbali, marafiki walimuhudumia japo sio kivile na wakati mwingine alipitisha hata siku tatu bila kuoga, (inshort) alihitaji huduma ya karibu sanaa.

Mpenzi wake mpya hakumjali na wala hakujishughulisha nae, yule binti wa kwanza alipopata habari kuwa jamaa anapata tabu sana alikwenda kumuona na kuamua kumhudumia vizuri sana hadi jamaa alipopata nafuu, na binti alijitolea kweli hata kifedha.

Jamaa sasa akili ndio zikamrudi na akamuomba binti msamaha na kumuomba warudiane, ila binti alikataa katakata na kumwambia kuwa amemuhudumia tu kama ambavyo angeweza kumhudumia binadamu yeyote aliyepatwa na shida ila hawezi kurudiana nae. Jamaa alijitahidi kila njia ila binti aligoma kurudiana nae.

Baada ya mwaka binti aliolewa na mwanaume mwingine. Na jamaa kabaki hadi sasa anahangaika tu na kulaani wanawake anasahau kuwa yeye pia aliwahi kuvurunda huko nyuma.

Hapo ndipo nikawaza "ama kweli wanaume hawajui nini wanataka kwakweli".
Dah umeuliza swali la msingi sana, na kisa ulichokitoa kina mafundisho ndani yake kwa siye wanaume,

Kimsingi kwangu mimi kumchagua mke mwema wa kuoa naangalia vigezo vifuatavyo;

1) Mwanamke mwenye mapenzi ya kweli.
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke.

2) Mwanamke mwenye tabia nzuri.
Tabia njema ndiyo silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda.

3) Mwanamke mwenye uchu na maendeleo.
Hapa naongelea mwanamke anayejituma na kujishughulisha ktk masuala ya maendeleo,

4) Mwanamke mvumilivu.
Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha. Huu ndiyo wakati wa kuona uvumilivu mwanamke.

Naomba kuwasilisha hoja, japokuwa mtaniambia sifa hizo nilizozitaja hapo juu ni za Malaika.
[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
 
Mengi mno.Usafi wako,kujituma kazi,uwezo wa kutatua matatizo ya kawaida,historia ya ukoo na mengineyo.
 
Sometimes is very hard to find someone with all those attributes kwa pamoja.

Ila unaweza ukampata mwenye atleast hizo attributes kisha ukazijazia nyama.

Kuna tabia unaweza ukazi instal kwa mwanamke unazozitaka. Ni swala la muda na mhusika kuwa ready kubadilika.

28yrs muda bado upo. Ni swala la kutulia, na kutuliza akili huku ukimwomba Mungu.

Kila la kheri
Thank you mkuu, ila i come to know uzuri siku hizi tunaweza kudownload so naangalia sana kichwani.
 
Dah umeuliza swali la msingi sana, na kisa ulichokitoa kina mafundisho ndani yake kwa siye wanaume,

Kimsingi kwangu mimi kumchagua mke mwema wa kuoa naangalia vigezo vifuatavyo;

1) Mwanamke mwenye mapenzi ya kweli.
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke.

2) Mwanamke mwenye tabia nzuri.
Tabia njema ndiyo silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda.

3) Mwanamke mwenye uchu na maendeleo.
Hapa naongelea mwanamke anayejituma na kujishughulisha ktk masuala ya maendeleo,

4) Mwanamke mvumilivu.
Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha. Huu ndiyo wakati wa kuona uvumilivu mwanamke.

Naomba kuwasilisha hoja, japokuwa mtaniambia sifa hizo nilizozitaja hapo juu ni za Malaika.
[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
Hahahaaaa!! Hope nawe unastahili mwanamke wa aina hiyo.
 
Back
Top Bottom