Hivi ulishawahi kujiuliza kama mimi ninavyojiuliza! Kwa namna tunavyosoma vitabu vya dini na historia zake (dini zote), tunaaminishwa ya kuwa wanawake walikuwa wanavaa nguo za kuwafunika sana, yaani hata kuuona upaja hauwezi (ukiacha wale malaya waliokuwa wanaelezewa namna wanavyovaa na kusimama njia panda kujiuza, japo haielezewi wanavaa nusu uchi, ila manukato yao kwa sana), wenyewe waliwajua.
Sasa kwa utangulizi huo hapo juu, utapata picha ya kuwa, wanaume tumeumbwa kutamani kwanza na kupenda kunafuatia.
Sasa ninachojiuliza ni, pale Yesu, alipowaambia enzi hizo wafuasi na wengine wale '....... Bali yeyote amtazamaye mwanamke na kumtamani, ameshazini naye....' Mathayo 5:27-28
hebu oneni sasa namna gani kutamani kulivyo, yaani hata avae dela zito ama baibui zito, bado tu wanaume kutamani kunaanza kwanza, maana usipomuoa shepu, utamuona sura ama nywele, na ndiyo maana wanawake wameambiwa wajisitiri na hata nywele wasiziache wazi.
Hivi miaka ile kulikuwa na vimini kweli?! Hapo unapata picha pana, na ndiyo maana hadi leo vitabu vitakatifu vina nguvu bado.
Hivyo narudia tena, mkiamua kuoana, muangalie vipaumbele vyenu kwanza kabla hamjaingia kwenye taasisi hiyo.
Ahsante!