LadyAJ
JF-Expert Member
- Oct 21, 2015
- 7,173
- 9,656
Bahati mbaya au nzur wewe bwana Huijui ndoa unajilopokea tu kwa Kudhihaki upande wa wanawake ndoa ni zaidi ya mavazi/kujisitiri kwa mtu! Hakuna aliyezaliwa yuko timamu wengi hujifunza kutokana na mahitaji na mienendo ya watu wetu wa karibu na tunaowapenda, binafsi nililelewa kwa Uhuru wa kuvaa ila nilipompata mwenza wangu niligundua kuna vitu hapend nivae na alikuwa muwazi wa kunionyesha kwa vitendo, anakupeleka dukan kila ukichagua vazi lililokinyume na yeye anakataa analiponda kuwa hupendez, kwa kuwa mwanamke anataka kusifiwa na mumewe bila shaka siku hadi siku atakua anavaa vile ambavyo mpenziwe husema amependeza !! La muhimu usimuoe mwanamke mwenye tabia za hovyo japo anajisitiri mpaka ukucha! Usioe mwanamke mbishii,asiye mtii,mwenye kiburi visasi na chuki! Eti kisa ni mzuri au anavaa mavazi uliyoyaandika hapo
Ndoa ni zaidi ya unavyoona wewe, ukimpenda mtu mlete karibu chukua nafasi ya kum shape aendane na matakwa yako, mke au mume mzuri (mwema)hutengenezwa na sio hushushwa vile alivyo
Ndoa ni zaidi ya unavyoona wewe, ukimpenda mtu mlete karibu chukua nafasi ya kum shape aendane na matakwa yako, mke au mume mzuri (mwema)hutengenezwa na sio hushushwa vile alivyo