Polisi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,082
- 640
Wakuu, mdogo wangu amefikia makubaliano na mke wake wa ndoa kuwa wapeane talaka. Walifunga ndoa mwaka 2007 huko kigoma lakini baada ya mwezi mmoja tu mke wake aliomba arudi dar es salaam akaendelee na kazi yake kwa madai kuwa maisha ya mshahara mmoja yasingewezekana. Mume alikataa na kupelekea ugomvi wa kutisha huku mke akimwita mume ni mchawi, muuaji na amemwibia hela zake kwenye kabati. Mume akaridhia maana ndani mke akawa mtu wa kununa, hapiki hafui. Wakiwa mbalimbali ugomvi haukwisha, kila kukicha ktk cm ni kesi tu. Mume akienda dar kama alipanga kukaa wiki, anaishia siku tatu au mbili.. Kesi zao zimeongelewa sana kifamilia na kushindikana. Mwaka juzi disemba mke alikwenda kgm na ndani ya wiki moja ukazuka ugomvi wa kufa mtu. Ndipo majirani walipowakalisha na kuwaomba watengane wasije wakajeruhiana. Mwaka sasa umepita mke yuko dar na mdogo wangu kahamia mwanza kikazi. Wamefikia maamuzi wapeane talaka ili kila mmoja awe huru.
kinachotupa shida hapa wana ndugu ni nani aanze kufungua kesi. Mdogo wangu tayari amezaa na msichana mwingine na yuko confortable tu. Pili kama mdogo wangu ataamua kufungua kesi, afungulie wapi? Ndoa ilikofungwa (kigoma), anakoishi mke (dar) au anakoishi mdogo wangu (mza) na kwa utaratibu upi.
nimesoma thread karibu zote za talaka humu jf. Nimejifunza mengi ila utata umekuja kwa kuwa wanaishi mbalimbali mno.
nisaidieni nimsaidie dogo