Wanataka kuvunja ndoa; tuwasaidiaje?

Polisi

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,082
639
Wakuu, mdogo wangu amefikia makubaliano na mke wake wa ndoa kuwa wapeane talaka. Walifunga ndoa mwaka 2007 huko kigoma lakini baada ya mwezi mmoja tu mke wake aliomba arudi dar es salaam akaendelee na kazi yake kwa madai kuwa maisha ya mshahara mmoja yasingewezekana. Mume alikataa na kupelekea ugomvi wa kutisha huku mke akimwita mume ni mchawi, muuaji na amemwibia hela zake kwenye kabati. Mume akaridhia maana ndani mke akawa mtu wa kununa, hapiki hafui. Wakiwa mbalimbali ugomvi haukwisha, kila kukicha ktk cm ni kesi tu. Mume akienda dar kama alipanga kukaa wiki, anaishia siku tatu au mbili.. Kesi zao zimeongelewa sana kifamilia na kushindikana. Mwaka juzi disemba mke alikwenda kgm na ndani ya wiki moja ukazuka ugomvi wa kufa mtu. Ndipo majirani walipowakalisha na kuwaomba watengane wasije wakajeruhiana. Mwaka sasa umepita mke yuko dar na mdogo wangu kahamia mwanza kikazi. Wamefikia maamuzi wapeane talaka ili kila mmoja awe huru.

kinachotupa shida hapa wana ndugu ni nani aanze kufungua kesi. Mdogo wangu tayari amezaa na msichana mwingine na yuko confortable tu. Pili kama mdogo wangu ataamua kufungua kesi, afungulie wapi? Ndoa ilikofungwa (kigoma), anakoishi mke (dar) au anakoishi mdogo wangu (mza) na kwa utaratibu upi.

nimesoma thread karibu zote za talaka humu jf. Nimejifunza mengi ila utata umekuja kwa kuwa wanaishi mbalimbali mno.

nisaidieni nimsaidie dogo
 
suala la kufungua kesi za namna hiyo huwa linaanzia chini kwenye mabaraza kama mabaraza ya kata n.k, ila kama imefikia hatua ya kufungua kesi mahakamani nafikiri kitu cha kwanza kuzingatia ni eneo ambalo ndoa hiyo imefungwa ambapo kwa maelezo yako ni kigoma. Suala la pili la kufikiria mahali ambapo mmoja wenu anaishi .tatu nilazima uzingatie eneo ambalo litakuwa rahisi kati yenu kupatikana mara mtakapohitajika mahakamani. Kwa mawazo yangu kwa kuwa mpaka sasa mdogo wako amevunja agano/mkataba wa ndoa kwa kuoa/kuzaa na mke mwingine nje ya ndoa halali (japo hujatueleza ndoa hiyo ni ya aina gani) ila tuchukulie ni ya mke mmoja, naamini mahakama inaweza kuvunja ndoa hiyo, kitu cha msingi ni wewe kufungua kesi eneo ambalo mke wako wa ndoa ndiyo makazi yake ya kudumu, hata hivyo kabla hatua hizo hazijafikiwa nafikiri ni vema kujaribu kutafuta muafaka au kumjulisha mkewe kusudio la kuvunja ndoa hiyo kutokana na abc zilizofikia kama mkewe atakuwa radhi wanaweza kukubaliana sehemu ambayo kesi ifunguliwe. (haya ni mawazo yangu tafadhali usije ukayachukulia kama msimamo wa kisheria, aidha siungi mkono watu kuachana maana mungu hapendi kuachana)
 
pole sana kwa matatizo ya mdogo wako kama wao 2 wamekubaliana na wameridhia kabisa kuachana wanaweza kwenda kwa mwanasheria akawatengenezea hayo makubaliano yenu nafikiri kuna namna wanafanya then mnakwenda ustawi wa jamii kisha mahakamani kwa vile akuna mabisahano kati yenu wala madai kunakuwa akuna longo longo mahakama inavunja huo ni mtazamo wangu base to what i have hear bfore mkuu
 
Mtafute Mzee Butiku, yeye na mke wake waliondoka mgu kwa mguu mpaka Mahakamani kuomba talaka bila kupigiana kelele wala manung'uniko. Mahakama ilitoa talaka. Hawakwenda baraza la usuluhishi wala ustawi wa jamii. Wanasheria huwa wana-cite ndoa hiyo kwenye kesi wanazoendesha
 
eti nini mkuu yani akuna shoti kati mh inawezekana cunajua wenye nchi yao hawa
 
Mkuu nakushukuru sana
 
pole sana kwa matatizo ya mdogo wako kama wao 2 wamekubaliana na wameridhia kabisa kuachana wanaweza kwenda kwa mwanasheria akawatengenezea hayo makubaliano yenu nafikiri kuna namna wanafanya then mnakwenda ustawi wa jamii kisha mahakamani kwa vile akuna mabisahano kati yenu wala madai kunakuwa akuna longo longo mahakama inavunja huo ni mtazamo wangu base to what i have hear bfore mkuu

Asante sana mkuu
 
Mtafute Mzee Butiku, yeye na mke wake waliondoka mgu kwa mguu mpaka Mahakamani kuomba talaka bila kupigiana kelele wala manung'uniko. Mahakama ilitoa talaka. Hawakwenda baraza la usuluhishi wala ustawi wa jamii. Wanasheria huwa wana-cite ndoa hiyo kwenye kesi wanazoendesha

Butiku huyu wa nyerere foundation? sisi watu wa chini kuwaona hao ni ngumu sana amewaweza babu wa loliondo tu. Nashukuru kwa mchango wako
 
mbona suala ni dogo sana sa ka dogo keshapata mtu mwingine na wako safi tu tatizo liko wapy umetake trouble hadi ya kuleta habariyako huku jamvini kutusumbua tu hebu waambie wapelekane kwenye tribunals huko.
 
Siyo hivyo mkuu. Hata kama wao wamefikia uamuzi wa kuachana nadhani bado sheria zinatakiwa kufuatwa. Nilichotaka mimi ni JINSI YA KUFUATA SHERIA
 
Sasa wakishapata baraka za ustawi wa jamii na suala likaenda mahakamani itaendeshwa kesi kama kesi nyingine (yaani kuleta mashahidi, kesi kupigwa kalenda n,k) au ni mara moja tu inavunjwa?
 
Mkuu, mahakama ina base sana kwenye recommendations za baraza la usuluhishi la taifa ambayo hupokea recommendations kutoka ustawi wa jamii n.k. Kama kesi imepelekwa mahakamani ina maana usuluhishi umeshindikana. Mahakama haiwezi kuplay role ya kusuluhisha. Itachukua muda tu kama kutakuwa na ubishani katika matunzo na malezi ya watoto na mgawanyo wa mali. Hata hivyo ikidhibitika kuwa mdogo wako ameoa kabla hajampa talaka huyo mwingine, anaweza kutakiwa kulipa fidia kubwa tu kutegemea na kipato chake au kwenda jela akishindwa kulipa. Kwa sasa aendelee kumtunza huyo mke wake wa zamani kama kumlipia kodi ya nyumba, nguo n.k hadi hapo ndoa yao itakapotenguliwa. Huu ni uzoefu wangu based on hukumu nilizopata kuzisikia
 
hilo la fidia na jela sidhani kama ni applicable. Otherwise hii sheria ya ndoa itakuwa ipo upande wa wanawake tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom