Wanasubiri ukosee wakunase, usikubali kufeli

ShalomP

Member
Jun 14, 2019
97
154
Kuna baadhi ya watu wanaweza kuonesha wanakuunga mkono kwa nje katika juhudi zako kumbe ndani wanakuombea ufeli.

Unaweza ukawa unafanya Mambo mengi mazuri lakini ukipatwa na baya huinuka na kuanza kukuhukumu na kukukwaza kwa maneno badala ya kukuombea.

Unapofanya mema hawatasadiki ila watafanya juu chini wakuwekee mtego uteleze au ujikwae ili wapate sababu, Yaani wapo wanaokutumia kwa ajili ya kazi fulani kwa manufaa yao wakishamaliza kukutumia wanakutema na kukuona hufai.

Wanapokutema watahesabu mabaya yako mema yako watayafuta kuwa makini sio kila mtu ni wa kumweleza maono yako Bali wengine ni wanafiki.

Unaweza ukawa unakazana kumwomba Mungu ufanikiwe kumbe mwengine anakuombea ufeli. Wanatazama vibanzi kwenye macho ya wenzao wakati wao boriti hawajatoa machoni mwao.

Kuwa makini wanakuchekea machoni moyoni wanatafuta ulipokosea ili wakuhukumu, Wanasubiri ukosee Ili wakunase.

Unaweza ukamfanyia Mtu kazi iliyo njema Sana lakini siku utakopokosea atafuta mema yako yote atahesabu mabaya tu,Hata wale uliowaamini watainuka na kukushambulia kwa vyovyote vile.

Hapo ndipo utajua Nani rafiki,Nani mnafiki,au Nani msaliti au Nani akufaaye wakati wa dhiki. Unapopatwa na tatizo ndipo utajua Nani mnafiki au nani rafiki, Unayemuhukumu Kama sio Kweli umemsemea kwa uwongo hakika malipo ni hapa hapa.

Thibitisha ndipo ulopoke sio kumtungia mtu shutuma za kufikirika yaani unadhania tu.

Ni heri kuwa na marafiki wachache wanakujari wakati wa dhiki kuliko kundi la marafiki wengi wanafiki wanaokuombea ufeli.

Unapofanikiwa watainuka na kusaga meno kumbe Nia yao ni kukuona unafeli.Haina kufeli kimya ni jibu tosha.

73099101_483842489006583_5482948184852398080_n.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio waafrika tu...hata wazungu wanafanyiana ubaya.


Hujiulizi kwann Quotes tunazogugo nyingi ni zawazungu???....



Ila Waafrika, TUMEZIDI...MTU yupo radhi apoteee miezi 2--3 ..unaweza dhania kaenda tafuta maisha, kumbe kaenda tafuta Uchawi wakukulogezea Uanguke.
 
Hili jambo lilinisumbua kwa muda mrefu sana nilikuwa nawaamini watu kirahisi ma kuact nice kwao kuwasogeza kwenye maisha yangu lakini mwisho wa siku hakuna ambae nikagundua yupo upande wangu hata kimaombi au kunitakia mema,

yani unaweza ukamletea mtu habari za jambo lako kukwama kisha ukaona mood yake inavyo badilika yani kuna kijifuraha fulani anakipata kwa muda ule hata machoni pake unakiona ila atajibaraguza kuwa oooh pole pole kumbe ni bullshit kabisa

Kuna muda nikawa nawaza labda ni jamii niliyokuwa ninaishi nayo mimi ndio yenye hilo tatizo lakini hata nikihama sehemu moja kwenda nyingine bado nakutana na watu wa sifa hizo hizo.. nikawaza labda huenda ni jamii zetu za watu weusi ila kwa wazungu mambo yatakuwa vizuri ila sikupata jibu kwa sababu sijawahi kuishi na mzungu hata mmoja


Kitu muhimu nilicho jifunza na kinanisaidia kwa asilimia kibwa kwa sasa ni kuwa na privacy yaani nimekuwa msiri mpaka najiogopa mwenyewe na hiyo ndio dawa yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom