Wanasheria wetu! Tumaini jipya?

Wanasheria wetu! Tumaini jipya?

Mtani...hivi kweli unaona/unadhani hiyo kesi aliyoifungua bi Karume ina mashiko?

Na kweli ni kesi ya kuwakilishwa na mawakili 29?

Hata kesi ya karne [O.J. Simpson murder trial] O.J. hakuwakilishwa na mawakili 10....

Au ni kiki tu hizo?
Mtani,wapi nilipotaja kesi ya Wakili Msomi Fatma Amani Karume? Au unataka maoni yangu? Ni kwamba,mahakama iko kwa ajili ya kumaliza mabishano na kupata tafsiri ya sheria. Hivyo,yuko sawa kwa mujibu wake.
 
Call it what you want.

It's a stunt.
Mkuu povu la Kizungu... Stumt with positive effect.. Hatuwezi kukaa na Serikali isiyokubali kukosolewa... Sasa kule waadabishana kwa vifungu....

Kama mnataka kaeni juu ya hivyo vifungu mseme ni vya mwaka 1975 havitumiki 2017+
 
Mtani,wapi nilipotaja kesi ya Wakili Msomi Fatma Amani Karume? Au unataka maoni yangu? Ni kwamba,mahakama iko kwa ajili ya kumaliza mabishano na kupata tafsiri ya sheria. Hivyo,yuko sawa kwa mujibu wake.

Oh..naona hukunipata tu vizuri.

Wala sisemi kuwa umeitaja hiyo kesi.

Mimi nilikuwa nachomekea tu ili nipate maoni yako.

Na umeyatoa. Inatosha.
 
Mtani...hivi kweli unaona/unadhani hiyo kesi aliyoifungua bi Karume ina mashiko?

Na kweli ni kesi ya kuwakilishwa na mawakili 29?

Hata kesi ya karne [O.J. Simpson murder trial] O.J. hakuwakilishwa na mawakili 10....

Au ni kiki tu hizo?
Jiongeze, umeshaambiwa ni alama ya solidarity forever. Acha mahaba.
 
Kwa mfano TLS ikivunjwa halafu wanasheria wakaundiwa bodi kama vile makandarasi na wanataaluma wengine, bado kutakuwa na hizi mbwembwe zinazoendelea?. Hii solidarity itaendelea kuwepo?.
 
Jijibu mwenyewe. Umeuliza maswali mepesi,ya kitoto na ya kiutabiri. Wivu unakusumbua. Kama umeshindwa kuwa Mwanasheria,fanya ulichofanikiwa kukiweza.
 
Kwanini hilo lifanyike sasa? Tatizo nini? Woga!? Juu ya nini? Kunguru mwoga hukumbiza bawa lake mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jijibu mwenyewe. Umeuliza maswali mepesi,ya kitoto na ya kiutabiri. Wivu unakusumbua. Kama umeshindwa kuwa Mwanasheria,fanya ulichofanikiwa kukiweza.
Siwezi kujijibu kwa sababu mimi sio mwanasheria, na ni mtu ambaye ni mwepesi kuheshimu taaluma za watu.

Kuna spirit ya uanaharakati ndani ya majumuiko ya wanasheria, sasa spirit hii itaendelea kuwepo iwapo muundo wa umoja utabadilika huko mbeleni?.

Taaluma ya sheria moja kwa moja ni sehemu ya maadui wa watu fulani haswa wale wenye ushawishi kwenye jamii, hivyo wanasheria wapo vitani japo kisaikolojia. Wanajiandaaje ikiwa mamlaka zitaamua kubadilisha TLS kwa kuanzishwa kwa bodi ya wanasheria?.
 
Miaka ile ya 2000 wakati wa Gen P. Musharaf wa Pakistan, vyama vingine vyote vya siasa vikiwa vimebanwa mbavu na kuminywa hasa.... Likatokea jambo la nadra sana, sikumbuki vizuri ilikuwaje lakini nakumbuka wanasheria walichokonolewa wakachokozwa
Hawakukubali wakaandaa maandamo ya amani kuelekea Islamabad mji mkuu wa Pakistan, maandamano hayo yalitokea miji mingine mikuu kama Peshawar, Lahore na Karachi
Nakumbuka wiki ya maandalizi ya yale maandamano wanasheria walitishwa sana... Lakini wakashikilia msimamo wao wa kuandamana kwa amani.... Na hatimaye wakaandamana.......
Huku kwetu kuna kila dalili ya yale ya Pakistan kujirudia.... Ni wazi na sio siri vyama vya siasa vile vyenye nguvu vimebanwa kila kona na vinafanyiwa hujuma zisizoisha kila uchao, viongozi wanakatishwa tamaa kwa malundo ya kesi, hujuma ni nyingi mno na kesi pia ni nyingi.... Ni mkakati maalum uliosukwa kwa ufundi kudhoofisha na hatimaye kuua kabisa vyama makini vya upinzani
Lakini siku zote penye nia pana njia! Wote tunajua hofu waliyokuwa nayo watawala kwa Lisu kuchaguliwa kuwa rais wa chama cha wanasheria Tanganyika! Tulishuhudia vibweka vya kila aina.... Wanasheria wakagoma kuburuzwa, wakagoma kupangiwa wakagoma kupelekeshwa! Na kubwa kuliko yote wakagoma KUNUNULIWA.....
Mshikamano wao wakati ule wa uchaguzi likikuwa jambo geni, wengi walidhani baada ya pale wataachana njiapanda.... HAWAKUFANYA HIVYO..... kauli yao imekuwa SOLIDARITY FOREVER!
Mambo ya nadra yameendelea kutokea kwenye kaliba hii ya wasomi wanataaluma mahiri.... Tumeshuhudia kwenye kesi ya Lisu, tumeshuhudia kwenye kesi ya mwanamama machachari Bi Fatma Karume.... kuna bonding ya aina yake kwa hii kaliba ya sheria... Mamlaka hazipedi kabisa hili jambo lakini pengine ndio ule wakati umetimia sasa..... A long way to freedom

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao ni Wana UKAWA sio wanasheria
 
Mh! Mkuu una kumbukumbu nzuri sana. Hili la Wanasheria kuwa na mshikamano wa hali ya juu kule Pakistan nalikumbuka sana na pia nilikuwa nalifuatilia kwa karibu mno. Pia nilikuwa upande wa wanasheria na kutaka sana waandamane kupinga kilichokuwa kinachoendelea nchini mwao UDIKTETA UCHWARA kama hiki kinachoendelea nchini mwetu tangu bwana yule ashike utamu. Katika hili sakata hili hapa nchini kwetu kwa mara nyingine tena niko upande wa Wanasheria! Najua kutakuwepo na wasaliti wachache lakini kama 80% kwenda juu ya wanasheria nchini wakiamua kushikamana basi hawa wanaweza kabisa kumsimamisha huyu dikteta uchwara, lakini dalili zimeshaanza kujionyesha jinsi hii Serikali dhalimu inavyopanga mkakati wa kuwabana mbavu wanasheria nchini.

Naamini kabisa hawa wanasheria nchini mwetu wakiamua kuwa kitu kimoja na kuonyesha mshikamano wa hali ya juu kupinga katiba ya nchi kudharauliwa, kupinga sheria za nchi kudharauliwa na haki ya raia kujieleza kuminywa, haki ya vyama vya upinzani kufanya shughuli zao nchi nzima bila ya kuingiliwa na yeyote yule kuminywa, Bunge kudharauliwa na hivyo pesa za walipa kodi kuchotwa kienyeji tu bila idhini ya Bunge na kuwa kama vile mtu anatia mkono kwenye mfuko wa suruali na kuchukua kiasi akitakacho kufanyia lolote lile liwe na maslahi au la kwa Tanzania na Watanzania yeye hajali.

Kwa maoni yangu mshikamano wa hawa wanasheria ndiyo utaweza kumsimamisha huyu dikteta uchwara pale watakapotamka ENOUGH IS ENOUGH (We're not going to tolerate this non sense anymore) hawa nao wakishikwa na hofu na kuamua kunyamaza kimya kama vile wanavyofanya wastaafu wa nchii waliowahi kushika nyadhifa za juu with exception of few, viongozi wa dini etc basi nchi yetu itakuwa haikaliki na haitatamanika tena kwa udikteta uchwara utakavyozidi kuimarika na hivyo kuminya haki zote za Watanzania.

[HASHTAG]#solidarityforever[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Togetherweshallovercome[/HASHTAG]

Miaka ile ya 2000 wakati wa Gen P. Musharaf wa Pakistan, vyama vingine vyote vya siasa vikiwa vimebanwa mbavu na kuminywa hasa.... Likatokea jambo la nadra sana, sikumbuki vizuri ilikuwaje lakini nakumbuka wanasheria walichokonolewa wakachokozwa
Hawakukubali wakaandaa maandamo ya amani kuelekea Islamabad mji mkuu wa Pakistan, maandamano hayo yalitokea miji mingine mikuu kama Peshawar, Lahore na Karachi
Nakumbuka wiki ya maandalizi ya yale maandamano wanasheria walitishwa sana... Lakini wakashikilia msimamo wao wa kuandamana kwa amani.... Na hatimaye wakaandamana.......
Huku kwetu kuna kila dalili ya yale ya Pakistan kujirudia.... Ni wazi na sio siri vyama vya siasa vile vyenye nguvu vimebanwa kila kona na vinafanyiwa hujuma zisizoisha kila uchao, viongozi wanakatishwa tamaa kwa malundo ya kesi, hujuma ni nyingi mno na kesi pia ni nyingi.... Ni mkakati maalum uliosukwa kwa ufundi kudhoofisha na hatimaye kuua kabisa vyama makini vya upinzani
Lakini siku zote penye nia pana njia! Wote tunajua hofu waliyokuwa nayo watawala kwa Lisu kuchaguliwa kuwa rais wa chama cha wanasheria Tanganyika! Tulishuhudia vibweka vya kila aina.... Wanasheria wakagoma kuburuzwa, wakagoma kupangiwa wakagoma kupelekeshwa! Na kubwa kuliko yote wakagoma KUNUNULIWA.....
Mshikamano wao wakati ule wa uchaguzi likikuwa jambo geni, wengi walidhani baada ya pale wataachana njiapanda.... HAWAKUFANYA HIVYO..... kauli yao imekuwa SOLIDARITY FOREVER!
Mambo ya nadra yameendelea kutokea kwenye kaliba hii ya wasomi wanataaluma mahiri.... Tumeshuhudia kwenye kesi ya Lisu, tumeshuhudia kwenye kesi ya mwanamama machachari Bi Fatma Karume.... kuna bonding ya aina yake kwa hii kaliba ya sheria... Mamlaka hazipedi kabisa hili jambo lakini pengine ndio ule wakati umetimia sasa..... A long way to freedom

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani sasa nyie ambao hamko pamoja na wale wasaliti muanze kuvaa zile fulana za UKUTA kama Kamanda Lissu. By the way kuna mtu humu anafahamu zile fulana za UKUTA zinapatikana wapi? Mtaani zinauliziwa sana ingawaje inawezekana kabisa ukivaa utaitwa MCHOCHEZI na kubambikiwa kesi.

Asante kwa kutukubali. Fahamu kuwa tasnia yetu hairandani na porojo,utapeli na propaganda. Ni mambo ya kifungu kwa kifungu;hoja kwa hoja. Mambo yako mahakamani mkuu!
 
Mtani...hivi kweli unaona/unadhani hiyo kesi aliyoifungua bi Karume ina mashiko?

Na kweli ni kesi ya kuwakilishwa na mawakili 29?

Hata kesi ya karne [O.J. Simpson murder trial] O.J. hakuwakilishwa na mawakili 10....

Au ni kiki tu hizo?
Hapa issue si ukubwa wa kesi au aina ya kesi, it's significance of the case
 
Mtani...hivi kweli unaona/unadhani hiyo kesi aliyoifungua bi Karume ina mashiko?

Na kweli ni kesi ya kuwakilishwa na mawakili 29?

Hata kesi ya karne [O.J. Simpson murder trial] O.J. hakuwakilishwa na mawakili 10....

Au ni kiki tu hizo?

the story of o.j simpson
ila ile dream team ya kina r.shapiro ni balaa
 
Back
Top Bottom