Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Mh. Spika alisema hawatafanya kazi na Prof. Assad ila si ofisi ya CAG. Akaongeza kuwa kama ripoti itakuwa na saini ya Assad hawataipokea (lakini leo imepokelewa ikiwa na saini hiyo). Wanasheria mlio humu naomba ufafanuzi juu ya hili-Kukiuka azimio lililopitishwa.
Kwa hili lililotokea leo linatukumbusha kutafakari hoja zifuatazo:
-Ni nini wajibu wa mwanasheria mkuu wa serikali katika kutafsiri katiba na sheria pale zinapoleta mkanganyiko?
-Ni nini wajibu wa kila mbunge? Je, akubali kufuata yote yanayosemwa na kiti cha spika?
-Je, wale walioadhibiwa kwa kumuunga mkono Assadi, adhabu zao zitatenguliwa?
TUJIANDAE KUPATA TUKIO JIPYA LA KUPOZA MOTO HUU UNAOFUKUTA!