Wanasheria mtusaidie, Spika anaposhindwa kusimamia Azimio lililopitishwa na Bunge, nini kitatokea?

Azimio Batili na ufafanuzi batili, usipotekelezwa, hakuna kosa lolote kikatiba kwa sababu katiba imefuatwa. Lingetekelezwa ndipo kungetokea matatizo ikiwemo kuvunjwa kwa Bunge.
P

Bunge kutoa azimio kama hilo kwa mtu kama CAG unaitaje ni azimio batili? hakuna kosa KIVIPI kwa mhimili mkubwa kama huo kutoa azimio kubwa kwa mhimili mwingine na kisha kushindwa kusimamia azimio hilo?
 
Hii ni "kula matapishi" na kwa mtu timamu,msomi mwenye misimamo,asiyeng'ang'ania vyeo ingempasa ajiuzulu cheo chake maana anathibitisha UDHAIFU wake hadharani!!
Pili ametumia vibaya muda na pesa za walipakodi kuruhusu mjadala wakijinga ambao haujaweza kutekelezwa,Tabia ya kutumia vibaya rasilimali za serikali ni tabia mbaya!! mamilioni yamepotea kukutibu alafu unapoteza tena kwa mjadala feki kwenye jumba la serikali,wangeenda kujadilia makao makuu ya chama chao.
 
Wale wameonewa na tulishasema hiyo kamati ya maadili ipo kwa ajili ya kufanya hujuma na kutisha watu,wala haipo kutenda haki.
Sasa nini kitafanyika kwa hawa wabunge wawili, Mdee na Lema. Mimi naona ni busara wabunge kwa pamoja waseme jambo juu ya hao waliopewa adhabu kwa msimamo wao juu ya CAG.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bunge kutoa azimio kama hilo kwa mtu kama CAG unaitaje ni azimio batili? hakuna kosa KIVIPI kwa mhimili mkubwa kama huo kutoa azimio kubwa kwa mhimili mwingine na kisha kushindwa kusimamia azimio hilo?
Binafsi sijakuelewa, labda wengine watakuelewa. Nadhani hujui Kiswahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani huwa wanaifanyia Kazi Miaka uliyopita?

Chanzo Cha Mgogoro huu Ni kutofanyia Kazi Na wasipofanyia Kazi Tena Assad anasema atawaita Tena dhaifu
Umeona eeeehh... Hawa wabunge wa CCM kazi kubwa ni kugonga meza na kelele za ndiyooooooo, bila kuhusisha bongo zao ndiyo maana report huwa hazifanyiwi kazi. Kama mbunge kazi yake ni kusimama na kuitetea serikali badala ya kuihoji na kuisimamia, unategemea serikali itatekeleza kweli. Fuatilia vizuri wabunge wa CCM utaona kazi kubwa ni kusimama upande wa serikali eti kwa sababu ni serikali ya CCM. Wabunge wa CCM ndo wametufikisha hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu katika sheria kinaitwa VOID AB INITIO, Maana yake sheria inachukulia jambo lolote lililotekelezwa kwa ubatili na uharamu kuwa halina nguvu kisheria, halipo na halikuwahi kuwapo, ni la kupuuzwa.

Azimio la Bunge juu ya CAG lilikuwa VOID AB INITIO.
Halitambuliki. Walikuwa wanacheza iyena iyena tu in a silly session.

Sana sana wanachoweza kufanya ni kumdharau huyo aliwalisha matango pori kama kiongozi wa hovyo.
 
Kwa Matiki hiyo hata wale walio pewa adhabu kutokana na kadhia hiyo adhabu zao ni batili.
 
Kwani huwa wanaifanyia Kazi Miaka uliyopita?

Chanzo Cha Mgogoro huu Ni kutofanyia Kazi Na wasipofanyia Kazi Tena Assad anasema atawaita Tena dhaifu
Oh, kweli Mkuu,
Nilimaanisha kukaa na kuijadili.

By the way unafikiri kwanin Bunge hili linaloongozwa na kutawaliwa na CCM hua haliifanyiagi kazi hizi report miaka yote hii?? Nini sababu hasa?
 
wabunge wa CCM hawatumii akili wala busara na cha ajabu wengi wana degree zao au ndio elimu yetu ya kukariri? Ma Pro na Ma Dr wakiwa vyuoni wanaiponda sana serikali lakini wakipewa vyeo wanakua wajinga kabisa utadhani sio wao
 
CC Dkt Bashiru
 
Back
Top Bottom