Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,441
2,000
Wanabodi

Leo naendelea tena na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", Jee Azimio la Bunge kutofanya kazi na CAG Prof. Mussa Assad, ni uamuzi halali au batili?, na jee una maslahi gani kwa Taifa?, jee una maana gani kwa Bunge lenyewe, kwa Rais wa JMT, kwa Ofisi ya CAG na kwa Watanzania kwa jumla?, nini kitatokea iwapo Bunge litaamua kuutekeleza uamuzi huo. licha ya ubatili wa uamuzi huo nitakao uainisha humu, karibu uandamane nami.

Huu ni uzi wa mfululizo wa makala elimishi kuhusu Katiba ya Tanzania. Japo Katiba ni kakitabu kadogo tuu ka kurasa 112, na kameandikwa kwa lugha mbili za Kiswahili na Kiingereza, lakini kukasoma na kukaelewa, kunataka kiwango fulani cha uelewa, na Katiba halisi yenye usahihi ni ile ya Kiingereza, ile ya Kiswahili ina makosa madogo madogo mengi, sasa kwa vile baadhi ya viongozi wetu, inasemekana lugha ya Kiingereza ni tatizo, na waheshimiwa Wabunge wetu baadhi ni darasa la saba, na wengine ni form 4, 6, hadi Ph.D lakini kwa baadhi yao, maneno yao wanayosema na matendo yao wanayofanya, hata hao wa darasa la saba wana afadhali, na ndio maana wamekasirika kuambiwa ukweli wa udhaifu wao, na kuleta Kamusi, halafu wanakuja na Azimio la kiajabu ajabu ambalo hawana uwezo huo.

Kitendawili cha Azimio hilo batili la Bunge kutofanya kazi na CAG Prof. Mussa Assad, kitatenguliwa rasmi ndani ya siku 7 zijazo. Aliyepanga kitendawili hicho lazima kitenguliwe ndani ya siku 7 zijazo sio mimi, Paskali, bali ndivyo Katiba ya JMT ya mwaka 1977 inavyoelekeza, ambapo ime weka siku za Ripoti ya CAG kukabidhiwa Bungeni, imesema ripoti hiyo ifike mezani kwa Spika ndani ya siku 7, and numbers don't lie, kitendo cha Katiba ku prescribe siku za ripoti hiyo kukabidhiwa Bungeni ni ili kumzuia rais asije kuikalia ripoti hiyo hata iwe ni adverse vipi, ripoti ikiishakabidhiwa kwa rais, lazima itinge Bungeni, ndani ya siku zilizopangwa, tena ripoti hiyo inatakiwa kukabidhiwa hivyo hivyo ilivyo na sahihi ya CAG.
 1. Utangulizi. Tangu nimejiunga JF, sijawahi hata siku moja kujivunia elimu yangu, lakini unapochambua mambo makubwa na mazito kuhusu mustakabali wa taifa letu, sio vibaya ukiweka kaji bios kadogo tuu ili kutoa authority ya unachokijadili, kuonyesha hayo unayoyasema unatumia mamlaka fulani ya kupikwa na wapishi bingwa ukaiva.
 2. Hoja ya bandiko hili ni hoja ya kikatiba, na sio hoja ya kisiasa, Azimio la Bunge kutofanya kazi na CAG ni Azimio la kisiasa na sio la kikatiba, sio la kisheria, sio la kikanuni wala la kiutaratibu, kwa sababu uwepo wa ofisi ya CAG ni takwa la kikatiba, Bunge kufanya kazi na CAG ni takwa la Kikatiba na sio kwa utashi wa mtu hivyo, Bunge halina uwezo wa kupitisha Azimio linalokwenda kinyume cha Katiba, hivyo Azimio hilo Bunge, ni Azimio batili na kauli ya jana ya Mhe. Spika kuwa watafanya kazi na ofisi ya CAG lakini sio CAG Prof Mussa Assad, nayo ni kauli tuu ya kisiasa ili kujifurahisha, Kama ulivyo ubatili wa azimio kwa sababu, huwezi kuitenganisha ofisi ya CAG na CAG mwenyewe Prof. Mussa Assad.
 3. Kwa mara ya kwanza humu JF naomba kujivunia kuwa mimi Pascal Mayalla, ni mmoja wa wanafunzi wahitimu wa Sheria LL.B wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM aliyehitimu mwaka 2007, japo kiwango changu ni just a PASS tuu, lakini Shahada yangu ni "With Honours" na somo pekee ambalo nilipata alama za juu za A+ ni somo la LW 100: Constitutional Law, lililokuwa likifundishwana Prof. Issa Shiviji, hivyo hapa naomba mnione kama mnapata dose ya katiba kutoka kwa kaji Shivji fulani kadogo
 4. Tena mwaka wetu wa kwanza, kipindi chetu cha kwanza kilikuwa LW 101 tukifundishwa na ka teacher fulani hivi, kasichana karefu, kembamba, cheusi rangi ya chocolate chenye kasura cha baby face, wakati huo kakionekana kama kanaogopa ogopa, na kwa umbo na wembamba wake, kalionekana kama tunafundishwa na katoto cha sekondari form six kanafundisha Chuo Kikuu!, sasa sisi wengine tuliosoma ukubwani, tunasoma na mengi, sasa inapotokea unakutana na vialimu vitoto vitoto, basi akili yako inakuhama kabisa, nilikuwa silielewi kabisa somo lake, mwalimu akiingia kufundisha wewe macho yako ni kwa mwalimu tuu kumwangalia badala ya ku concentrate na anachofundisha. Naomba nisilitaje jina la hako kaalimu ka wakati huo maana kwa sasa... hayo tuyaache,
 5. Lakini kitendo cha kufundishwa na waalimu manguli wa sheria kama Prof. Shivji, Dr. Kabudi, Prof. Mgongo Fimbo, Prof. Kanywani, Prof. Luoga, etc na kupata A+ somo la Shivji is not a joke, nina haki kabisa ya kujitamba nami ni kaji bingwa kadogo ka Katiba kwa humu jf kama Shivji na Kabudi, walivyo mabingwa kitaifa na kimataifa.
 6. Hivyo ninavyoandika hapa, usikute hata Bunge wenyewe bado hawajua kuwa kukataa kupokea Ripoti ya CAG katika muda uliopangwa na Katiba utasababishwa Bunge livunjwe na pia usikute hata rais Magufuli mwenyewe saa hizi yuko busy akichapa kazi ziarani Mtwara kuwapooza Chingas na maumivu ya Korosho, hivyo hata na yeye hajui kuwa atapaswa kulivunja Bunge hili ndani ya siku 7 zijazo, iwapo litakataa kuipokea ripoti ya CAG, kufuatia Azimio lao batili la kutofanya kazi na CAG Prof. Mussa Assad.
 7. Watunga Katiba kuna kitu walidhaniria ndio maana kuitaka ripoti hiyo ikabidhiwe Bungeni ndani ya siku 7, na haimpi rais optios za kuchagua ama aikabidhi ama asiikabidhi, the option ni either aipeleke yeye au CAG aibimbirishe mwenyewe.
 8. Katiba imeeleze rais akiishapokea Ripoti ya CAG, anatakiwa kuifikisha Bungeni ndani ya siku 7 zijazo na asipokabidhi, then CAG ataikabidhi. Zikipita siku 7, Ripoti ya CAG haijafika mezani kwa Spika, kesho yake Bunge linapaswa kuvunjwa. Ingekuwa kikao cha Bunge kimeanza wiki iliyopita, siku ya leo ndio ingekuwa siku ya mwisho ya kukabidhiwa kwa Ripoti ya CAG Bungeni kwa mujibu wa katiba, ripoti hiyo inatakiwa iwe imekabidhiwa Bungeni ndani ya siku 7 za kikao cha Bunge, baada ya kukabidhiwa kwa rais. Ripoti ya CAG ilikabidhiwa kwa rais Machi 28, 2019, hivyo siku ya 7 ni leo tarehe 5, Mwezi April. Lakini kwa vile Bunge limeanza vikao vyake siku ya Jumanne tarehe 2 April, siku ya 7 ni Jumanne ijayo Tarehe 9, au wakitumia siku 7 za kibenki, yaani working days, then siku saba ni siku ya Alhamisi ijayo tarehe 11 April, 2019, Ripoti ya CAG ni Bungeni Dodoma.
 9. Bunge lisipoipokea, ripoti hiyo, then siku ya Ijumaa Ijayo Tarehe 12 ya Mwezi huu wa April, 2019, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais wa JMT atatakiwa kulivunja rasmi Bunge kwa mujibu wa Katiba
 10. Katiba pia imeeleza, kama rais asipoikabidhi ripoti hiyo ndani ya siku hizo 7, then CAG mwenyewe anaikabidhi Bungeni, na Bunge halikupewa option ya kuchagua ama kuipokea ama kuikataa, Ripoti ya CAG ikiishafika Bungeni ni lazima ipokelewe mezani hivyo kugeuka kuwa a public document.
 11. Bunge lina uhuru wa kuijadili, au kuipuuzia na kuithibitishia dunia ule udhaifu wao, lakini sio kuamua kuipokea au kutokuipokea, Ripoti ya CAG kupokelewa Bungeni ni jambo lazima Kikatiba, hivyo lile Azimio la Bunge ni batili na tangazo la jana la Spika kuwa Bunge litaipokea Ripoti ya CAG, kama itasainiwa na mtu mwingine pia ni batili.
 12. Ripoti ya CAG inasainiwa na CAG mwenyewe, hoja ya Bunge kuwa kama itasainiwa na mtu mwingine asiye CAG, ndio itapokelewa ni hoja muflis . Ripoti ya CAG lazima iwe na saini ya CAG mwenyewe Prof. Mussa Assad, na sio mtu mwingine yeyote.
 13. Hoja kuwa Bunge halitaipokea Ripoti hiyo kwa sababu limepitisha azimio la kutofana kazi na CAG Prof. Assad, kumbe masikini Bunge letu na Wabunge wetu, hawakujua kuwa wamepitisha azimio batili, hawana uwezo wa huo waliodhani wanao, wa kuamua wafanye kazi na nani, wasipoipokea Ripoti ya CAG Prof. Assad, rais anatakiwa kulivunja Bunge mara moja bila kuchelewa.
 14. Siku zote Ripoti ya CAG huwa unapokelewa Ikulu kwa mbwembwe na picha na taarifa toka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, huku jioni kwenye luninga na kesho yake kwenye magazeti, hii ikiwa ndio habari kuu, lakini Ripoti ya mwaka huu imepokelewa kimya kimya.
 15. Kwa uzoefu wangu wa miaka 29 katika tasnia ya habari, najua picha zilipigwa na video zipo, ila ikaamuliwa iwe kimya kimya, hivyo by connecting the dots, kumbe ukimya huu ulikuwa na sababu.
 16. This is my thinking aloud kuwa Nyumba kubwa was tipped, uamuzi wa Bunge kuhusu CAG kabla haijatangazwa Bungeni, hivyo CAG asipokabidhi ripoti yake wakamlia kobitz tuu, halafu watu tukiwaambia humu kuna watu mahali huwa wanajipendekeza mahali, hamuamini, sana sana tutaitwa kuhojiwa, lakini matokeo ya kujipendekeza huko, sasa yanaonekana wazi, Nyumba kubwa ikapokea ripoti kimya kimya, wakijua huo ndio mwisho wa ripoti hiyo, kumbe kesho yake mwenyewe mwenye ripoti yake akaweka wazi kuwa ameisha kabidhi ripoti kwenyewe kunako.
 17. Usikute wenzetu wale wameisoma Ibara ya 143 (4)ya Katiba tuu ya Kiswahili ambayo imeishia kusema maneo haya " (4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hiyo "Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge". Kwenye katiba hiyo ya Kiswahili, iliishia hapo bila kusema nini kitatokea kama rais hataiwasilisha Ripoti hiyo Bungeni, ndio maana wakaipokea kimya kimya, na Bunge likatoa Azimio batili hata baada ya kusikia kuwa Ripoti ya CAG imeisha wasilishwa Ikulu kwa rais na kupokelewa.
 18. Lakini Kama Wabunge wetu makini, na Bunge letu Tukufu makini, wangeisoma Katiba ya Kiingereza, yenye kueleza nini nini kitafanyika Iwapo rais hataiwasilisha Ripoti ya CAG Bungeni ndani ya Siku 7, then Bunge letu lisingepitisha Azimio bandia, wala jana Spika asingetoa taarifa kuwa Bunge halitapokea Ripoti yenye saini ya CAG Prof. Mussa Assad, Kifungu hicho kwa Katiba ya Kiingereza kinasema "If the President does not take steps of submitting such report to the National Assembly, then the Controller and Auditor-General shall submit the report to the Speaker of the National Assembly"
 19. Katiba yetu kuna vitu imempa rais discretion powers ya kuamua ama kutoamua, na vifungu vinamuelekeza rais kutekeleza kwa lazima na sio kwa utashi wake.Mfanoini death warrant, rais yuko huru kusaini hukumu ya kifo na wahalifu kunyongwa mpaka kufa au kutosaini, lna wakaendelea kuishi,
 20. Lakini katika kupokea ripoti ya CAG, rais hana uhuru wa kutoipokea na akiisha ipokea hana uhuru wa kuikalia, ndio maana amepewa siku 7. Asipoikabidhi then CAG mwenyewe anaikabidhi na inakuwa a public document, sasa Bunge lijadili au lisijadili, hayo sasa ni ya Bunge siyo ya CAG, CAG anakuwa ameisha timiza wajibu wake
 21. Pia kaika uteuzi, rais yuko huru kumteua mtu yoyote katika nafasi yoyote, kwa sifa zozote au bila sifa zozote, kwa sababu zozote au bila sababu zozote, na rais anaweza kutengua uteuzi huo wakati wowote kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote. Lakini kwenye uteuzi wa baadhi ya nafasi nyeti za kiutendaji, katiba imeweka sifa na vigezo wa uteuzi wa baadhi ya nafasi, na miongoni mwa nafasi hizo, ziko nafasi ambazo ni za kikatiba yaani maofisa waliolezwa ndani ya katiba sifa zao na vigezo vyao ambapo katika nafasi fulani, rais anatakiwa kumteua mtu mwenye sifa fulani, na uwezo wa rais ni kumteua tuu na sio kumtengua anapojisikia, watu hawa ni pamoja na Jaji Mkuu, Majaji, GAG, na Gavana wa BOT, watu hawa wana kinga ya kikatiba inaitwa security of tenure, rais anaweza kuwateua tuu, lakini hawezi kuwatengua. Sii wengi wanaojua kuwa CAG ana hadhi kama ya Jaji Mkuu, kitendo cha siku ile anafika Bungeni kuhojiwa na Kamati alipitishwa kusachiwa ni udhalilishaji mkubwa wa hadhi ya CAG.
 22. Japo rais hawezi kutengua uteuzi wa CAG, lakini CAG akifanya makosa ya kustahili kuondolewa anaondolewa, au akifanya makosa kustahili kushitakiwa anashitakiwa, ila kiukweli kabisa kuusema ukweli kuhusu Bunge sii kosa.
 23. Ripoti ya CAG ili iwe ni Ripoti ya CAG kweli ni lazima isainiwe na CAG mwenyewe, hiyo ripoti Spika aliyoizungumza isainiwe na mtu mwingine asiye CAG, then sio ripoti ya CAG.
 24. Kosa la CAG, Prof Mussa Assad, ni kusema ukweli kuhusu Bunge limeonyesha udhaifu, sio kosa la kupelekea kutenguliwa kwa CAG kwa sababu huo ndio ukweli bayana kuhusu Bunge hili hata kama wenyewe hawaupendi ukweli huu uwekwe bayana, hata kama wanakasirika na kumuita kila anayeusema ukweli huu lakini ukweli siku zote unabaki kuwa ukweli.
 25. Hivyo bandiko hili litawasaidia wanasheria wetu wa Bunge kuwafungua macho kuwa pamoja na kupitisha azimio lao batili, ripoti ya CAG yenye sahihi ya Prof. Assad, lazima ipokelewe vinginevyo Bunge linavunjwa.
 26. Ripoti ya CAG inaitwa tuu jina la Ripoti ya CAG kwa sababu inatayarishwa na CAG na kusainiwa na CAG, ripoti hiyo ni lazima iwasilishwe kwanza kwa rais, ila kuipa mamlaka ya kirais
 27. Hivyo Ripoti ya CAG, ikiishakabidhiwa kwa rais, inakuwa ime change hands za kimamlaka, sasa inagueka kuwa ni ripoti ya rais, inayoitwa kwa jina tuu la Ripoti ya CAG.
 28. Kule Bungeni ripoti hiyo inapoingia, inaingia kama Ripoti ya Ukaguzi iliyotoka kwa rais wa JMT kwa jina tuu la Ripoti ya CAG, kazi ya Bunge ni kuipokea tuu na kuiwasilisha mezani.
 29. Bunge halina mamlaka ya kumuingilia rais Ripoti yake ya CAG isainiwe na nani, wala halina mamlaka ya kutoipokea ripoti ya CAG kwa sababu hii ni ripoti ya rais, hivyo Bunge lisipopokea ripoti hii, rais kwa kutumia mamlaka ya Ibara ya 90 kifungu (c), rais anapaswa kulivunja Bunge.
 30. Hivyo kama Tanzania tutafuata utawala wa Katiba, Bunge liko chini ya Katiba, linaelekezwa na katiba linaweza kufanya nini na haliwezi kufanya nini, kwa mujibu wa vifungu nilivyowakea hapo, Bunge halina mamlaka ya kukataa kuipokea Ripoti ya CAG, wala Spika hana mamlaka ya kumuamuru rais Ripoti ya rais kwa jina la Ripoti ya CAG, isainiwe na nani, kazi ya CAG ni kufanya tuu ukaguzi, kutoa ripoti, kuisaini na kuikabidhi kwa rais, baada ya kuikabidhi ripoti hiyo kwa rais, kazi yake imekwisha, lakini iwapo rais hataikabidhi Bungeni ndani ya siku 7, kazi ya CAG inaendelea, kwa CAG kuichukua Ripoti hiyo na Kuikabidhi kwa Spika, na kazi ya Bunge ni kuipokea na kuiwasilisha Mezani.
 31. Bunge halina mamlaka wala jeuri ya kuikataa ripoti rais wa JMT kwa jina la Ripoti ya CAG et sijui mpaka isainiwe na nani, hivyo ndani ya siku 7 hizi ni lazima Bunge letu liipokee Ripoti ya CAG iliyosainiwa na CAG, Prof. Mussa Assad na hili halina mjadala, wasipofanya hivyo, ni Ijumaa ijayo itampasa rais kulivunja Bunge.
 32. Kama Rais wa JMT ataamua kufuata katiba, rais baada ya kuipokea Ripoti ya CAG, haombwi kuiwasilisha Bungeni bali anaelekezwa, kwa vile Katiba yetu inamheshimu sana rais na haimlazimishi kufanya jambo lolote. imempa fursa na muda wa kutosha wa kukaa na ripoti hiyo kuitafakari, Kisha aamue aiwasilishe au asiiwasilishe, kule kuipokea kimya kimya ni dalili tuu ya awali, hivyo ili kumzuia rais wetu asiwe mnyonge kuwasilisha Bungeni kutokana na kuwa bize na mambo muhimu zaidi, then CAG ameelekezwa ataiwasilisha yeye Bungeni.
 33. Hivyo hadi kufikia Jumatano Ijayo Saa 9:30 jioni muda wa mwisho wa kazi kiserikali, ripoti hiyo haojatua Bungeni, then Alhamisi Saa 3:00 asubuhi, CAG Prof. Mussa Assad atatinga ofisi za Bunge Dodoma na Ripoti yake mkononi na kufuatia hizi figisu figisu za Bunge, hadi ile dispatch book hata beba mesenja, bali atabeba CAG mwenyewe, na mtu wa kupokea ni Spika mwenyewe au Naibu wa Spika, ndio watasaini dispatch book ya CAG ili wasipoiwasilisha mezani siku hiyo hiyo, kesho yake Rais atapaswa kulivunja Bunge.
Hitimisho.
Namalizia kwa ule ule msisitizo nilioanza nao kuwa huu ni uzi wa swali tuu, "Jee Wajua Bunge Linaweza Kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. Lisipopokea Ripoti ya CAG, Bunge Linavunjwa Kwa Mujibu wa Katiba". Swali sasa ni nini kitatokea ndani ya hizi siku 7 kuanzia leo. Ila pia, kwa vile kuna matukio mengi ya ukiukwaji wa katiba nchini mwetu ambayo yanaachwa hivi hivi, sitashangaa na hili pia likipita, ila hili likitokea kwa Ripoti ya CAG Prof. Assad kutopokelewa na Bunge na kisha Bunge lisivunjwe, yaani liendelee tuu as if nothing has happened, then wenzangu na mimi mjue hawa wenzetu hawa, lao ni moja, mimi kama ilivyo kawaifa yangu huwa nasimama na ukweli, na kusimama na ukweli katika hili ni kusimama na CAG.

Mungu Mbariki Rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli ili azidi kutuongoza vyema, na ailinde, aisimamie na kutekeleza Katiba kama alivyo apa.

Mungu Ibariki Tanzania

Nawatakia Furahi Dei Njema

Paskali

Mwanafunzi wa Shivji ambaye ni Ki Shvji Kidogo

Mwaka wa Kwanza alifundishwa somo la LW. 101 na Tulia Akson (as she was then)

Supervisor wangu wa LL.B Dissertation ni Dr. Palamagamba Kabudi (as he was then)

Dean Wangu pale FoL wakati huo ni Dr. Ibrahim Juma (as he was then)

Just to name but few.
Update,
Bunge halivunjwi tena kwa sababu Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG, Prof. Mussa Assad, imewasilishwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba. Azimio lile la Bunge la kutokufanya kazi na CAG ni azimio batili, limepuuzwa. Ufafanuzi wa Spika kuwa Bunge halitapokea Ripoti ya CAG kama imesainiwa na CAG mwenyewe Prof. Assad, ila itapokelewa kama itasainiwa na mtu mwingine pia ni batili, na imepuuzwa, Ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bungeni imesainiwa na CAG, Prof. Assad, hivyo huu mjadala nimeufunga rasmi.
Hongera kwa Bunge letu kufuata Katiba.
P.
 

Attachments

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,001
2,000
Pascal Mayalla Ahsante kwa elimu ya katiba hasa kwa sisi ambao tuligusa tuu "Merchantile Law" kama sehemu ya somo la biashara. Swali kama ripoti imewasilishwa kwa Mh Raisi kimya kimya na wewe na mimi tulijua baada ya CAG kutoa PRESS RELEASE sasa CAG atajuaje kama Mh Raisi amewasilisha Bungeni au La kama uwasilishwaji wa kimya kimya utaendelea?
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
10,986
2,000
Wanabodi

Leo naendelea tena na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", Jee Uamuzi wa Bunge Kotafanya Kazi na CAG ni Uamuzi Halali, una maslahi gani kwa Taifa?, una maana kwa Bunge lenyewe, Kwa Rais, Kwa Ofisi ya CAG na Kwa Watanzania kwa jumla, nini kitatokea iwapo Bunge litaamua kutekeleza uamuzi huo. andamana nami.
 1. Utangulizi. Tangu nimejiunga JF, sijawahi hata siku moja kujivunia elimu yangu, lakini unapochambua mambo makubwa na mazito kuhusu mustakabali wa taifa letu, ni vizuri ukiweka kaji authority japo kidogo, kuonyesha hayo unayoyasema unatumia mamlaka gani, hii hoja ya kikatiba, hivyo kwa mara ya kwanza humu JF naomba kujivunia kuwa mimi Pascal Mayalla, ni mmoja wa wanafunzi wahitimu wa Sheria LL.B wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM aliyehitimu mwaka 2007, japo kiwango changu ni just a PASS tuu, lakini Shahada yangu ni "With Honours" na somo pekee ambalo nilipata alama za juu za A+ ni somo la LW 100: Constitutional Law, lililokuwa likifundishwana Prof. Issa Shiviji, hivyo hapa naona mnione kama hapa mnapata dose kutoka kwa Ka Shivji fulani kadogo
 2. Tena mwaka wetu wa kwanza, kipindi chetu cha kwanza kilikuwa LW 101 tukifundishwa na ka teacher kasichana karefu,kembamba, cheusi chenye baby face, wakati huo kakionekana kama katoto fulani cha form six, sasa sisi watu wengine tumesoma ukubwani, vitoto vyeusi ndio ugonjwa wetu, basi nilikuwa silielewi kabisa somo lake, mwalimu akiingia kufundisha wewe macho yako ni kwa mwalimu badala ya ku concentrate na masomo, naomba nililitaje jina la kaalimu hako wakati huo maana sasa.. hayo tuyaache,
 3. lakini kitendo cha kufundishwa na waalimu kama Prof. Shivji, na kupata A+ somo lake, nina haki kabisa ya kujitamba nami ni bingwa wa Katiba kama Shivji na Kabudi, hivyo ninavyoandika hapa, usikute hata Bunge wenyewe hawajua kuwa kukataa kupokea Ripoti ya CAG katika muda uliopangwa na Katiba utasababishwa Bunge livunjwe, Usikute hata rais Magufuli, saa hizi yuko busy ziarani Mtwara kuwapooza Chingas na maumivu ya Korosho, hivyo na yeye hajui kuwa atapaswa kulivunjilia mbali Bunge hili ndani ya siku 7 zijazo, iwapo litakataa kupokea ripoti ya CAG, kufuatia Azimio lao batili la kutofanya kazi na CAG Prof. Mussa Assad.
 4. Huu ni mfululizo wa makala elimishi kuhusu Katiba ya Tanzania. Japo Katiba ni kakitabu kadogo tuu ka kurasa 112, na kameandikwa kwa lugha mbili za Kiwahili na Kiingereza, lakini kukasoma na kukaelewa, kunataka kiwango fulani cha uelewa, na Katiba halisi yenye usahihi ni ile ya Kiingereza, ile ya Kiswahili ina makosa mengi tuu, sasa kwa vile baadhi ya viongozi wetu inasemekana lugha ya Kiingereza ni tatizo, na waheshimiwa Wabunge wetu baadhi ni darasa la saba, na wengine ni form 4 hadi Ph.D lakini kwa baadhi ya mambo wanayosema na kufanya, hata darasa la saba wana afadhali.
 5. Kitendawili cha Azimio batili la Bunge kutofanya na CAG Prof. Mussa Assad, kitatenguliwa rasmi ndani ya siku 7 zijazo. Aliyepanga kitendawili hicho lazima kitenguliwe ndani ya siku 7 zijazo sio mimi, bali ni Katiba ya JMT ya mwaka 1977 ambayo ime weka siku za Ripoti ya CAG kukabidhiwa Bungeni. Kuna msemo usemao numbers don't lie, kitendo cha Katiba ku prescribe siku za ripoti hiyo kukabidhiwa Bungeni ni ili kumzuia rais asije kuikalia ripoti hiyo hata kana ni adverse vipi, ripoti ikiishakabidhiwa kwa rais, rais anatakiwa kuikabidhi ripoti hiyo Bungeni ndani ya siku7, tena ripoti hiyo inatakiwa kukabidhiwa hivyo hivyo na sahihi ya CAG. Katiba ina maana yake kuitaka ripoti hiyo ikabidhiwe Bungeni ndani ya siku 7, na haumpa rais mamlaka ya kuchagua ama aikabidhi ama asiikabidhi, Katiba imeeleze rais akiishapokea Ripoti ya CAG, atanatakiwa kuikabidhi Bungeni ndani ya siku 7 zijazo.
 6. Ingekuwa kikao cha Bunge kimeanza wiki iliyopita, siku ya leo ndio ingekuwa siku ya mwisho ya kukabidhiwa kwa Ripoti ya CAG Bungeni kwa mujibu wa katiba, ripoti hiyo inatakiwa iwe imekabidhiwa Bungeni ndani ya siku 7 za kikao cha Bunge, baada ya kukabidhiwa kwa rais. Ripoti ya CAG ilikabidhiwa kwa rais Machi 28, 2019, hivyo siku ya 7 ni leo tarehe 5, Mwezi April. Lakini kwa vile Bunge limeanza vikao vyake siku ya Jumanne tarehe 2 April, siku ya 7 ni Jumanne ijayo Tarehe 9, au wakitumia siku 7 za kibenki, yaani working days, then siku saba ni siku ya Alhamisi ijayo tarehe 11 April, 2019, Bunge lisipopokea Ijumaa Ijayo Tarehe 12 ya Mwezi huu wa April, 2019, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais atalivunja rasmi Bunge.
 7. Katiba pia imeeleza, kama rais asipoikabidhi ripoti hiyo ndani ya siku hizo 7, then CAG mwenyewe anaikabidhi Bungeni, na Bunge halikupewa option ya ama kuipokea ama kuikataa, Ripoti ya CAG ikiishafika Bungeni ni lazima ipokelewe mezani hivyo kugeuka kuwa a public document, Bunge lina uhuru wa kuijadili, au kuipuuza, lakini sio kuamua kuipokea au kutokuipokea, hivyo Tangazo la jana la Spika kuwa Bunge litaipokea Ripoti ya CAG, kama itasainiwa na mtu mwingine asiye CAG, likini akisainiwa na CAG, Prof. Mussa Assad, Bunge halitaipokea kwa sababu limepitisha azimio la kutofana kazi na CAG Prof. Assad, kumbe masikini Bunge letu na Wabunge wetu, hawakujua kuwa wamepitisha azimio batili, hawana uwezo wa kuamua wafanye kazi na nani, wasipoipokea Ripoti ya CAG Prof. Assad, rais anatakiwa kulivunja Bunge mara moja bila kuchelewa.Siku zote Ripoti ya CAG huwa unapokelewa Ikulu kwa mbwembwe na picha na taarifa toka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, huku jioni kwenye luninga na kesho yake kwenye magazeti, hii ikiwa ndio habari kuu, lakini Ripoti ya mwaka huu imepokelewa kimya kimya, kwa uzoefu wangu wa miaka 29 katika tasnia ya habari, najua picha zilipigwa na video zipo, ila ikaamuliwa iwe kimya kimya, hivyo by connecting the dots, kumbe ukimya huu ulikuwa na sababu, nyumba kubwa was tipped, uamuzi wa Bunge kuhusu CAG kabla haijatangazwa Bungeni, watu tukiwaambia humu kuna watu huwa wanajipendekeza mahali, tutaitwa kuhojiwa, lakini matokeo ya kujipendekeza huko, sasa yanaonekana wazi, Nyumba kubwa ikapokea Ripoti ya CAG kimya kimya, wakijua huo ndio mwisho wa ripoti hiyo, kumbe kesho yake CAG mwenyewe akaiweka wazi.
 8. Usikute wenzetu wale wameisoma Ibara ya 143 (4)ya Katiba tuu ya Kiswahili ambayo imeishia kusema maneo haya " (4) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atawasilisha kwa Rais kila taarifa atakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hii. Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho. Iwapo Rais hatachukua hatua za kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge". Kwenye katiba hiyo ya Kiswahili, iliishia hapo bila kusema nini kitatokea kama rais hataiwasilisha Ripoti hiyo Bungeni, ndio maana wakaipokea kimya kimya, na Bunge likatoa Azimio batili hata baada ya kusikia kuwa Ripoti ya CAG imeisha wasilishwa Bungeni.
 9. Lakini Kama Wabunge wetu makini, na Bunge letu Tukufu makini, wangeisoma Katiba ya Kiingereza, yenye kueleza nini nini kitafanyika kama rais hataiwasilisha Ripoti ya CAG Bungeni ndani ya Siku 7, then Bunge letu lisingepitisha Azimio Bandia, wala jana Spika asingetoa taarifa kuwa Bunge halitapokea Taarifa yenye saini ya CAG Prof. Mussa Assad, Kifungu hicho kwa Katiba ya Kiingereza kinasema "If the President does not take steps of submitting such report to the National Assembly, then the Controller and Auditor-General shall submit the report to the Speaker of the National Assembly"
 10. Katiba yetu kuna vitu imempa rais discretion ya kuamua ama kutoamua, mfano kusaini death warrant, rais yuko huru kusaini hikumu ya kunyongwa au kutosaini, lakini katika kupokea ripoti ya CAG, rais hana uhuru wa kutoipokea na akiisha ipokea hana uhuru wa kuikalia, ndio maana amepewa siku 7. Asipoikabidhi then CAG mwenyewe anaikabidhi na inakuwa a public document, sasa Bunge lijadili au lisijadili, hayo sasa ni ya Bunge siyo ya CAG, CAG anakuwa amaisha fanya kazi yake.
 11. Pia kaika uteuzi, rais yuko huru kumteua mtu yoyote katika nafasi nafasi ya yoyote, kwa sifa zozote au bila sifa zozote, kwa sababu zozote au bila sababu zozote, na rais anaweza kutengua uteuzi huo wakati wowote kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote, lakini kwenye utuzi wa nafasi za kiutendaji, katika imeweka sifa na vigezo wa uteuzi wa baadhi ya nafasi, na miongoni mwa nafasi hizo, ziko nafasi ambazo ni za kikatiba yaani maofisa waliolezwa ndani ya katiba sifa zao na vigezo vyao ambapo katika nafasi fulani, rais anatakiwa kumteua mtu mwenye sifa fulani, na uwezo wa rais ni kumtua tuu na sio kumtengua anapojisikia, watu hawa ni pamoja na Jaji Mkuu, Majaji, GAG, na Gavana wa BOT, watu hawa wana kinga ya kikatiba inaitwa security of tenure, rais anaweza kuwateua tuu, lakini hawezi kuwatengua.
 12. Ripoti ya CAG ni lazima isainiwe na CAG, rais hana uwezo wa kumuondoa CAG bila kosa, kusema Bunge limeonyesha udhaifu, sio kosa la kupelekea kutenguliwa kwa CAG kwa huo ndio ukweli bayana kuhusu Bunge hili hata wenyewe hawaupendi ukweli huu uwekwe bayana, lakini ukweli siku zote unabaki kuwa ukweli, hivyo bandiko hili litawasaidia wanasheria wetu wa Bunge kuwafungua macho kuwa pamoja na kupitisha azimio lao batili, ripoti ya CAG yenye sahihi ya Prof. Assad, lazima ipokelewe vinginevyo Bunge linavunjwa.
 13. Ripoti ya CAG inaitwa tuu jina la Ripoti ya CAG kwa sababu inatayarishwa na CAG na kusainiwa na CAG, ripoti hiyo ni lazima iwasilishwe kwanza kwa rais, ila kuipa mamlaka ya kirais, hivyo Ripoti ya CAG, ikiishakabidhiwa kwa rais, unageuka kuwa ni ripoti ya rais, inayoitwa Ripoti ya CAG, na kule Bungeni inaingia kama Ripoti iliyoka kwa rais kwa jina tuu la Ripoti ya CAG, Bunge halina mamlaka ya kumuingilia rais Ripoti yake ya CAG isainiwe na nani, wala halina mamlaka ya kutoipokea ripoti ya CAG kwa sababu hii ni ripoti ya rais, hivyo Bunge lisipopokea ripoti hii, rais kwa kutumia mamlaka ya Ibara ya 90 kifungu (c)
 14. Hivyo kama Tanzania tutafuata utawala wa Katiba, Bunge liko chini ya Katiba, linaelekezwa na katiba linaweza kufanya nini na haliwezi kufanya nini, kwa mujibu wa vifungu nilivyowakekea hapo, Bunge halina mamlaka ya kukataa kuipokea Ripoti ya CAG, wala Spika hana mamlaka ya kumuamuru rais Ripoti ya rais kwa jina la Ripoti ya CAG, isainiwe na nani, kazi ya CAG ni kufanya tuu ukaguzi, kutoa ripoti, kuisini na kuikabidhi kwa rais, baada ya kuikabidhi ripoti hiyo kwa rais, kazi yake imekwisha, lakini iwapo rais hataikabidhi Bungeni ndani ya siku 7, kazi ya CAG inaendelea, kwa CAG kuichukua Ripoti hiyo na Kuikabidhi kwa Spika, na kazi ya Bunge ni kuipokea na kuiwasilisha Mezani, Bunge halina jeuri ya kuikataa ripoti ya CAG et sijui mpaka isainiwe na nani, hivyo ndani ya siku 7 hizi ni lazima Bunge letu liipokee Ripoti ya CAG iliyosainiwa na CAG, Prof. Mussa Assad na hili halina mjadala, wasipofanya hivyo, ni Ijumaa ijayo itampasa rais kulivunja Bunge.
 15. Kama Raia wa JMT ataamua kufuata katiba, rais baada ya kuiopokea Ripoti ya CAG, haombwi kuiwasilisha Bungeni bali anaelekezwa, kwa Katiba katiba yetu inamheshimu sana rais na haimlazimishi kufanya jambo lolote. imempa fursa ya muda wa kutosha wa kukaa na ripoti hiyo akijiuliza aiwasilishe au asiiwasilishe, kule kuipokea kimya kimya ni dalili tuu ya awali, hivyo ili kumxuia rais wetu asiwe mnyonge kuwasilisha Bungeni kitu ambacho roho yake haitaki, then CAG ameelekezwa ataiwasilisha yeye Bungeni, hivyo hadi kufikia Jmatano Ijayo Saa 9:30 jioni muda wa mwisho wa Kiserikali, then Alhamisi Saa 3:00 asubuhi, CAG Prof. Mussa Assad atatinga ofisi za Bunge Dodoma na Ripoti yake Mkononi na kufuatia hizi figusu figisu, hadi ile dispatch book hata beba mesenja, bali atabeba CAG mwenyewe, na mtu wa kupokea ni Spika mwenyewe au Naibu wa Spika, ndio watasaini dispatch book ya CAG ili wasipoiwasilisha mezani siku hiyo hiyo, kesho yake Rais atapaswa kulivunja Bunge.
Hitimisho, namalizia kwa ule ule msisitizo nilioanza nao kuwa huu ni uzi wa swali tuu, "Jee Wajua Bunge Linaweza Kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. Lisipopokea Ripoti ya CAG, Bunge Linavunjwa Kwa Mujibu wa Katiba". Swali ni nini kitatokea katika siku 7 hizi. Ila pia, kwa vile kuna matukio mengi ya ukiukwaji wa katiba nchini mwetu ambayo yanaachwa hivi hivi, sitashangaa na hili pia likipita, ila hili likitokea kwa Ripoti ya CAG Prof. Assad kutopokelewa na Bunge na kisha Bunge lisivunjwe, yaani liendelee tuu as if nothing has happened, then wenzangu na mimi mjue hawa wenzetu lao ni moja, mimi kama ilivyo kawaifa yangu huwa nasimama na ukweli, na kusimama na ukweli katika hili ni kusimama na CAG.

Nawatakia Furahi Dei Njema

Paskali
Mwanafunzi wa Shivji ambaye ni Ki Shvji Kidogo
Mwaka wa Kwanza alifundishwa somo la LW. 101 na Tulia Akson (as she was then)
Supervisor wangu wa LL.B Dissertation ni Dr. Palamagamba Kabudi (as he was then)
Dean Wangu pale FoL wakati huo ni Dr. Ibrahim Juma (as he was then)
Just to name but few.
hii ni nyundo, mkuu.
kudos!!
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,489
2,000
Ni uchambuzi wa kisomi. Cha ajabu kuna wanaoponda hata sielewi kwa nini. Tunajua kama ulivyo weka kufuatwa kwa katiba ni jambo lingine hasa kwa watu ambao wanafikiri mawazo na maneno yao ndiyo katiba.
Jiulize CAG alikosea kusema Bunge lina Udhaifu-wakati maelezo ya supika hayaendani na wajibu wa Bunge kikatiba. Sasa wale wanasheria wa Bunge wanafanya kazi gani au tuonyeshe ubabe kwanza ndio mengine yafuate.
Katiba na sheria sio vitu vya kuchukulia poa hata siku moja-naambiwa huwa wanafundishwa jinsi ya kutafsiri hayo madude hivyo kujua kingereza na kiswahili tu haitoshi.
Mwisho kabisa P.apunguze mbwembwe kwenye issue kama hizi umekula para za kutosha kueleza degree yako ya UDSM sijui nani kakufundisha. Inatosha tu kusema una LL.B ya UDSM. Hata hivyo endelea kutuelimisha kama afanyavyo TL tutakuelewa tu
.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom