Wanasheria mtusaidie, Spika anaposhindwa kusimamia Azimio lililopitishwa na Bunge, nini kitatokea?

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Mh. Spika alisema hawatafanya kazi na Prof. Assad ila si ofisi ya CAG. Akaongeza kuwa kama ripoti itakuwa na saini ya Assad hawataipokea (lakini leo imepokelewa ikiwa na saini hiyo). Wanasheria mlio humu naomba ufafanuzi juu ya hili-Kukiuka azimio lililopitishwa.

Kwa hili lililotokea leo linatukumbusha kutafakari hoja zifuatazo:
-Ni nini wajibu wa mwanasheria mkuu wa serikali katika kutafsiri katiba na sheria pale zinapoleta mkanganyiko?
-Ni nini wajibu wa kila mbunge? Je, akubali kufuata yote yanayosemwa na kiti cha spika?
-Je, wale walioadhibiwa kwa kumuunga mkono Assadi, adhabu zao zitatenguliwa?

TUJIANDAE KUPATA TUKIO JIPYA LA KUPOZA MOTO HUU UNAOFUKUTA!
 
Sawa hapo sasa ndiyo anatuthibitishia kuwa yeye Ndugaye ndiyo dhaifu kuliko
Mkuu wajua hapa spika anapewa hii report na Rais, so akigoma kupokea basi anakua anamgomea Rais, kitu ambacho asingethubutu kwa jinsi anavyomuogopa na kumnyenyekea.

In God we trust
 
Na Professor Assad alisisitiza na kukazia kwenye mkutano wake na waandishi habari kwamba.....
Neno DHAIFU ni neno la kimkakati, na pia yeye pamoja na ofisi yake hawato acha kulitumia neno hilo DGAIFU
Hapo ni jino kwa jino

In God we trust
 
Azimio Batili na ufafanuzi batili, usipotekelezwa, hakuna kosa lolote kikatiba kwa sababu katiba imefuatwa. Lingetekelezwa ndipo kungetokea matatizo ikiwemo kuvunjwa kwa Bunge.
P
Sawa lakini nini kifanyike going forward kuepukana na matukio kama haya yanayosababisha nchi nzima kuwaka moto pasipo sababu za maana wala tija?!, Spika should have known from the word go kwamba azimio alilolisimamia halikuwa na mashiko hata kidogo; na kwamba alikuwa anapandisha political temperatures nchini bila sababu mpaka watendaji kina Moroto wanakiuka maadili ya kazi zao kwa kuropoka sentensi zisizo na weledi!
 
Sawa hapo sasa ndiyo anatuthibitishia kuwa yeye Ndugaye ndiyo dhaifu kuliko

In God we trust
Hivi Mkuu unadhani Ndugai haijui kua ni dhaifuest?
Anajijua fika, sema tu hua anakasirikaga kama akiambiwa hadharani
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom