Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
Najua nitarushiwa mawe! Nimejiandaa kwa hilo. Nimeamka na hang over nikitafakari nchi yangu niipendayo inaelekea wapi. Nimegundua wanasheria they have real fuc..k..ed our country. Ukianzia na Chenge Andrew yule ni mwanasheria, Hosea wa PCB amesomea sheria, Mzee Msekwa amesomea sheria, Mzee Sitta aliyeingia kwa mbwembwe kwenye usipika kumbe naye ni msanii ni mwanasheria, wale jamaa walikuwa wana sign mikataba hewa ya deep green ni wanasheria tena wazawa wa nchi hii hii....
Lawrence Masha naye alikuja na issue yake ya kimitego na vitambulisho lohh the list goes on
whats wrong na wanasheria hivi hawana uchungu na nchi yetu?
Ni wanataaluma wa fani ipi ndio unafikiri ni wazuri? Leta data kutoka kwenye Baraza la Mawaziri! Nionavyo suala sio UANASHERIA, bali ni la mtu binafsi! Ndio maana tuna mifano mizuri ya Wanasheria makini kama akina Dk Slaa, Mwakyembe, Halima Mdee na Tundu Lissu! Tukivuka mipaka tunaye Rais Obama ambaye ni mwanasheria mahiri na mtu maarufu sana! Au ulikuwa unamaanisha wanasheria wa Tanzania ndio tatizo?