Najua nitarushiwa mawe! Nimejiandaa kwa hilo.
Nimeamka na hang over nikitafakari nchi yangu niipendayo inaelekea wapi. Nimegundua wanasheria they have real fuc..k..ed our country. Ukianzia na Chenge Andrew yule ni mwanasheria, Hosea wa PCB amesomea sheria, Mzee Msekwa amesomea sheria, Mzee Sitta aliyeingia kwa mbwembwe kwenye usipika kumbe naye ni msanii ni mwanasheria, wale jamaa walikuwa wana sign mikataba hewa ya deep green ni wanasheria tena wazawa wa nchi hii hii....
Lawrence Masha naye alikuja na issue yake ya kimitego na vitambulisho lohh the list goes on
whats wrong na wanasheria hivi hawana uchungu na nchi yetu?
Hapa sijui umewachukulia wanasheria wana haribu nchi hii kwa mtazamo upi, kwa mimi mtazamo wa kwanza ni ile mwanasheria kufanya kazi yake ya sheria kwa kusimamia mambo yanayohusu sheria mfano andrew chage, pili ni ile mwanasheria kuteuliwa kushika wadhifa mwingine zaidi ya sheria mfano spika sita.
Nchi hii imefuata sana mfumo na taratibu za kiingereza kupendelea kuwapa wanasheria kuongoza mambo mbalimbali kama tume.kamati, nk wakiamini kuwa kutokana na taaluma zao watatenda haki na kwa mujibu wa sheria bila upendeleo, na ndio maana mara utasikia tume ya jaji fulani, tume ya uchaguzi, msajili nk nk.
Sasa hiii yote inapelekea wanasheria kuonekana ulivyosema. hili la mwanasheria kupewa wadhiwa mwingine siwezi kuliongelea sana. La mwanasheria kama mwanasheria hili unapaswa kujua kuwa kazi ya mwanasheria hasa katika mikataba ambayo ndio tabu kubwa nchi hii ni kuyaweka kisheria mambo ambayo pande mbili zimekubaliana, watu wa maswala ya tender, procurement wao ndio wana bargain power kisha wakimaliza wanakwenda kwa mwanasheria kuyaweka hayo walio kubaliana kisheria.
Sio kama nawatetea wako safi, hapana,mikataba mingi iliyo leta utata iliingiliwa na wana siasa wakafanya maamuzi yao kisiasa, mwanasheria anawajibu wa kushauri pia lakini tumeona hivi majuzi wakati wa kikao cha bunge jinsi ilivyokuwa ngumu kuwashauri wanasiasawakati wanapitisha sheria ya mifugo, kila mwanasheia akisema hivi wabunge wana kataa.
Kwa mfano hivi karibuni kamati ya akina zito ilipendekeza inunuliwe mitambo chakavu ya dowans serikali ingekubali unategemea mwanasheria atafanyanini, wanasheria ni binadamu wanamabungufu yao.
SWALA KUONGOZA KUFUJA MALI ZA UMMA BASI WATU WA PROCUREMENT WANAONGOZA