Wanasheria Mnatungusha Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria Mnatungusha Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masanja, May 27, 2009.

 1. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Jamani mimi kuna jambo linanitatiza naomba tulijadili. Kwa ambao tumefuatilia mwenendo wa hii vita ya ufisadi kila mtu anasema kwamba kesi zipelekwe mahakamani kwenye vyombo vya sheria watuhumiwa wawajibishwe. Kifupi kila mtu..fisadi na asiye fisadi, mkulima na mfanyakazi, mtawala na mtawaliwa..wote tunaamini kwamba sheria ndo suluhu ya huu ufisadi! Lakini cha kushangaza ni kwamba hizi kesi ambazo zinahusu mabillion ya pesa za walipa kodi zimekuwa zikitupiliwa mbali kila zikifikishwa pale mahakamani Kutokana na makosa madogo madogo "technicalities".

  Maoni na maswali yangu ni haya:

  1. Iweje hizi technicalities ziwe ni kwenye kesi kubwa kubwa tuu zinazohusisha pesa nyingi na wala siyo kesi za walalahoi akina Babu Seya na wengineo? Mfano Liyumba kaachiwa..fuatilia kesi za akina Yona, Mramba et al..issue ni ile ile..hati za mashtaka zinakosewa kuandikwa! na angalia pesa iliyo-involved! Ina maana kweli watu hawajifunzi kwa kosa moja? Tumeona mikataba ya Buzwagi, IPTL, TANESCO, DOWANS name them..Mikataba inaacha maswali mengi kuliko majibu. Hawa watu walisoma vyuo gani????? hata kama ni siasa na kulazimishwa..hawakufundishwa hata minimum decency ya neno ethics?

  2. Ina maana wanasheria wetu kweli hawawezi kudraft document isiyo na makosa ambayo inaweza kukubaliwa mahakamani? Labda tuambiwe nani anahakiki documents kama hizi kabla hazijapelekwa mahakamani? siwezi amini kwamba hati ya mashtaka ya billion 225 itapitiwa na legal officer..bila kuhakikiwa na principal State Attorney. Ni vigumu kuamini.

  3. Is it possible kwamba haya makosa yanafanywa kimakusudi kuwanusuru wahusika wakati huo huo wakituridhisha sisi walalahoi kwamba sheria ndo imewaachia wahusika? Na ni nani atawawajibisha hawa wanasheria uchwara? No way..somebody must answer for this mess!

  4. Ofcourse mahakama ina haki na wajibu wa kumuachilia mtuhumiwa kama hati ina makosa, lakini hebu tujiulize..what is happening katika huu mchezo wa kupelekana mahakamani?

  5. Kama wanasheria wetu hawawezi ku-prosecute kesi kubwa kama hizi,je kuna haja ya kutafuta independent prosecutors kuendesha hizi kesi?

  6. NAJUA KUNA WANASHERIA WANA INTEGRITY. Lakini lazima tufike mahali tushtuke..this is too much! Ina maana wanasheria ofisi za serikali wote ni vilaza? who does the hiring then? Hapana nahisi wananchi tunachezewa akili na wala nchi.

  HAIWEZEKANI TUDANGANYWE kwamba sheria zipo harafu hao hao wahusika wanacheza na hizo sheria sisi tunaonekana wajinga. Siyo wote tumebahatika kusoma sheria. LAKINI naamini mtu aliyesomea kazi yake, huwezi peleka document mahakamani bila kuihakiki! Ingekuwa ni typo error..ingekuwa kingine..but for Heavens sake..hapa tunamtuhumu mtu kutuibia kama taifa more than 225 billions! and we let the guy scot free..simply because we cant draft a proper charge sheet? Mungu atunusuru!
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tundu Lisu amekuwa msaada sana kwa jamii kuhusu mambo mbalimbali ya kupindisha sheria.Sasa natoa wito kwa wanasheria msaidie watu masikini wapate Elimu kwa kuwasaidia kupinga upandaji holela wa ada katika vyuo vya elimu ya juu hasa vya binafsi.Mtakuwa msaada sana kwa jamii mkifanya hivyo hasa kwa mambo mengine yanayohasi maendeleo ya jamii yetu ya Tanzania.Natoa hoja.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ingawa swala zima linayumkinika, presentation yako mbovu, ukiwauliza "kwani mpaka mlipwe" wakakujibu "kwani ulitusaidia kulipa ada tulivyokuwa chuoni?" utawajibu vipi?

  Inabidi kutumia nguvu ya ushawishi kuwaonyesha kwamba hata kama hawaamini katika wajibu wa kutoa huduma hizi (some frankly don't believe in charity/ church work) itakuwa kwa faida yao wenyewe wakiamua kufanya hizi kazi.

  Kuna watu wanajulikana kwa kupitia kesi hizi za bure na baada ya hapo inakuwa kama free advertisement, wanapata wateja wengi, wanajenga jina, wanajionyesha kuwa altruistic (a shame really, but hey, it is a win win situation)

  Kwa hiyo inabidi waonyeshwe kwamba hata kama hawaamini katika kutoa huduma bure, the PR effect could be quite worthwhile.

  Katika mfumo wa soko huria ni mwiko kumuuliza mtu "kwani lazima ulipwe?"
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mimi naona kesi nzuri ingekuwa ya kuilazimisha loans board itoe mikopo 100% na bila ya masharti kwamba division 1 na two ndio wanapewa au education , science na udaktari ndio wanapewa. Kwa sababu ni mkopo wa elimu hutakiwi kutoa kwa percentage mwanafunzi apewe hela yote kila mwaka ili amalize elimu yake basi.

  Sheria iko very clear kigezo kilichowekwa kisheria ni kuwa mtu awe mtanzania na apate admission kwenye higher learning institution hata nje ya nchi sio necessarily Tanzania nyingine zote ni siasa na longolongo za loans board.
   
 5. C

  CHAUMBEYA Member

  #5
  Aug 25, 2009
  Joined: Nov 15, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama unahitaji msaada wa bure wa sheria nenda Kitua cha Haki za Binadamu (LHRC) pale kijitonyama au Kinondoni. Pia waweza kwenda Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) ambao ofisi yao iko IPS Building Ghorofa ya 9. Huko watakusikiliza na kukupa ushauri wa kisheria na kama kesi yako ina merit basi utapewa mtu wa kukuwakilisha mahakamani kama Strategic Litigation.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Najua nitarushiwa mawe! Nimejiandaa kwa hilo.

  Nimeamka na hang over nikitafakari nchi yangu niipendayo inaelekea wapi. Nimegundua wanasheria they have real fuc..k..ed our country. Ukianzia na Chenge Andrew yule ni mwanasheria, Hosea wa PCB amesomea sheria, Mzee Msekwa amesomea sheria, Mzee Sitta aliyeingia kwa mbwembwe kwenye usipika kumbe naye ni msanii ni mwanasheria, wale jamaa walikuwa wana sign mikataba hewa ya deep green ni wanasheria tena wazawa wa nchi hii hii....

  Lawrence Masha naye alikuja na issue yake ya kimitego na vitambulisho lohh the list goes on

  whats wrong na wanasheria hivi hawana uchungu na nchi yetu?
   
 7. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ukiwowa mwanasheria nayo shida
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  I hate that professional....binti yangu hatosemea hiyo!
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni njaa na tamaa ndizo zinawaponza hawa watu...
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Masanilo, usilaumu wanasheria, walaumu wale manaoconcieve hizo plans dhalimu na kuzitekeleza mwanasheria ni mtu wa mwisho na mara nyingi wanakuwa side steped. Kwenye utaratibu wa kawaida kuna procuring process ambayo haiko chini ya mwanasheria, kuna tendering process ambayo wanasheria wanaandika minutes tu hawafanyi recommendations ( eti ni technical), baada ya hapo ndo mkataba unatayarishwa na wanaheria ambao hawakuwepo kwenye negotiations.

  Baada ya hapo yanaanza malipo, kuna internal auditors ambao kazi yao pia ni kucheki hivyo vitu kama vimepita process yote ya procurement kama sheria inavyotaka, wao wanapitisha tu.

  Sasa hapo mwanasheria ana kosa gani?

  Tatizo ni kuwa Watanzania wote hatuna morals, tunataka hela haraka bila kufanya kazi ili wote tuendeshe vogue, tuwe na ghorofa watoto wasome UK, USA, tule movenpick, tushop nje ya nchi , twende vocation South Africa bila kujua kuwa tunafanya hivyo kwa hela ya walipa kodi.
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Masa, please hate a particular wrong doer not all of them, some are jolly good and clean
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kuna mwanasheria mmoja mstaafu, niliongea naye hili! Alikubaliana nami kuwa hii fani imeingiliwa vijana wanamaliza sheria UD wanataka kesho yake waendeshe BMW na Mercedes! waishi nyumba za kifahari mzee aliendelea hawa watu wanafanya kazi za kisiasa zaidi kuliko kufata ethics za kazi.

  Wanasheria wa kitanzania wako tayari kupindisha chochote mradi apate 30% bila kujali maslahi ya nchi wala watanzania wenzake. Mikataba mingi wanaandika na hata huweza kubadili kulinda wanasiasa.....
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Fidel, Tatizo ni tamaa, kama una hela ya kutosha ugali na maharage, halafu unaiba ili uende lunch movenpick au Kempiski hiyo sio njaa hiyo ni tamaa. Kama una usafiri bado unataka mwingine wa hali ya juu hiyoo ni tamaa. Kumbuka:

  There is a sufficiency in the world for man's need but not for man's greed.
  Mohandas Gandhi
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Masa nisamehe bure, kwenye bold naomba iwe na isomeke "hawa watu ( kama wapo) wanafanya kazi na wanasiasa na wanataaluma wengine bila kufuata ethics za kazi. Baadhi ya wanataaluma wa kitanzania wako tayari kupindisha chochote mmradi wapate.... bila kujali maslahi ya nchi wala watanzania wenzao".
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Lawyers are Monsters.....................
  sio wote
   
 16. bht

  bht JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  anakuchuna au tatizo liko wapi???
   
 17. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  don't hate the game...hate the player.!!!!
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nitajie wanasheria 4 walio madarakani ambao wanatetea maslahi ya nchi! You have my 10 sent ukiweza
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ongeza dau bana.....................
   
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tuanzane na wanasheria walio madarakani . Ni akina nani?
   
Loading...