Wanasheria, mnaichambuaje hii kitaaluma yenu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria, mnaichambuaje hii kitaaluma yenu?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mcheza Karate, Jul 2, 2011.

 1. Mcheza Karate

  Mcheza Karate JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 691
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  Wadau naomba mnisaidie hii. Nilisimuliwa tu wakati naanza maisha ya ukanda huu wa pwani na nikaona baadaye kwa rafiki yangu. Sijui "mila" au utaratibu wa "sheria za nchi" au "sheria za uislamu" hasa upande huu wa pwani utakuta mwanaume anamtaka binti na wakaelewana safi kwa ridhaa yao na binti sio mwanafunzi au mke au mchumba wa mtu lakini baadaye wanakuja ndugu zake wakati mko "faragha" wanakuja na kusema wamekufumania. Hivyo kutakiwa binti kumwoa au kulipa fidia ya pesa Je huu mbona utaratibu ambao ndo mosi nimeuona ukanda huu tu wa pwani je ni sheria ya nchi, sheria ya dini au mila tu? Naomba mnielekeze kisheria zaidi maana hili ni jipya kwangu.
   
 2. n

  ng'wana mlingwa Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kaka hili suala ni mila na si sheria, pili hili sula halipo mikoa ya pwani tu kama unavyodhania, mimi ni msukuma na nimekuliwa usukumani kabisa na nimeshuhudia ukikutwa unafanya mapenzii au ktk hali ya kimapenzi na binti wa watu wazee wa kijiji kwa kisukuma "WANANZENGO" wanakulazimisha umuoe yule binti whether you want it or not. lakini the bottom line is sio sheria, na wala jambo hili halipo mikoa ya pwani peke yake.
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Unamaanisha ndoa za mkeka? Nilishamsikia waziri wa nchi ofisi ya Rais katiba na utawala bora Zanzibar akilalamikia hili jamo mwaka jana kuwa nyingine zikufungwa mpaka katika kituo cha polisi. Ofisi ya Kadhi Mkuu, nayo ililalamikiwa kwa hili. Ndoa zilizofungwa kimila zinatambulika na sheria ya ndoa. Ili zitambulike kisheria inabidi zifungwe kuwa kufuata desturi na taratibu za mila husika. Kwa kaida sheria za kiislamu zinatambulika kama moja ya sheria za mila na desturi zetu.

  Ndoa hali ya kiislamu ni lazima ifuate mashari yafuatayo.
  1. Anayeoa na anayeolewa lazima wakubali kuoana kwa hiyari yao wenyewe.
  2. Lazima walii (wazazi au walezi) wa msichana waidhinishe hiyo ndoa.
  3. Lazima kuwe na mashahidi wawili waadilifu katika hiyo ndoa.
  4. Lazima isomwe khutba ya kuozesha.

  Kama kijana na msichana walishaishi pamoja na kuzini inabidi kuwe na sharti jinginne la kuwatenganisha kwa muda ili kuwa na uhakika kama msichna ana mimba. Katika kipindi hicho inabidi wote warudi kwa ala kwa kuomba msamaha, kutubu na kutia azma ya kutorudia, kuacha maasiya na kufanya mema mengi. Yote haya yakitimizwa ndoa inaweza kufungwa na kutambuliwa kisheria baada ya kusajiliwa na sheria ya ndoa.

  Kwa vile ndoa ni muunganino wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke, sidhani kama ndoa za mkeka zinatambulika kisheria kwa sababu ni za kulazimishana. Makubaliano ya hiari ni element muhimu sana kwenye ndoa za aina zote, ziwe za kawaida au za kimila.

   
 4. mbasajohn

  mbasajohn JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hizi ndoa naamin hazkubalik wala kutamblka kisheria unless kuwe na consent ya wote wawili yaan wanandoa kwa sababu marriage n legal contract na ili mkataba wowote ukubaliwe lazma kuwe na makubaliano huru na ya hiari.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nili RED naona umechanganya sana na kupotoka kabisaaaa.

  USAHIHI: Kama watu hawa walizini ni ikithibitika basi inabidi Sheria za Mola dhidi ya wazinifu zichukue mkondo wake. Na baadae kama wakitaka kuoana basi taratibu za ndoa ya kiislamu zitasimama.

  Na kama Binti alipanda ujauzito basi inabidi binti asubiriwe mpaka ajifungue wakti wakiwa wametenganishwa na baada ya kujifungua basi hukumu za Mola dhidi ya wazinifu zitachukua mkondo wake na baadae kama watataka kuoana basi taratibu zitafuatwa kama ulivyo ziainisha.

  NAREJEA KWENYE SUALA au mada kuu.

  Tanzania kuna aina Tatu za ndoa. yaani kuna ndoa za Kidini, Ndoa za Kiserikali na ndoa za kimila.

  sasa tukizungumzia za Kiislam hakuna kitu cha namna hiyo kwani ni lazima wote wawili yaani muolewaji na muoaji lazima wakubali kuoana bila kushinikizwa na mtu. Na mmoja wao akikataa hakuna ndoa hata kama mzazi wa kike akilazimisha. Wote wakikubali basi utaratibu wa ndoa kama ulivyoainishwa unafuatwa.

  Upande wa ndoa za kimila. Nafikiri hili linaingia kwani kila kabila lina taratibu zake katika kuozesha.

  Upande wa Kikristu siwezi lisemea kwani mambo hapa huwa kuna taratibu za kanisa husika katika kuitangaza ndoa hiyo, kupata mafunzo ya ndoa na hatimaye kuoana chini ya usimamizi wa Kiongozi wa dini husika.

  Upande wa Sheria za ndoa za kiserekeli kuna taratibu za kisheria zilizobainishwa wazi ndani ya katiba.


  Nasriyah Saleh Al Nahdi ( Ummi Majjid)
  Mapumzikoni Unguja
   
Loading...